Nani ana uwezo wa kushtaki na kushtakiwa kisheria?

Nani ana uwezo wa kushtaki na kushtakiwa kisheria?

Joined
Apr 26, 2022
Posts
83
Reaction score
128
Jambo la kwanza kabla ya kuamua kushtaki au kufungua kesi Mahakamani hakikisha una miguu ya kusimamia Mahakamani, kisheria tunaita LOCUS STANDI.

Locus standi ni neno la kisheria lenye asili ya kilatini ikimaanisha maslahi au haki uliyo nayo au iliyovunjwa na mtu au taasisi na hivyo kukupa haki ya kusimama Mahakamani kulalamika.

Mahakama ya Rufaa nchini Tanzania imefafanua maana ya locus standi kwenye kesi mbali mbali, ikiwemo hii kesi ya SWEETBERT MATHIAS KUTAGA Vs EUGENIA RUTATORA, CIVIL APPEAL NO. 565 OF 2023, kwenye hiyo kesi Majaji watatu wa Mahakama ya Rufaa wanasema kwamba ili locus standi iwepo ni lazima;

"Mtu yeyote anayeleta kesi Mahakamani aweze kuthibitisha kuwa maslahi au haki yake imevunjwa au kuingiliwa"

Na hii si kwa anayeshtaki tu, bali hata anayeshtakiwa lazima uhakikishe unamshtaki mtu sahihi au mwenye miguu na uwezo wa kushtakiwa au kusimama Mahakamani. Sio kila mtu au taasisi inaweza kushtaki na kushtakiwa kisheria hata kama mtu amevunja haki yako bado unaweza usiwe na haki ya kumdai au kumshtaki yeye kama yeye.

Lengo ni kuzuia (stranger) mtu yeyote tu ambae hana connection au maslahi yoyote kuingia kwenye kesi kudai au kulalamika Mahakamani. Inapunguza utitiri wa kesi. Wasiliana na Wakili wako kabla ya kuamua kufungua kesi. Kwa sababu ukishtaki mtu asiye sahihi basi utawekewa pingamizi la kisheria na kesi yako haitafika kusikilizwa kwenye kiini bali itatupiliwa mbali asubuhi mapema sana.
 

Attachments

  • FB_IMG_1715491829933.jpg
    FB_IMG_1715491829933.jpg
    123.6 KB · Views: 17
Back
Top Bottom