Muongo wewe....
...you must be rushbo republican!
I always admire boldness yako on things you belive, ila pia kuelekea 2010, jihadhari sana na malumbano na ma opportunists watakaoimba nyimbo za shangwe na mapambio kuhusu CCM kwa sababu maalum, ila naamini ukweli wanaujua.
Muongo wewe....
Mkuu FMES sauti ya radi na umeme...heshima.
Kumbuka samaki mmoja akioza basi wote wameoza tambua hilo kwanza.
Lakini hivi leo ni nani anayeweza akakemea?
FMES,
Mkuu wangu maelezo yako mazuri sana kama utabakia ndani ya kabati... lakini ukweli ni kwamba Mwanakijiji kasema kitu kimoja kizito sana!..Yaani sina hata la kusema zaidi ya kujiuliza hivi kweli CCM hawayaoni haya?..
Mkuu wangu CCM ya mwalimu sio hii tena, imepoteza mwelekeo na wala sii kosa la Kikwete kwani naye kaendeleza ya baba yake Mkapa..Maneno haya siyatungi alisema mwenyewe Kikwete na kwa bahati mbaya sidhani kama anaona kuna matatizo ya uongozi ndani isipokuwa matatizo yanatoka nje.
Ni imani ambayo nina hakika CCM wote wanafikiri kuwa matatizo yao yanatoka nje, kuna watu wanafiki washenzi wenye wivu ambao wanataka kuwavuruga kumbe chama chao chenyewe kimekosa mwelekeo..
Mkuu wangu hakuna mtu hata mmoja anayetaka kujiunga na vyama nje ya CCM wala Chadema isingekuwepo for the same of making multi party isipokuwa CCM imepoteza mwelekeo na mambo mengi sana ukiyasoma ndani ya Chadema ni yale yaliyokuwa yakiaminiwa na wananchi toka tupate Uhuru...
Haiwezekani hata kidogo lawama hizi ukazipeleka kwa Nyerere kwa sababu ya viongozi waliokuwepo kuwa kizazi chake, mkuu wangu hata wewe na mimi sote ni kizazi cha mwalimu na ndio maana tumeweza kuona tofauti hizo.. Sii lazima wewe uwe na tabia sawa na baba yako wala character zako haziwezi kutokana na malezi ya baba yako..watoto wawili mnaweza kuwa tofauti kabisa baina yenu na tofauti na baba yenu..ila unaweza fuata profession ya baba yako na sii lazima ukawa mzuri/mbaya kama baba yako..
Kinachotokea leo CCM naogopa kusema ni CANCER ndani ya chama na kinajimaliza chenyewe.. hizo nguvu anazotangaza malecela na wengine ni aibu ya mgonjwa ambaye ananyonyoka nywele kwa sababu ndani ya akili yake anafikiria ana HIV hivyo ni aibu kwa jamii..
Maradhi ya CCM sio aibu wala sio HIV ni cancer na mkiwahi mnaweza kupata tiba!..
Heko mwanakijiji kwani sio kila siku tunawaponda CCM bila kuwapa mwanga wakayajua mapungufu yao...
OK nimekupata FMES lakini CCM ya sasa si CCM ya enzi ya akina mzee Julius siku hizi watu wamejaa unafiki mwingi na woga na kuwatukuza watu wasio stahili kila siku.
- Wa-Tanzania wote tuko hivyo tunaktaa upande mmoja lakini tunakubali wa pili, according to our interest, ndio cancer yenyewe ya taifa. Otherwise nimekusikia sana mkuu.
Respect
FMES!
Ndo hapo sasa nini kifanyike?
- Roma haikujengwa kwa siku moja mkuu, hivi unajua kuwa kuna wakati according to the history kule Europe, ilikuwa kuwa na choo ndani ya nyumba ni crime against the law of the land!
- Pole pole na mwendo wetu huu wa kibongo bongo tutafika tuu!
Respect!
FMES!
Nadhani umegusia ishu nzuri kuhusu Mwl Nyerere, mimi nasema you have answered the question, kama nchi imeoza na Mwalimu Nyerere ndo chanzo cha uongozi mzima wa leo, basi Nyerere was a lousy leader, I have no problem saying that.Then inakuja hoja ya kumuingizia Mwalimu, kwamba Mwalimu was best lakini CCM ya sasa ina problem, ninasema hizi ndio njia rahisi rahisi tulizoziwea wabongo za kutafuta majibu ya mawswali mazito, kwa sababu ukweli ni kwamba 95% ya viongozi wa ngazi mbali mbali tulionao leo Tanzania kuanzia CCM mpaka Upinzani ni creation ya Mwalimu, sasa mnatuambia nini kuhusu Mwalimu?
As a student of history nakataa kwani ukiangalia historia ya USA, walizaliwa katika mfumo wa multiparty demokrasia unaoheshimu property rights. Ni kweli walikuwa na utumwa na kadhalika lakini the environment that was created, the constitution that was written including its flexibility of the the Bills of Rights foresaw possbile changes in the future and came up with a way to address it, including an independent judiciary.hao US na Europe, ambao mara kwa mara ndio standard zetu hapa JF wamepitia miaka 300 sisi ndio kwanza tupo miaka 47, sasa 300-47= 253, eti unaweza kui-cover miaka 253 kwa miaka 14 tu toka tuamke na kuanza ku-practice Demokrasia, haiwezekani, lakini have we made some progress yes! tena a big one ingawa sio kwa speed ambayo wengi tunaitaka hapa JF.
I seriously respect your view, lakini naomba nikuulize kwa nini umeng'ang'ania kubaki ndani ya chama wakati uongozi wa juu mzima wa CCM hivi sasa ni wanamtandao? They are ineffective na walikuwa part and parcel of one of the most corrupt and sleazy campaign in the history of Tanzania. Tatizo si kuwa wametenda kosa, tatizo ni kuwa hawataki kukiri na kutubu makosa yao. They think it is just fine. Na watu waadilifu kama nyie FMES, ndo mnawapa nguvu ya kusema kwamba eti bado wanaendelea kupigiwa kura. This has to stop. Mtu ukivuruga basi ni lazima utimuliwe, uende ukajirudi. That is the healthy way. So kama mzalendo, naomba uweke pembeni ushabiki wa chama na upigie kura upinzani kwani kama unaipenda CCM basi kitu pekee kitakachonusuru chama chako ni kama ikishindwa katika uchaguzi halali (isiyochafuliwa na vyombo vya usalama, rushwa n.k.). Otherwise itakuwa kama vyama vya kikomunisti huko Eastern Europe which were dissolved and faded into irrelevance.kama wananchi wengine wanavyoamini kwamba dawa ni kuwa mpinzani kuweza kurekebisha mimi ninaamini ninaweza kwa kuanzia ndani ya CCM, kwa hiyo ni mtizamo tofauti lakini lengo ni lile lile.
- Then angesema kwanza Upinzani unaongozwa na nani, alinganishe na CCM ili kuipa hoja nguvu ya kielimu, badala ya maneno ya mtaani. Kwa sababu CCM tunao viongozi wetu tuliowachagua tena kwa kura.
FMES!
Kwa hizo propaganda zako zenye lengo la ajabu dhidi ya chama tawala, hakuna haja ya kuitisha japo mkutano wa Shina wacha Mkutano Mkuu!Je, ipo haja ya haraka kwa Rais Kikwete kuitisha MKUTANO MAALUM WA HALMASHAURI KUU YA TAIFA?
Pundamilia07,
Mkuu sasa hapa mkuu wangu unaharibu mjadala.. mbona unaanza kushambulia watu badala ya hoja?.. iweje unachoona wewe ndio basi chenye busara wakati busara haina formula..Kwa kipimo gani ulichotumia kufikia maamuzi hayo! tupe darasa mwenzetu.
Kisha basi haya maswala ya chama kingine yanatoka wapi, mbona watu wanazungumzia chama CCM na Uongozi wake kukosa mwelekeo..Ndicho chama tawala no doubt, ndiye mlezi wetu sote sasa kama wazee wetu wakiwa bwii wakatembea uchi tusiseme jamani, imekuwa tunavunja heshima sisi kumtazama mzee aliye uchi, kweli ndio hekima na busara hizo mkuu wangu...
FMES,
Mkuu hapa unatafuta pa kutokea.. raia wote wa Tanzania hatuwezi kuwa viongozi.. tuna matatizo yetu kama raia na unaweza kutoa makosa/maradhi yetu kama raia...In my terms Cancer ni matokeo ya maelezo yote ya Mwanakijiji na sidhani kama sisi raia wote tuna dalili au symptons hizo isipokuwa tuna maradhi mengine kama Utapiamlo..Na tuta address maradhi yetu (mapungufu) kwa kutazama tiba ya Utapiamlo..na kwa sababu hizo ndio maana mimi hukubali kuwa sisi Ndivyo Tulivyo!
Kwa hizo propaganda zako zenye lengo la ajabu dhidi ya chama tawala, hakuna haja ya kuitisha japo mkutano wa Shina wacha Mkutano Mkuu!
Ta'adabu!