SoC04 Nani amtetee Raia kutokana na unyanyasaji wanaofanyiwa na vyombo vya ulinzi na usalama?

SoC04 Nani amtetee Raia kutokana na unyanyasaji wanaofanyiwa na vyombo vya ulinzi na usalama?

Tanzania Tuitakayo competition threads
Joined
Jan 31, 2021
Posts
15
Reaction score
10
Tanzania ni nchi salama yenye hali nzuri ki siasa, kijamii na kiusalama, lakini kama watanzania ama mtanzania napenda kusimama kuzungumza na kushauri mambo kadhaa hasa yanayohusu vyombo vyetu vya ulinzi na usalama polisi na jeshi.

Polisi na Jeshi katika utaratibu wao wa kufanya kazi ni nani anawasimamia, ama wanafanya kazi bila taasisi inayowasimamia? Mfano wenzetu Kenya wana tume ya usimamizi wa maadili ambao hufuatilia utendaji wa polisi na wanajeshi. Ikitokea Polisi wala rushwa, hukamatwa na tume na kufikishwa mbele ya sheria.

Kwetu hapa nchini kumekuwa na matukio ya polisi, wanajeshi kuvunja sheria katika ukamataji ama ndani ya jamii, kutisha, ubabe na fujo, kudhurumu, kuendesha vyombo vya usafiri vibovu, kula rushwa, kupiga raia na kadharika, lakini wanapokamatwa husimamiwa na walewale polisi wenzao na haki haitendeki. Mfano kuna tukio lilitokea Dar es Salaam ambapo polisi aliyekuwa doria kwenda kwenye baa akanywa pombe kisha akaanza kitishia raia kwa bunduki.

Kuna mifano ya matukio ya wanajeshi kupiga raia mtaani. Je, hapa raia anapata vipi haki yake tena kesi inasimamiwa na polisi ama wanajeshi walewale?

Nashauri kiwepo chombo kinachojitegemea kitakachowasimamia polisi na wanajeshi lengo kuchangiza utendaji na weledi wao hii itapunguza malalamiko ya wananchi kwa polisi ama wanajeshi

Pili nashauri liwepo dawati katika kila kata ambalo litadumisha mahusiano mema baina ya raia na wahusika wa vyombo hivi vya usalama.
 
Upvote 1
Nashauri kiwepo chombo kinachojitegemea kitakachowasimamia polisi na wanajeshi lengo kuchangiza utendaji na weledi wao hii itapunguza malalamiko ya wananchi kwa polisi ama wanajeshi
Hii ni nzuri, kila anayepaswa kuwajibika anatakiwa awe na chombo kinachomuwajibisha. Katika mfumo unaofanya kazi vizuri "check and balance"
 
Askari wengi Sana wa Tanzania ni watu wa hovyo kupita kiasi, kama hujawahi kukutwa na matukio yao ya hovyo unaweza kudhani ni watu wa maana lakini wana ushetani ndani yao
 
Back
Top Bottom