Nani amemwelewa Waziri wa Kilimo anatupeleka wapi?

Resilience

JF-Expert Member
Joined
Jan 4, 2023
Posts
1,096
Reaction score
4,948
Miaka miwili ya Waziri Bashe imekatika; Kwa tathimini ya kisekta Nani amemwelewa anatupeleka wapi? Je, unaona picha ya nchi kuwa na kilimo kama uti wa mgongo?

Tukimkumbusha kwamba UPO uwezekano akawa anamilikisha ardhi kwa wageni akiamini anainua kilimo tutakuwa tunakosea? Ana uhakika kwamba anaowaita wawekezaji ni wawekezaji au niwamiliki wa ardhi?
 
Bashe apewe muda amekutana na ufunguzi wa mipaka kama sera ya sasa ya rais Samia na ukame pia vita ya Ukraine iliyotatiza mzunguko wa chakula duniani huku wakulima wakitaka kuuza nje zaidi

USSR
 
Mimi nalia na sumu zinazopulizwa kwenye mazao, hasa matunda na mbogamboga, nilikuwa Iringa, eneo linaitwa Isagwa, dear God! sumu inayopulizwa kwenye nyanya halafu tunakula kachumbari ni mauaji, wale vijana wanapuliza hizo sumu wapo na vishati vyepesi wamelowa zile sumu mwili mzima, hata sijui mwisho wake utakuwaje?
Hili nalo tulitazame jamani.
 
Miaka miwili ya Waziri Bashe imekatika; Kwa tathimini ya kisekta Nani amemwelewa anatupeleka wapi? Je unaona picha ya nchi kuwa na kilimo kama uti wa mgongo?

Tukimkumbusha kwamba UPO uwezekano akawa anamilikisha ardhi Kwa wageni akiamini anainua kilimo tutakuwa tunakosea? Ana uhakika kwamba anaowaita wawekezaji ni wawekezaji au niwamiliki WA ardhi?
Anatupeleka huku
 
Ni sumu zinazokubalika kiafya with minimal effects.
 
Miaka miwili ya Waziri Bashe imekatika; Kwa tathimini ya kisekta Nani amemwelewa anatupeleka wapi? Je unaona picha ya nchi kuwa na kilimo kama uti wa mgongo?

Tukimkumbusha kwamba UPO uwezekano akawa anamilikisha ardhi Kwa wageni akiamini anainua kilimo tutakuwa tunakosea? Ana uhakika kwamba anaowaita wawekezaji ni wawekezaji au niwamiliki WA ardhi?
Subiri chawa wake waje kukushambulia.
 
Kwa sisi tunaolima Tumbaku huku naona ameamua kutufanya masikini.

Amechelewesha Mbolea na Dawa huku utaratibu wa Kuinunua Tumbaku zetu kupitia vyama vya Msingi akiwa ameubadirisha kwa kuipa tender Kampuni ambazo zimekuwa nyonyaji wa bei 🙌
 
Miaka miwili ya Waziri Bashe imekatika; Kwa tathimini ya kisekta Nani amemwelewa anatupeleka wapi? Je unaona picha ya nchi kuwa na kilimo kama uti wa mgongo?

Tukimkumbusha kwamba UPO uwezekano akawa anamilikisha ardhi Kwa wageni akiamini anainua kilimo tutakuwa tunakosea? Ana uhakika kwamba anaowaita wawekezaji ni wawekezaji au niwamiliki WA ardhi?
Waulizeni watu wa kusini, walionunua 70% ya mbolea ya Ruzuku aka Bashe mbolea. Wao wanajua zaidi kuliko hawa walaji wa mazao ya kilimo waliopo Dar na miji mingine.
 
Miaka miwili ya Waziri Bashe imekatika; Kwa tathimini ya kisekta Nani amemwelewa anatupeleka wapi? Je unaona picha ya nchi kuwa na kilimo kama uti wa mgongo?

Tukimkumbusha kwamba UPO uwezekano akawa anamilikisha ardhi Kwa wageni akiamini anainua kilimo tutakuwa tunakosea? Ana uhakika kwamba anaowaita wawekezaji ni wawekezaji au niwamiliki WA ardhi?
Madalali wa biashara ya nafaka watakutukana mpaka ujute kuketa huu uzi wako.

Hao ndiyo wanamuelewa sana kupitia biashara ya ulanguzi wa mazao ya chakula. Na kwa sasa ndiyo wamejivika joho na kujiita wakulima!
 
Bashe apewe muda amekutana na ufunguzi wa mipaka kama sera ya sasa ya rais Samia na ukame pia vita ya Ukraine iliyotatiza mzunguko wa chakula duniani huku wakulima wakitaka kuuza nje zaidi

USSR
Nchi inauza vyakula bora nje ya nchi na kuagiza vyakula vibovu kutoka Mashariki ya kati.

Sent from my TECNO BB2 using JamiiForums mobile app
 
Miaka miwili ya Waziri Bashe imekatika; Kwa tathimini ya kisekta Nani amemwelewa anatupeleka wapi? Je, unaona picha ya nchi kuwa na kilimo kama uti wa mgongo?

Tukimkumbusha kwamba UPO uwezekano akawa anamilikisha ardhi kwa wageni akiamini anainua kilimo tutakuwa tunakosea? Ana uhakika kwamba anaowaita wawekezaji ni wawekezaji au niwamiliki wa ardhi?
Bashe sio waziri wa ardhi
 
Mimi nalia na sumu zinazopulizwa kwenye mazao, hasa matunda na mbogamboga, nilikuwa Iringa, eneo linaitwa Isagwa, dear God! sumu inayopulizwa kwenye nyanya halafu tunakula kachumbari ni mauaji, wale vijana wanapuliza hizo sumu wapo na vishati vyepesi wamelowa zile sumu mwili mzima, hata sijui mwisho wake utakuwaje?
Hili nalo tulitazame jamani.
Washakufa watu wangapi na hizo sumu ?
 
Na pia haieleweki wapi kafaulu mpaka sasa??
Ni maneno mengi tu hana maajabu yoyote yale!!ndio maana kuna mbunge ameuliza inakuwaje bajeti iliyopita kuna pesa ilitengwq bilioni 200!!lakini hadi leo ni bilioni 40 tu ndio imepelekwa!!sawa tuna mdanganya nani?!!
 
Back
Top Bottom