Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Maana yake hata mimi sijaelewa au ndio naambiwa noti zangu nilizochimbia uchagoni nozisalimushe?Je vipi hata zile zilizo uswiss natakiwa kuzisalimisha?Linaeleweka soma vizuri mkuu au usichoelewa ni aina zipi za noti?
Tangazo ni hili
--
TAARIFA KWA UMMA KUHUSU KUONDOA KWENYE MZUNGUKO NOTI ZA ZAMANI ZA SHILINGI YA TANZANΝΙΑ
Benki Kuu ya Tanzania inapenda kuufahamisha Umma kuhusu zoezi la kuondoa kwenye mzunguko noti za zamani za shilingi ishirini (20), mia mbili (200), mia tano (500), elfu moja (1000), elfu mbili (2000), elfu tano (5000) na elfu kumi (10000) kwa matoleo ya mwaka 1985 hadi mwaka 2003, na noti ya shilingi mia tano (500) iliyotolewa mwaka 2010 zenye sifa zilizoainishwa kwenye Tangazo la Serikali Na. 858 la tarehe 11 Oktoba 2024.
Zoezi la ubadilishwaji linatarajiwa kuanza tarehe 06 Januari 2025 hadi tarehe 05 Aprili 2025 kupitia Ofisi zote za Benki Kuu na benki zote za biashara kwa kupatiwa malipo yenye thamani sawasawa na kiasi kitakachowasilishwa. Aidha, matumizi ya noti hizo yatafikia ukomo wa kuwa fedha halali za Tanzania kuanzia tarehe 06 Aprili, 2025. Baada ya tarehe hiyo, mtu yeyote au taasisi yoyote inayomiliki fedha hizo haitaruhusiwa kuzitumia katika kufanya malipo popote duniani; na benki zote hazitaruhusiwa kulipa wala kupokea amana au maombi ya kubadilisha noti zilizoondolewa kwenye mzunguko.
Hivyo, Benki Kuu inatoa rai kwa wananchi wote wenye akiba ya noti hizo za zamani, kuzibadilisha au kuziweka amana kwenye benki yoyote ndani ya kipindi kilichotolewa.
Kwa taarifa/msaada zaidi tafadhali wasiliana na: Kurugenzi ya Usimamizi wa Sarafu, Benki Kuu ya Tanzania, 2 Mtaa wa Mirambo, S.L.P 2939 Dar es Salaam; au kwa Barua Pepe: info@bot.go.tz au botcommunications@bot.go.tz; au kwa simu +255745 802 007.
Emmanuel M. Tutuba.
GAVANA
View attachment 3135997