Historia ya mambo ya kuagizia nguzo aliyatoa Dkt Kalemani. Kipindi hicho Dkt Kalemani alipoleta hilo wazo Dkt Magufuli alikataa na waziri mkuu pia aligoma, yaani kwa ufupi serikali ilikataa. Na wasi wasi wao mkubwa ilikuwa ni kuhusu uwezo wetu wa ndani kuweza kutosheleza mahitaji ya nguzo. Ndipo Dkt Kalemani akakomaa, ila alichoambiwa na wakubwa zake kipindi hicho ni kuwa ole wake awadanganye hivyo akapewa ruhusa with conditions. Mungu mkubwa mahitaji yaliweza kukidhi kabisa na hapakuwa na upungufu. Zali lilikuwa kwa kundi la wafanya biashara wenyr dili la nguzo walikuwa wanamizigo iko njie hivyo lile katazo la waziri lilifanya walioagizia mizigo iwe njiani au wapi walikula hasara. Na ndiyo maana Mama kafika cha kwanza ongeza bei ya umeme, na agiza nguzo toka nje ili waliopoteza hela za nguzo waweze kufidishiq hizo gharama kwa kuongeza bei ya umeme na kuunganisha. Sasa hivi kitakachofuata ni kuongeza bei ya umeme. Hata bwawa la Strigler mwenye wazo la kufufua alikiwa na Dkt Kalemani. Dkt Magufuli akiwa ndiyo kaingia madarakani aliwataka nishati walete miradi ya kupunguza bei ya umeme, hivyo Dkt Kalemani akaenda kwenye makabrasha ya wizara na kukuta huo mradi, ndiyo akaenda kumpelekea Dkt Magufuli na ikawa ndiyo ajenda. Ukiangalia serikali ya Dkt Magufuli ililenga kupunguza gharama za maisha. Ila nashukuru sana Mama kupitia JK wanatufundisha adabu yaani Mama aendelee kukaza hivyo hivyo na aendelee hivyo hivyo kuwapa ulaji jamaa zake, maana uongozi ake ulihitajika sana kipindi hiki. Tena ajijenge na Familia ya Mzee Dkt JK ijijenge na itawale kabisa hata miaka 100 ili akili za watanzania zikae sawa