Ww n mzushi na mdini japo sio baya niseme mbaguzi wa dini
unaandika historia kutoka katika masimulizi siku zote historia inayo andikwa kutokana na masimulizi upoteza ualisia mtu anaweza kupindisha jinsi anavyotaka sema unatafuta nafasi ya ndungu zako sijui babu yako katika historia ya Tanganyika
Watu watakao kutilia maanani ni wale ambao wanataka mambo yawe kama ww unavyotaka na jamii yako
Na mm nikitaka nitaandika historia ya babu yangu OSCAR KAMBONA jambo ambalo sio kweli
Ss waafrica hatuna tamaduni za kuto kuandika autobiography zetu ndo maana tukifa zinapotea uwezi kumlaumu mtu katika wao kupotea katika Historia ya Tanganyika
Sema kma unatafuta skapegoat labda lakini si fingine
Visidady,
''Mzushi,'' na ''Mdini.''
Naandika kutokana na simulizi.
Uzushi maana yake ni uongo.
Mimi nimeandika upya historia ya TANU na hakuna aliyeweze kuipinga
toka kitabu kilipochapwa 1998.
Mimi ndiye niliyesahihisha yale yaliyokosewa.
Kitabu changu kimefanyiwa mapitio kadhaa na mabingwa wa historia ya
Afrika kama
John Iliffe,
Jonathon Glassman,
James Brennan na
wengineo na kuchapwa katika jarida maarufu, ''Cambridge Journal of African
History.''
Hakuna popote waliposema mimi, ''Mzushi,'' au ''Mdini.''
Brennan yuko katika hatua za mwisho katika kukamilisha kitabu cha babu
yako
Oscar Kambona.
Ukitaka kujua umuhimu wa simulizi katika kutafiti historia soma kitabu hiki
''The Rise and Fall of the Third Reich,'' cha
William L. Shirer.
Waafrika wanaandika, ''autobiography,'' zao na nitakupa mifano kutoka hapa
hapa nyumbani.
Kleist Sykes ameandika maisha yake kabla hajafariki 1949,
Andrew Tindegebage
na yeye kaandika pia, halikadhalika
Shaban Robert.
Lakini kama unataka kujua tatizo la udini wasome waandishi hawa,
P van Bergen
(1981),
John Sivalon (1992) na
Njozi (2002).
James Brennan na Mohamed Said, Dar es Salaam