Nani anafuatilia maudhui yanayorushwa kwenye tv za mabasi yanayosafirisha abiria?

Nani anafuatilia maudhui yanayorushwa kwenye tv za mabasi yanayosafirisha abiria?

gcmmedia

Member
Joined
Jul 19, 2024
Posts
34
Reaction score
75
Nimekuwa nikisafiri kwa mabasi kwenda mikoa mbalimbali na kuna maudhui mbalimbali (muziki na filamu) yanarushwa kwenye tv za basi.

Vyombo hivi vya usafiri husafirisha watu wa umri tofauti, undugu wa karibu na dini tofauti. Maudhui yanayorushwa wakati Fulani hayazingatii mazingira ya wasafiri hawa.

Je, Nani anayedhibiti maudhui yanayorushwa ili yasiwe kero kwa wengine?
 
Latra hawafanyi kazi wapo wapo tu na huu ni ushahidi mojawapo
 
Kinacho udhi ni zile za kutafsiri ...zinakuwaga na matusi sana
 
Mnaweza ongea na makondakta mbadilishiwe,kulalamika jukwaani hakutasaidia
 
LATRA wapo bize na Katarama vs Ally's hawana muda wa kufatilia maudhui hayo
 
Back
Top Bottom