Ni kweli pasi na shaka kuwa muandishi wa habari huibua mambo na kuwapasha watu habari
Hatahivyo,unapoandika habari unapaswa ujrdhshe kabla ya kuandika. Kwa mfano katika kuandika habari hiyo hakuna popote unapothbtsha uhusiano wa kujitoa kwa marehemu Dossa na kufilisika kwake.
Aidha kuwa jirani na mtu sio lazima kuijua historia yake. Pia sidhani kama ni kweli kuwa usingeandika wewe basi wengine tusingejua. Tunakushukuru kwa kusambaza habari ambayo naamini na wewe umepekua mabuku kuisoma.
Amani Msumari,
Sishangai kuwa leo unaulizwa ushahidi kuhusu
Dossa.
Kwani huko nyuma nilishangaa sana kwani hata jina lake ilipoandikwa
historia ya TANU na Chuo Cha Kivukoni, halikuwapo kitabu kizima.
Wala sikushangaa
Dossa aliposahauliwa wakati
Nyerere alipotoa medali
zaidi ya 3000 kwa watu waliotoa mchango mkubwa katika Tanzania.
Waarabu wana msemo wanasema, ''Sababu huondoa ajabu.''
Ama hilo la kuwa historia hii ingelijulikana hata mimi kama ninsingeandika
labda niseme kuwa kwa mara ya kwanza nilipoandika historia hii na kuchapwa
na gazeti la Africa Events (London), toleo zima lilikusanywa na kutolewa katika
mzuguko lisisomwe.
Jina la makala yangu ilikuwa, ''In Praise of Ancestors,'' March/April 1988.
Nafahamu mengi sana kuhusu historia hii.
Ukitaka kuthibitisha hebu soma historia ya babu yangu mmoja wa wazalendo
waliopigania uhuru wa Tanganyika kwa hali na mali:
Mohamed Said: KUTOKA JF: BABU YANGU SALUM ABDALLAH
Mimi sikupekua buku lolote kuijia historia hii.
Chanzo changu cha kwanza ni nyumbani kwetu na chanzo cha pili ni
Nyaraka
za Sykes.
Ingia hapo chini:
Mohamed Said: NYARAKA ZA SYKES KATIKA KAVAZI LA MWALIMU NYERERE