Nani anaiongoza CCM?

Nani anaiongoza CCM?

JK alidhania kuongoa nchi ni kukaa kimya na kucheka cheka na kuwabeba washikaji....kizazi hiki balaaa atakoma kama alidhania fasion analo...hakuna kukimbia na kila kitu lazima afanye na katiba mpya lazima chama kitamdodea akifanya mchezo uchaguzi zbar ndio balaa zaidi...huku bara wapinzani wajipange wapate wabunge wengi...kwisha habari yao..wataacha kubebana...
 
I always admire boldness yako on things you belive, ila pia kuelekea 2010, jihadhari sana na malumbano na ma opportunists watakaoimba nyimbo za shangwe na mapambio kuhusu CCM kwa sababu maalum, ila naamini ukweli wanaujua.

- Somebody has to be a pert of a solution, badala ya sisi wote kulazimishwa kua part of the problem, mimi sikuwekeza kwenye kampuni ya Mwakyembe kwamba sasa asipopata ubunge tena au urais nitalala na njaa, ndio maana ninamheshimu sana Mwandosya kwa sababu huwa hana time na wawekezaji uchwara kama mimi Bwa! ha! ha! ha!

- Nowa on a serious note, ni kwamba wakati umefika tuanze kutoa alternative kwa taifa na wananchi wa Tanzania, sikubaliani na hoja za generalizations, sio kwa sababu Zitto anataka Dowans, basi Chadema nzima inataka Dowans, ni kweli CCM tuna matatizo ya uongozi yanayosababishwa na baadhi ya viongozi wetu wachache, lakini haitufanyi CCM nzima tukawa majuha au hatuna viongozi, hapana sio kweli.

- Then inakuja hoja ya kumuingizia Mwalimu, kwamba Mwalimu was best lakini CCM ya sasa ina problem, ninasema hizi ndio njia rahisi rahisi tulizoziwea wabongo za kutafuta majibu ya mawswali mazito, kwa sababu ukweli ni kwamba 95% ya viongozi wa ngazi mbali mbali tulionao leo Tanzania kuanzia CCM mpaka Upinzani ni creation ya Mwalimu, sasa mnatuambia nini kuhusu Mwalimu? Kwamba alikuwa na sura mbili za uongozi moja safi ya kuigwa na nyingine ndio hii tunayoiona kwa viongozi wetu wa sasa? Kama jawabu ni hapana then keep Mwalimu out of this mess of ours, CCM na Upinzani included wote tumechanganyikiwa kwa sababu kila chama cha siasa kina viongozi wabovu na kuwatoa ni tatizo, na mara kwa mara tulio clean tunalazimika kuwabeba. Rais wangu Dr. Slaaa anasema Dowans haifai, halafu anaulizwa what that means kuhusu kauli za Zitto kwamba Dowans inafaa, anasema no comments, lakini akifanya haya kiongozi wa CCM anakuwa mnafiki, na hafai, ameishiwa akili, amepitwa na wakati, na yeye ni fisadi, na sisi wananchi wote hapa tunatakiwa kukubali hizi great ideas as a solution kwa taifa letu, tukihoji basi tumetumwa na mafisadi, tunatetea something na blah! blah! sisi sio wazalendo!

- Tutoe solution zinazolingana na mazingara yetu tuliyonayo sasa Tanzania, ama sivyo tunakua out of touch na reality ya kinachoendelea politically katika taifa letu, transformation ya kutoka kwenye one stage ya giza ambamo wote tulikuwemo kwenda kwenye mwanga haiwezi kufanyika kama unavyopigwa mpira wa golf, hao US na Europe, ambao mara kwa mara ndio standard zetu hapa JF wamepitia miaka 300 sisi ndio kwanza tupo miaka 47, sasa 300-47= 253, eti unaweza kui-cover miaka 253 kwa miaka 14 tu toka tuamke na kuanza ku-practice Demokrasia, haiwezekani, lakini have we made some progress yes! tena a big one ingawa sio kwa speed ambayo wengi tunaitaka hapa JF.

- Tuongee matatizo na tuyatolee solutions, lakini ku-generalize wengine wote kwa sababu ya matatizo ya viongozi wachache ambao hata hawafikii .5% ya wanachama karibu Millioni 5 wa CCM, it is unfair, taifa ni letu sote hili sio kwa sababu ya kuwa na mtizamo flani ambao ni unrealistic na kuna wengi wanaoukubali, basi tusiokubali tunakuwa sio wazalendo na tumetumwa na mafisadi, hapana ni demokrasia makini wananchi kuwa na mitizamo tofauti katika kujaribu kutafuta solutions za taifa letu sote, na ni lazima tuheshimiane in the process, mimi siamini kwamba Chadema nzima wanataka Dowans.

- Mimi ni mwanchama hai wa CCM sijawahi kuficha, ninaamini kwamba ndani ya chama changu tuna matatizo ya uongozi yanayohitaji a serious marekebisho, kama wananchi wengine wanavyoamini kwamba dawa ni kuwa mpinzani kuweza kurekebisha mimi ninaamini ninaweza kwa kuanzia ndani ya CCM, kwa hiyo ni mtizamo tofauti lakini lengo ni lile lile.

Lakini viongozi wachache wabovu ndani ya taifa letu hawatufanyi wananchi wote wa Tanzania kuwa ni wabovu.

Ahsante Wakuu na Tuendelee kuelimishana, taifa liko njia panda, ninawashukuru wachangiaji karibu wote kwa ustaarabu mliouonyesha katika huu mjadala, ingawa yupo jamaa yangu mmoja mwenye kujaribu kuleta matatizo yake ya personal, Ahhh! huyu tulishamsamehe, otherwise hii ni great debate na heshima tele kwa mleta mada, tukutane tena soon maana taifa linaelimika wka topic kama hizi.

Respect!

Wazee wa sauti ya umeme FMES!
 
Mkuu FMES sauti ya radi na umeme...heshima.
Kumbuka samaki mmoja akioza basi wote wameoza tambua hilo kwanza.
Lakini hivi leo ni nani anayeweza akakemea?
 
FMES,
Mkuu wangu maelezo yako mazuri sana kama utabakia ndani ya kabati... lakini ukweli ni kwamba Mwanakijiji kasema kitu kimoja kizito sana!..Yaani sina hata la kusema zaidi ya kujiuliza hivi kweli CCM hawayaoni haya?..

Mkuu wangu CCM ya mwalimu sio hii tena, imepoteza mwelekeo na wala sii kosa la Kikwete kwani naye kaendeleza ya baba yake Mkapa..Maneno haya siyatungi alisema mwenyewe Kikwete na kwa bahati mbaya sidhani kama anaona kuna matatizo ya uongozi ndani isipokuwa matatizo yanatoka nje.

Ni imani ambayo nina hakika CCM wote wanafikiri kuwa matatizo yao yanatoka nje, kuna watu wanafiki washenzi wenye wivu ambao wanataka kuwavuruga kumbe chama chao chenyewe kimekosa mwelekeo..
Mkuu wangu hakuna mtu hata mmoja anayetaka kujiunga na vyama nje ya CCM wala Chadema isingekuwepo for the same of making multi party isipokuwa CCM imepoteza mwelekeo na mambo mengi sana ukiyasoma ndani ya Chadema ni yale yaliyokuwa yakiaminiwa na wananchi toka tupate Uhuru...

Haiwezekani hata kidogo lawama hizi ukazipeleka kwa Nyerere kwa sababu ya viongozi waliokuwepo kuwa kizazi chake, mkuu wangu hata wewe na mimi sote ni kizazi cha mwalimu na ndio maana tumeweza kuona tofauti hizo.. Sii lazima wewe uwe na tabia sawa na baba yako wala character zako haziwezi kutokana na malezi ya baba yako..watoto wawili mnaweza kuwa tofauti kabisa baina yenu na tofauti na baba yenu..ila unaweza fuata profession ya baba yako na sii lazima ukawa mzuri/mbaya kama baba yako..

Kinachotokea leo CCM naogopa kusema ni CANCER ndani ya chama na kinajimaliza chenyewe.. hizo nguvu anazotangaza malecela na wengine ni aibu ya mgonjwa ambaye ananyonyoka nywele kwa sababu ndani ya akili yake anafikiria ana HIV hivyo ni aibu kwa jamii..
Maradhi ya CCM sio aibu wala sio HIV ni cancer na mkiwahi mnaweza kupata tiba!..
Heko mwanakijiji kwani sio kila siku tunawaponda CCM bila kuwapa mwanga wakayajua mapungufu yao...
 
Mkuu FMES sauti ya radi na umeme...heshima.
Kumbuka samaki mmoja akioza basi wote wameoza tambua hilo kwanza.
Lakini hivi leo ni nani anayeweza akakemea?

- Hapana mkuu nina tatizo sana na mifano kama huu wako, kwa sababu siamini kwamba wananchi wote wa Tanzania, kwa kuichagua CCM kutuongoza for the last 47 years, basi wote tumeoza! Hapana mimi sikuoza niko clean na ndio maana ninakuja hapa kukata ishus bila uoga, unajua ukishakuwa mchafu ndio unaanza kujificha ficha na kubadilika badilika rangi, na kuimba imba taarabu kila kona humu JF, lakini ukiwa clean unasimama na kusema bila kuogopa wala kujali umaarufu, au matusi, maana hoja nzito ni nzito tu

- Tuache tu kuchanganya ishu zetu binafsi za udini, ukabila, na uwekezaji, na taifa, au vyama vyetu vya siasa, au viongozi, kwa sbabu havina uhusiano wowote tujali wananchi sio mpaka interest zetu zikiguswa tu basi maneno meengi, sio vizuri.

- Haya mkuu tuendelee kuelimishana na kukata ishus kiroho mbaya, maana taifa ni letu wote!

FMES!
 
FMES,
Mkuu wangu maelezo yako mazuri sana kama utabakia ndani ya kabati... lakini ukweli ni kwamba Mwanakijiji kasema kitu kimoja kizito sana!..Yaani sina hata la kusema zaidi ya kujiuliza hivi kweli CCM hawayaoni haya?..

Mkuu wangu CCM ya mwalimu sio hii tena, imepoteza mwelekeo na wala sii kosa la Kikwete kwani naye kaendeleza ya baba yake Mkapa..Maneno haya siyatungi alisema mwenyewe Kikwete na kwa bahati mbaya sidhani kama anaona kuna matatizo ya uongozi ndani isipokuwa matatizo yanatoka nje.

Ni imani ambayo nina hakika CCM wote wanafikiri kuwa matatizo yao yanatoka nje, kuna watu wanafiki washenzi wenye wivu ambao wanataka kuwavuruga kumbe chama chao chenyewe kimekosa mwelekeo..
Mkuu wangu hakuna mtu hata mmoja anayetaka kujiunga na vyama nje ya CCM wala Chadema isingekuwepo for the same of making multi party isipokuwa CCM imepoteza mwelekeo na mambo mengi sana ukiyasoma ndani ya Chadema ni yale yaliyokuwa yakiaminiwa na wananchi toka tupate Uhuru...

Haiwezekani hata kidogo lawama hizi ukazipeleka kwa Nyerere kwa sababu ya viongozi waliokuwepo kuwa kizazi chake, mkuu wangu hata wewe na mimi sote ni kizazi cha mwalimu na ndio maana tumeweza kuona tofauti hizo.. Sii lazima wewe uwe na tabia sawa na baba yako wala character zako haziwezi kutokana na malezi ya baba yako..watoto wawili mnaweza kuwa tofauti kabisa baina yenu na tofauti na baba yenu..ila unaweza fuata profession ya baba yako na sii lazima ukawa mzuri/mbaya kama baba yako..

Kinachotokea leo CCM naogopa kusema ni CANCER ndani ya chama na kinajimaliza chenyewe.. hizo nguvu anazotangaza malecela na wengine ni aibu ya mgonjwa ambaye ananyonyoka nywele kwa sababu ndani ya akili yake anafikiria ana HIV hivyo ni aibu kwa jamii..
Maradhi ya CCM sio aibu wala sio HIV ni cancer na mkiwahi mnaweza kupata tiba!..
Heko mwanakijiji kwani sio kila siku tunawaponda CCM bila kuwapa mwanga wakayajua mapungufu yao...

Mkuu Bob,

- Heshima mbele bro, sina tatizo na baadhi ya hoja nzito sana za mleta mada yaani Mkulu Mwanakijiji, tatizo langu ni generalization na kwamba CCM haina uongozi, hapana CCM tunao viongozi ila tunao wachache wabovu na sio rahisi kuwang'oa kwa sababu kama ile aliyoisema Rais wangu Dr. Slaaa, kwamba hana comments on Zitto na Dowans, principle ni ile ile, sasa nashangaa kwamba kwa CCM inakuwa tatizo lakini sio kwa Upinzani.

- CCM hawana uongozi, good kulinganisha na nani ambao wanao uongozi? Kwamba eti CCM hatuna muelekeo, basi kina Lowassa na Msabaha, Karamagi wangekua bado viongozi wa juu mpaka leo, kina yona na Mramba wasingekuwa nje kwa dhamana, baadhi ya viongozi wa CCM ni wabovu? Yes tena sana na hawa wapo hata upinzani,

- Eti CCM haina nguvu? Ninaamini kwamba you know better than this, kwamba eti ina cancer kweli lakini ni cancer yetu wote taifa zima ndio maana hakuna wa kumfunga kengele mwingine, Eti tunapewa mwanga kwa kutukanwa kwamba CCM hatuna uongozi na huku tunao viongozi wetu tuliochagulia kwa mujibu wa katiba yetu? Hapana tunao viongozi wazuri na wabovu.

Ahsante Mkuu.

FMES!
 
OK nimekupata FMES lakini CCM ya sasa si CCM ya enzi ya akina mzee Julius siku hizi watu wamejaa unafiki mwingi na woga na kuwatukuza watu wasio stahili kila siku.
 
OK nimekupata FMES lakini CCM ya sasa si CCM ya enzi ya akina mzee Julius siku hizi watu wamejaa unafiki mwingi na woga na kuwatukuza watu wasio stahili kila siku.

- Wa-Tanzania wote tuko hivyo tunaktaa upande mmoja lakini tunakubali wa pili, according to our interest, ndio cancer yenyewe ya taifa. Otherwise nimekusikia sana mkuu.

Respect

FMES!
 
- Wa-Tanzania wote tuko hivyo tunaktaa upande mmoja lakini tunakubali wa pili, according to our interest, ndio cancer yenyewe ya taifa. Otherwise nimekusikia sana mkuu.

Respect

FMES!

Ndo hapo sasa nini kifanyike?Wakati nyie wazalendo mpo mbali huko nani ataiokoa nchi hii inayo elemewa???
 
Ndo hapo sasa nini kifanyike?

- Roma haikujengwa kwa siku moja mkuu, hivi unajua kuwa kuna wakati according to the history kule Europe, ilikuwa kuwa na choo ndani ya nyumba ni crime against the law of the land!

- Pole pole na mwendo wetu huu wa kibongo bongo tutafika tuu!

Saafi saana, kata issue, tuko pamoja. Mimi ninamwaga chaki kwanza!

Kuna wachangiaji hapa walionekana kuwa ni mahiri lakini sasa wanaonekana with true colors kuwa si lolote si chochote ni reflection ya viongozi wabovu.

Walikuwa ni wajenga hoja wakubwa, lakini sasa wanakula matapishi yao na kusahau wajibu wao ni upi. Wamevaa miwani ya mbao kwa makusudi mazima ili wasione ukweli wa mambo na badala yake wanakwenda kama bendera wakielekea kule kwenye upepo unapokwenda. Uongozi wa kweli na thabiti unahitaji mtu mvumilivu, makini na juu ya yote hekima na busara, hebu niambie ni Chama gani chenye hazina kubwa katika haya niliyoyataja.

Ukweli utaendelea kuwa ukweli, pamoja na mapungufu ya hapa na pale (ambayo yapo kila mahali kwenye ulimwengu huu) Tanzania ni nchi inayoongozwa vizuri sana na hii yote ni kwa sababu CCM ni makini na imara
 
FMES: umeandika na kuainisha vyema hoja zako.
Then inakuja hoja ya kumuingizia Mwalimu, kwamba Mwalimu was best lakini CCM ya sasa ina problem, ninasema hizi ndio njia rahisi rahisi tulizoziwea wabongo za kutafuta majibu ya mawswali mazito, kwa sababu ukweli ni kwamba 95% ya viongozi wa ngazi mbali mbali tulionao leo Tanzania kuanzia CCM mpaka Upinzani ni creation ya Mwalimu, sasa mnatuambia nini kuhusu Mwalimu?
Nadhani umegusia ishu nzuri kuhusu Mwl Nyerere, mimi nasema you have answered the question, kama nchi imeoza na Mwalimu Nyerere ndo chanzo cha uongozi mzima wa leo, basi Nyerere was a lousy leader, I have no problem saying that.

hao US na Europe, ambao mara kwa mara ndio standard zetu hapa JF wamepitia miaka 300 sisi ndio kwanza tupo miaka 47, sasa 300-47= 253, eti unaweza kui-cover miaka 253 kwa miaka 14 tu toka tuamke na kuanza ku-practice Demokrasia, haiwezekani, lakini have we made some progress yes! tena a big one ingawa sio kwa speed ambayo wengi tunaitaka hapa JF.
As a student of history nakataa kwani ukiangalia historia ya USA, walizaliwa katika mfumo wa multiparty demokrasia unaoheshimu property rights. Ni kweli walikuwa na utumwa na kadhalika lakini the environment that was created, the constitution that was written including its flexibility of the the Bills of Rights foresaw possbile changes in the future and came up with a way to address it, including an independent judiciary.
Sasa what I say is that we do not need to reinvent the wheel and to go through the same mistakes eti kwa sababu sisi ni taifa changa. We have many relevant examples that we can emulate.

kama wananchi wengine wanavyoamini kwamba dawa ni kuwa mpinzani kuweza kurekebisha mimi ninaamini ninaweza kwa kuanzia ndani ya CCM, kwa hiyo ni mtizamo tofauti lakini lengo ni lile lile.
I seriously respect your view, lakini naomba nikuulize kwa nini umeng'ang'ania kubaki ndani ya chama wakati uongozi wa juu mzima wa CCM hivi sasa ni wanamtandao? They are ineffective na walikuwa part and parcel of one of the most corrupt and sleazy campaign in the history of Tanzania. Tatizo si kuwa wametenda kosa, tatizo ni kuwa hawataki kukiri na kutubu makosa yao. They think it is just fine. Na watu waadilifu kama nyie FMES, ndo mnawapa nguvu ya kusema kwamba eti bado wanaendelea kupigiwa kura. This has to stop. Mtu ukivuruga basi ni lazima utimuliwe, uende ukajirudi. That is the healthy way. So kama mzalendo, naomba uweke pembeni ushabiki wa chama na upigie kura upinzani kwani kama unaipenda CCM basi kitu pekee kitakachonusuru chama chako ni kama ikishindwa katika uchaguzi halali (isiyochafuliwa na vyombo vya usalama, rushwa n.k.). Otherwise itakuwa kama vyama vya kikomunisti huko Eastern Europe which were dissolved and faded into irrelevance.
Asante mkuu kwa mjadala mzuri.
 
Pundamilia07,
Mkuu sasa hapa mkuu wangu unaharibu mjadala.. mbona unaanza kushambulia watu badala ya hoja?.. iweje unachoona wewe ndio basi chenye busara wakati busara haina formula..Kwa kipimo gani ulichotumia kufikia maamuzi hayo! tupe darasa mwenzetu.
Kisha basi haya maswala ya chama kingine yanatoka wapi, mbona watu wanazungumzia chama CCM na Uongozi wake kukosa mwelekeo..Ndicho chama tawala no doubt, ndiye mlezi wetu sote sasa kama wazee wetu wakiwa bwii wakatembea uchi tusiseme jamani, imekuwa tunavunja heshima sisi kumtazama mzee aliye uchi, kweli ndio hekima na busara hizo mkuu wangu...

FMES,
Mkuu hapa unatafuta pa kutokea.. raia wote wa Tanzania hatuwezi kuwa viongozi.. tuna matatizo yetu kama raia na unaweza kutoa makosa/maradhi yetu kama raia...In my terms Cancer ni matokeo ya maelezo yote ya Mwanakijiji na sidhani kama sisi raia wote tuna dalili au symptons hizo isipokuwa tuna maradhi mengine kama Utapiamlo..Na tuta address maradhi yetu (mapungufu) kwa kutazama tiba ya Utapiamlo..na kwa sababu hizo ndio maana mimi hukubali kuwa sisi Ndivyo Tulivyo!
 
- Then angesema kwanza Upinzani unaongozwa na nani, alinganishe na CCM ili kuipa hoja nguvu ya kielimu, badala ya maneno ya mtaani. Kwa sababu CCM tunao viongozi wetu tuliowachagua tena kwa kura.

FMES!

Hujajibu swali husika. CCM inaongozwa na nani?
 
Je, ipo haja ya haraka kwa Rais Kikwete kuitisha MKUTANO MAALUM WA HALMASHAURI KUU YA TAIFA?
Kwa hizo propaganda zako zenye lengo la ajabu dhidi ya chama tawala, hakuna haja ya kuitisha japo mkutano wa Shina wacha Mkutano Mkuu!

Ta'adabu!
 
Pundamilia07,
Mkuu sasa hapa mkuu wangu unaharibu mjadala.. mbona unaanza kushambulia watu badala ya hoja?.. iweje unachoona wewe ndio basi chenye busara wakati busara haina formula..Kwa kipimo gani ulichotumia kufikia maamuzi hayo! tupe darasa mwenzetu.
Kisha basi haya maswala ya chama kingine yanatoka wapi, mbona watu wanazungumzia chama CCM na Uongozi wake kukosa mwelekeo..Ndicho chama tawala no doubt, ndiye mlezi wetu sote sasa kama wazee wetu wakiwa bwii wakatembea uchi tusiseme jamani, imekuwa tunavunja heshima sisi kumtazama mzee aliye uchi, kweli ndio hekima na busara hizo mkuu wangu...

FMES,
Mkuu hapa unatafuta pa kutokea.. raia wote wa Tanzania hatuwezi kuwa viongozi.. tuna matatizo yetu kama raia na unaweza kutoa makosa/maradhi yetu kama raia...In my terms Cancer ni matokeo ya maelezo yote ya Mwanakijiji na sidhani kama sisi raia wote tuna dalili au symptons hizo isipokuwa tuna maradhi mengine kama Utapiamlo..Na tuta address maradhi yetu (mapungufu) kwa kutazama tiba ya Utapiamlo..na kwa sababu hizo ndio maana mimi hukubali kuwa sisi Ndivyo Tulivyo!

Je, unataka mimi niandike yale wewe unayotaka kuyaona? kama hivyo ndivyo basi andika halafu nitumie mimi nitapost hapa.

Vinginevyo, maelezo yangu yapo very clear na sijamtaja mtu iisipokuwa nina uhakika wale wote wanaojihisi watajitokeza na kajihami wenye.
 
Kwa hizo propaganda zako zenye lengo la ajabu dhidi ya chama tawala, hakuna haja ya kuitisha japo mkutano wa Shina wacha Mkutano Mkuu!

Ta'adabu!

Kibunango,
Hivi huyo jamaa anayetaka Kikwete aitishe mkutano wa Halmashauri Kuu ya CCM, kwanini amtake Kikwete afanye hivyo? hajui CCM inaongozwa na nani, sasa Kikwete katokea wapi? nadhani kwanza aeleze kama anajua CCM anawatambua viongozi then aeleze shida zake.

Pili, huyu anayetaka mikutano ya CCM iitishwe, anayo kadi? na kama anayo kadi ina maana hajui kuwa kuna ngazi tofauti. Mshaurini aanze na kwa mjumbe wa shina lake kwanza, mambo mengine yatamalizwa kwenye tawi lake.
 
Back
Top Bottom