Nani aliyetulaani wana wa mkoa wa Mara?

Nani aliyetulaani wana wa mkoa wa Mara?

Wanavuna wanayopanda. Ubinafsi ni tatizo sana
Kuna mmoja nilinunua gari lilikuuma hadi akaenda ikwangua na jiwe kumbe watu walimuona asee... nilichomfanya hatonisahau ktk maisha yake
 
Me sio bwana mdogo wako,acha maskhara,heshima tu ifuate mkondo wake,kwani tukiishi pasipo matusi,kudharauliana na kuvunjiana heshima kuna ttz gan?.
HOJA ULIYOTOA NA UNAYOTAKA NIIJIBU NI IPI?.
I have told you,and i can dare to repeat Once more,I'm not here to discuss People,bring Ideas On the table we will sail in the same table!!!.
Akili zako fupi kama haujadili watu unatafuta nini hapa? Hebu kimbia haraka
 
Eti mwanaume mzima unalalamika watu wa Mara wana wivu, seriously?

Aisee kwa style hii lazima utuchukie tu.

Mwanaume mwenye tabia za kike hawezi kuwapenda watu wa Mara!

Mwingine anaongelea uchawi, watu Mara ni washirikina kushinda watu wa shinyanga, tanga, Rukwa (sumbawanga)? Yani ukisema tuipange mikoa yenye ushirikina Mara ni ya mwisho kabisa.

Watu wa Mara hawana time for bull shit. Ukizingua anakuharibu physically, uchawi sio sehemu ya maisha yetu!

Mara kuna wakurya, wajaluo, wajita, wazanaki na makibila mengine madogo madogo kibao. Sasa kuna wapuuzi wakisikia Mara wanajua ni wakurya tu, educate your self!
 
Wewe ungesema watu wa Musoma vijijini hawaelewani. Maana hao wote kwao ni Musoma Vijijini.

Muhongo, Maswi, Werema na Mkono wote ni wa Musoma vijijini na mbunge wao alikua Mkono kabla hawajaligawanya jimbo hilo.

Watu wa Serengeti huna haja ya kuwalaum maana serikali mdio haikufanya mgawanyo sahihi wa rasilimali, Mbuga iko Serengeti ila makao makuu yakawa Arusha.

Watu wa Arusha wakaendelea kwa kutumia mgongo wa watu wa Serengeti.

Tatizo la mkoa wa Mara ni unequal distribution of resources. Mkoa wa Mara ni mkoa tajiri, una dhahabu na madini mengine karibu kila kijiji, una ziwa, una mbuga kubwa kuliko zote Afrika.

Cha ajabu, Dhahabu yote haiwasaidii watu aa Mara, migodi ya kihuni kama Meremeta imewaibia wana Mara, North Mara kila mtu anajua, Serikali ikaua viwanda vyote vya samaki, wao watauza wapi samaki? Wajita na wakwaya wamebakia kua na majungu tu maana hawana kazi nyingine ya kufanya.

Serengeti haiwasaidii wana serengeti, mbuga inayoingiza 80% ya mapato ya utalii Tanzania, cha ajabu wanaofaidika nayo ni watu wa Arusha na Kilimanjaro. Hata chuo kimoja cha utalii cha serikali cha ngazi ya cheti serikali haikuwajengea wakazi wa serengeti, vyote viko Arusha na Kilimanjaro.

Watu wa Mara hasa Serengeti na Tarime wana ardhi nzuri ya kulima, wanalima misimu 2 kwa mwaka lakini hawana masoko, wakitaka kuuza Kenya serikali haitaki, wanakua hawana namna zaidi ya wizi wa ng'ombe.

Serikali ndio imechangia kuua mkoa wa Mara. Watu wa Mara inabidi tuwalaum wenzetu waliotangulia kupata fursa kisha hawakuendeleza mkoa wetu.

Watu wengone wakipata uwaziri wa maji tu mikoa yao inakua na maji hadi ya kuogeshea kuku, urais ndio balaa.

Watu wa Mara tujifunze. Ukipata fursa itumie.
wa kuthibitisha Roho mbaya sikuizi mkoa wa mara unaanzia Bunda, kwanzia serengeti ni Simiyu eti... mwaka jana nmepita nmesikitika sana...
Wapoti mi naona Tukinukishe tu hakuna namna
 
mkoa wa mara mtauelewa pakinuka siku[emoji23]..... Mara ni mahala ambapo Kuna Marshal Tribes hapawezi kupendeza kindezi ndezi kama zanzibar
 
Na wala Mara sio wazubaifu kihivyo ila ni kama alivosema mchangiaji hapo juu,watu wengi wa Mara wakifanikiwa kidogo tu wanakimbilia kuwekeza Mwanza na mkoa wao unabaki bila fursa za mzunguko wa fedha siku hadi siku. Inasikitisha sana
Ndiyo wanakimbia majungu na kurogana , utasikia yego yego [emoji28] [emoji28] [emoji28] [emoji28] [emoji28]
 
Nilikuwaga na demu wa kikurya dadadeki...nilikoma mwenyewe siwezi kurudia tena
 
Wale watu ni development haters. Wao kwa wao kurogana ni nje nje. Wageni wanaofanya kazi kule wanapata shida sana ktk uwekezaji sababu ya ushirikina na majungu/fitna.
Jenga kijumba chako dar Mungu wangu wanahamia wote majungu sasa kwa mke wa ndugu yao usiombe uwe kabila jingine utakoma hasa wajita + wakerewe hawachelewi kukutumia mamba [emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23]
 
Nawashukuru kwa michango yenu ,ila kuna mambo nataka niyaweke sawa.Welema anatokea Kijiji kinaitwa kongoto wilaya ya Butiama,Mhongo anatokea Majita ,Mkono anatotokea Butiama na Eriakimu Maswi kwao ni tarime,Uliyeongelewa wakurya utakuwa hujafanya utafiti vzr,Hakuna kabila lenye husuda kwa mkoa wa Mara kama Wajita yego jaji, Suala la watu kujenga kwao inatengemeana ila siyo mambo ya kurongwa .Nenda kwao Jaji Warioba huwezi amini kuwa ndipo anatokea,Lkn kwao mke wake moshi mambo yako vzr,Hivyo hivyo kwao welema alijenga msonge tena baada ya wazee kukomalia kuwa huwezi kufikia kwenye nyumba mama yake mzazi,Kwahiyo suala la kujenga hata wanawake tunaoa wanaweza kuchangia mwanaume kushindwa kuwekeza nyumbani.
Hiyo kanda maalumu wabishi sana hata kushaurika ni mpaka ukauke koromeo tena kwa wake zao ndiyo kabisa ubabe sana, ukiona mke asiye wahuko kajenga kwao kashauri mpaka kachoka na kuamua kujiongeza
 
mara watu wake ni wagumu sana kuongeza wanawake nisifa mke kuletewa mke kwao ni sawa mwanaume anakula siri na wazazi akipata hawara jioni asubuhi ni mke [emoji12]ukiona amepata pesa tegemea wake hata kumi siyo maisha
Ndicho wanachoweza
 
Popoma kama wewe huwezi kuelewa hii ni nini maana yake

Tatizo la mkoa wa Mara ni Nyerere fullstop. Hata wakati wa vita watu wanajiandikisha wakapigane vita ya Uganda aliwapunguza idadi ili kuwe na mgawanyo nchi nzima.

Mkumbuke hata Nimrod Mkono na utajili wake wote pale Busegwe alikuwa anakaa kwa baba yake mpaka alipokufa Nyerere ndio amehama kwao amejenga kasri lake na amejenga mashule na kuikabidhi serikali, Mkono angekuwa anatoka mkoa mwingine yale mashule angeyafanya mradi wake private au angejenga mahotel Musoma mjini.

No research no right to speak
Mkuu matola kumbe na wewe MMARA mwenzangu
 
Kwa hilo la kusingizia wanawake litawagharimu sana,mwanamke anasababisha vp ww usijenge kwenu?,hebu kuweni serious bhana...
Na hiyo husingizia kama mke sio wa huko kwao ni(mnyamahanga) watu wenyewe wabishi hawashauriki
 
Walinita kazini huko kwao mara nikafanya miezi miwili tu kwa raha siku nyingine majungu visa mateso na kejeli kibao.
Nilikuwa mdogo sana.
So niliot joto la jiwe .
Kuna siku walisema nipo na bosy ndio maana na cheo.
Mama huyo alinitesa mpaka kiakili.
Akawa na shida kweli
Kajua niuongo kwisha tukaanza tena maisha wakaja eti kila siku nideki ofiso wamegoma kusafisha kisa nipo.
Kingine nikivaa nguo zakimalaya eti huko nimekuja kujiuza ukivaa chochote wanalazimisha umekosea ukifanya chochote wewe unafanya kwa maana unajiona unajua sisi hatujui.
Hawabadiliki kuwa maendelelo wao ni visa tu.
So ikaja siku moja wakanisingizia kuwa mimi nafanya hoteli kama yangu naninaipeleka kama ninavyotaka mimi kisa mi ni bi mdogo ndio tatizo nimepewa cheo wao hata form four hawajafika so ilikuwa shida mara nawapelekesha hawana raha hawawezi kufanya kazi kisa mimi nipona ninawachanganya kzi ipo ikagonga mwamba.
Sasa wakaona sumu ni sababu nayo siku ila nilisanuliwa halafu kingine wakaniwekea wabakaji na wauaji bado haijatiki kuona hivyo nikaona niache kazi.
Duu pole sana shost
 
Usiombe ndugu yao aoe kabila jingine wee wanamajungu hao
Kazi kweli kweli si kwa majungu hao, mi nilikuwa na boyfriend wa huko mbeya balaa hana siri mkikutana naye lazima akatangaze tu, uzalendo ukanishinda yani ni wambeya hao
 
Mkoa wa Mara unabebwa na wilaya inaitwa Tarime. Tarime ni wilaya inayo kuwa kwa kasi sana kwa siku za hivi karibuni. Tofauti na Musoma kupewa makao makuu ya mkoa basi wilaya hii ya Tarime ilifaa kabisa kupewa makao makuu ya mkoa. Tarime ni wilaya iliyo jirani kabisa na mpaka baina ya Tanzania na Kenya. Pia Wilaya ya Tarime ina mgodi mkubwa wa dhahabu. Na wilaya ya Tarime asilimia kubwa imekaliwa na kabila la wakurya hawa watu wako vizuri sana katika utafutaji. Sababu hizi tatu kwa uchache umeifanya wilaya ya Tarime kukua kwa kasi. Anae waponda wakurya ni vile hawajui hawa watu vizuri. Wakurya ni watafutaji balaa hawa watu achana nao kabisa kwa sasa wanakuja kwa kasi sana. Tizama Jiji la Mwanza wafanyabiashara asilimia kubwa ni wakurya nenda pale Mwanza mtaa wa Libeti maduka mengi ni ya wakurya. Mule makoroboi wamejazana balaa, haya nenda tena kule mabatini kuna wafanyabiashara wakurya wanauza nafaka we acha tu, Mwanza asilimia kubwa inaongozwa na wafanyabiashara wakurya. Ndio maana katika mkoa wa Mara wilaya iliyo katika hali nzuri ni Tarime ukitoa Musoma na Musoma ni vile ni makao makuu ya mkoa bila hivyo aisee Tarime ingekuwa mbali. Ww unae wasema wakurya vibaya aisee nakuonea huruma ni vile huwajui tu. Mwanza, Mara, Shinyanga, Kahama, nakwingineko Wakurya wamekamata vilivyo katika biashara.
 
Back
Top Bottom