Nani amesema Mzee Dosa Aziz Ali alifirisika kwa kupigania uhuru?

Xio kwamba cjui matusi na maneno ya kashfa,basi tuu yaishe
 
Visidady,
''Mzushi,'' na ''Mdini.''
Naandika kutokana na simulizi.

Uzushi maana yake ni uongo.

Mimi nimeandika upya historia ya TANU na hakuna aliyeweze kuipinga
toka kitabu kilipochapwa 1998.

Mimi ndiye niliyesahihisha yale yaliyokosewa.

Kitabu changu kimefanyiwa mapitio kadhaa na mabingwa wa historia ya
Afrika kama John Iliffe, Jonathon Glassman, James Brennan na
wengineo na kuchapwa katika jarida maarufu, ''Cambridge Journal of African
History.''

Hakuna popote waliposema mimi, ''Mzushi,'' au ''Mdini.''

Brennan yuko katika hatua za mwisho katika kukamilisha kitabu cha babu
yako Oscar Kambona.

Ukitaka kujua umuhimu wa simulizi katika kutafiti historia soma kitabu hiki
''The Rise and Fall of the Third Reich,'' cha William L. Shirer.

Waafrika wanaandika, ''autobiography,'' zao na nitakupa mifano kutoka hapa
hapa nyumbani.

Kleist Sykes ameandika maisha yake kabla hajafariki 1949, Andrew Tindegebage
na yeye kaandika pia, halikadhalika Shaban Robert.

Lakini kama unataka kujua tatizo la udini wasome waandishi hawa, P van Bergen
(1981), John Sivalon (1992) na Njozi (2002).


James Brennan na Mohamed Said, Dar es Salaam
 
Kila mtu anaongea lake, ilimradi tu...
CGO...
Halijapata kuwa kitu cha mpata mpatae yaani kila mtu analijua.

Historia ya TANU iko ile iliyoandikwa na Chuo Cha Kivukoni wengi
wa hao hawakuwa na taarifa za kutosha na hii niliyoandika mimi
kwa kutumia Nyaraka za Sykes waasisi wa African Association
mwaka wa 1929 chama kilichokuja kugeuzwa na kuwa TANU.

Hivyo hili si la ''kila mtu anaongea lake...''
Kitabu ndiyo hiki:



Unaweza pia kupata mengi hapo chini:
file:///C:/Users/yemen/Downloads/Tanzania_-_A_Nation_Without_Heroes_abridged%20(3).pdf
 
Shukran..
 
Sasa nimeelewa ndugu Mohamed Said. Unaona kuwa Dossa hakupewa kipaumbele kwenye historia ya ukombozi wa Tanganyika kwasababu ya dini yake. Nasema hivyo kwa kuzingatia maelezo yako kwenye kitabu hicho kumhsu Abdulwahid Sykes. Naomba maoni yako kuhusu A.M.N.U.T (Chama cha siasa) na harakati zake za kupigania uhuru wa Tanganyika.
 
Amani Msumari,
Haya mambo tumejadili hapa sasa yafika zaidi ya miaka mitatu.
Inaelekea ndugu yangu wewe ni mgeni hapa Majlis.

Hebu ingia www.mohammedsaid.com search, ''Africa Events.''
Hilo lilikuwa gazeti likichapwa London nikiandikia katika 1980s.

Utaona makala nilizoandika hapa Majlis kuhusu tatizo la historia
ya TANU.

Kuhusu AMNUT unngependa kujua kitu gani?
Mohamed Said: UTATANISHI KATIKA HISTORIA YA TANU
 
Nimekuelewa mkuu. Ngoja nikasome huko uliponielekeza.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…