Nani amemfundisha Harmonize kujibu Maswali vizuri mbele ya camera? Amepiga hatua kubwa na amewazidi wasanii wengi

Nani amemfundisha Harmonize kujibu Maswali vizuri mbele ya camera? Amepiga hatua kubwa na amewazidi wasanii wengi

Leak

JF-Expert Member
Joined
Feb 22, 2012
Posts
52,916
Reaction score
43,505
Wasalaam wana jamvi!

Ni ukweli ulio wazi kabisa Msanii Harmonize amefanikiwa kuweka historia ambayo pengine wengi wetu hatukutarajia kabisa kama Harmonize angeweza kufanya uzinduzi mkubwa namna ile wa album yake!

Katika Jambo ambalo limenithibitishia kuwa Harmonize amekuwa kimziki na kwa kila nyanja ni pamoja na uwezo wake mzuri nilio ushuhudia wa kukabili maswali ya wana habari mbali mbali!

Kwakweli Harmonize ameonesha ukomavu wa hali ya juu na uwezo mkubwa sana wa kujibu maswali kwenye interview alizofanya jana na wengi pengine tulitegemea ange zua gumzo au mtafaruku kutokana na majibu yake lakini ukweli ni kwamba alijibu maswali vizuri akidhihirisha ukomavu wa hali ya juu!


Kwakweli kwenye hili la kujibu maswali na kuhimili maswali amewashinda wasanii wetu wengi sana na wana lakujifunza kutoka kwake!

Harmonize amepiga hatua sana ana stahili pongezi
 
Kiba anajua sana kujibu maswali ila hataki kujionyesha
 
kwakweli hata mie nilimkubali sana, ktk majibu yake mengi haoneshi kbs ujivuni...anajishusha down to earth kutambua umuhimu wa watu wote ktk safari & mafanikio aliyoyapata.
kwa hili namfananisha sana na Diamond.

kuna siku nimemsikiliza Omy Dimpoz akihojiwa Clouds pamoja naye Nandy...hana nidham kbs ya mahojiano, anaingilia ingilia maswali yasiomhusu (yameelekezwa kwa Nandy), pia ni mjivuni balaa kwa kifupi aliniboa kishenzi.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom