Nani anafaa kuwa Mwenyekiti wa BAWACHA baada ya Viongozi kutimuliwa?

Nani anafaa kuwa Mwenyekiti wa BAWACHA baada ya Viongozi kutimuliwa?

Wakuu muda ni mchache sana na mambo ni lukuki, bila kupoteza muda Kamati kuu ya CHADEMA baada ya kutimua wasaliti, imeagiza mchakato wa kujaza nafasi zao uanze mara moja, jambo ambalo naliunga mkono .

Sasa kwa haraka haraka unadhani ni nani kati ya akina mama waliopo chadema kwa sasa anayefaa kutwaa nafasi iliyoachwa wazi na Msaliti Mdee baada ya kufurushwa? kumbuka kwamba Chadema haijawahi kupuuza maoni ya wengi.

Natanguliza Shukrani.
Kama yanayosemwa kuhusu Lissu ni kweli basi Lissu anafaa kuwa mwenyekiti wa BAWACHA taifa.
 
Ipo siku ccm itakosa hela ya kuhonga,
Suala sio kuhonga mkuu, ila lazima ukweli usemwe kuwa wanasiasa wataendelea kufanya siasa kwa maslahi yao na familia zao sio kuburudisha watu kama wengi tunavyoamini.
 
Sisi ya kwetu tumemaliza, hayo mengine hayatuhusu, yeye ajipigie tu hizo mil 600
We unaona mill 600 hela..? Kama mbunge anakula 40mill kwa mwezi ya mfuko wa jimbo na haitumii jimboni, unadhani kwa miaka 5 ana kiasi gani?
 
Yeyote mtakayemchagua kuwa M/kiti tutamnunua. Sasa Kama Hilda na umasikini wake, tukiweka hata mil 50 atachomoa kweli? Kwa hali ya Sasa ya kiuchumi ya watu wenu, mko compromised, ni rahisi kuhujumiwa kwavisenti kidogo
 
Catherine Ruge .. Chairperson
Yosefa komba.. Secretary
Hilda Newton...vice chairperson
.......
....
 
Wakuu muda ni mchache sana na mambo ni lukuki, bila kupoteza muda Kamati kuu ya CHADEMA baada ya kutimua wasaliti, imeagiza mchakato wa kujaza nafasi zao uanze mara moja, jambo ambalo naliunga mkono .

Sasa kwa haraka haraka unadhani ni nani kati ya akina mama waliopo chadema kwa sasa anayefaa kutwaa nafasi iliyoachwa wazi na Msaliti Mdee baada ya kufurushwa? kumbuka kwamba Chadema haijawahi kupuuza maoni ya wengi.

Natanguliza Shukrani.
Tumpe vyeo vyote Mbowe. Kwani yeye ndiyo kila kitu kwenye Chadema
 
Catherine Ruge .. Chairperson
Yosefa komba.. Secretary
Hilda Newton...vice chairperson
.......
....
Wote hawafahi bora tumpe vyeo vyote Mbowe mwenye uchungu na Chadema yake ambako tukikumbuka nae aliuza nafasi ya ugombea Urais kwa Lowassa kumbukeni maneno ya Dr Slaa
 
Mkuu kama Mdee yadaiwa kugeuka msaliti labda atafutwe malaika ambae hatuna uwezo wa kumteua.Labda tatizo lipo ndani ya uongozi wa juu kabisa.
Usaliti wa Mdee Ni Maslahi tu.Hata wale mitume 12 wa Yesu,Pesa ilimnyakua mmoja
 
Anaweza akawa anafaa sana ila yule sio wa mitandaoni, na ndio maana huoni mtu akimtaja na hata wewe jina tu umemsahau.
Chadema inaendeshwa kwa matukio na mihemko.
Anaitwa Dr.Maryrose
Yule dada aliyepambana na Lissu kutaka nafasi ya kugombea urais wa JMT yuko wapi?

Amandla...
 
Back
Top Bottom