Dr Matola PhD
JF-Expert Member
- Oct 18, 2010
- 60,050
- 104,466
Usimfananishe Yesu na mambo ya kijinga Tafadhali.Yesu alizaliwa kwenye banda la mifugo. Utu uzima wake wote hakuwa na makazi wala kibarua cha kudumu. Aliishi kwa fadhila za watu.
Nyerere alipojiunga na TAA alikuwa mwalimu wa kawaida tu ambae alikuwa anapakizwa kwenye baiskeli kurudi shuleni.
Bibi Titi Mohammed hakusoma na aliolewa akiwa na umri wa miaka 14. Alikuwa muimbaji kwenye kikundi cha ngoma.
Kutokana na mawazo yako, wote hawa hawakustahili uongozi kutokana na hali duni waliyokuwa nayo.
Mpimeni huyu binti kwa uwezo wake na sio vitu alivyokuwa navyo.
Amandla...