Adolph Jr
JF-Expert Member
- Nov 5, 2016
- 5,950
- 9,511
Lebanon imekuwa chini ya mashambulizi makali ya makombora kutoka kwa Israel katika muda wa wiki mbili zilizopita, ambayo yameua zaidi ya watu 1,000, na eneo lake limevamiwa na wanajeshi wa Israel. Hii ni kwa sababu ya mzozo wa sasa kati ya Israel na Hezbollah - chama cha kisiasa na wanamgambo ambao wanaishi nchini humo.
Wanamgambo wa Hezbollah wana nguvu zaidi kuliko jeshi la kitaifa la Lebanon na wanaungwa mkono na watu wengi, haswa miongoni mwa Waislamu wa Shia wa nchi hiyo.
Sio shirika rasmi la serikali, lakini limekuwa jeshi kubwa ndani ya Lebanon katika miongo minne iliyopita.
Kwa mujibu wa mkataba uliokubaliwa mwaka 1943, wakati Lebanon ilipopata uhuru kutoka kwa Ufaransa, rais alitakiwa kuwa Mkristo kutoka madhehebu ya Wamaroni, waziri mkuu Muislamu wa Sunni na spika wa bunge Muislamu wa Shia.
Hii ilionyesha ukubwa wa vikundi tofauti vya kidini huko Lebanon wakati huo.Wakati huo Wakristo walikuwa zaidi ya nusu ya idadi ya watu, zaidi ya Waislamu wa Sunni na Shia.
Hata hivyo, wengi wanasema makubaliano hayo yamepitwa na wakati kwa vile Wakristo, Waislamu wa Sunni na Waislamu wa Shia sasa wanakadiriwa kuwa zaidi ya asilimia 30 ya watu wote kila mmoja.
Kwa makubaliano, Wakristo na Waislamu pia wana idadi sawa ya viti bungeni, ingawa Waislamu kwa jumla sasa ndio wanasheheni idadi kubwa ya watu.
Kiuhalisia, hakuna chama kimoja au madhehebu ya kidini yenye mamlaka ya jumla nchini Lebanon. Serikali zinaundwa na miungano ya wabunge, na maamuzi yote makubwa yanapaswa kuchukuliwa kwa makubaliano. Hii mara nyingi husababisha migogoro ya kisiasa.
Hezbollah ilianzishwa kama wanamgambo wa kiislamu wa madhehebu ya Shia mwaka 1982, wakati wa vita vya wenyewe kwa wenyewe vya Lebanon, ili kupinga majeshi ya Israel ambayo yalikuwa yameikalia kwa mabavu kusini mwa Lebanon mwaka huo.
Imekuwa na silaha nyingi na kufadhiliwa na Jamhuri ya Kiislamu ya Iran.
Hezbollah kwa Kiarabu ni "chama cha Mungu".
Hezbollah ilitangaza rasmi kuwepo kwake mwaka 1985, na kutangaza kuwa inataka kuanzisha taifa la Kiislamu nchini Lebanon, kama lile la Iran. Pia iliapa kukomesha ukaliaji wa Israel kusini mwa Lebanon na maeneo ya Palestina.
Mnamo 2009, ilitoa ilani mpya ambayo haikurejelea kuunda serikali ya Kiislamu. Hata hivyo, ilidumisha msimamo wake dhidi ya Israeli.
Vita vya wenyewe kwa wenyewe vya Lebanon vilipoisha mwaka wa 1990, pande zote zinazopigana zilivunja wanamgambo wao. Walakini, Hezbollah ilibaki. Ilisema ilihitaji kupambana na uvamizi wa Israel kusini.
Israel hatimaye iliondoa majeshi yake katika eneo hilo mwaka 2000, na Hezbollah ikadai kuibuka na ushindi.
eneo hilo mwaka 2000, na Hezbollah ikadai kuibuka na ushindi.
Chanzo cha picha,Getty Images
Mnamo 1992,
Hezbollah ilianza kuwasimamisha wagombea ubunge.
Sasa ina wabunge kadhaa, na kuna mawaziri wa Hezbollah serikalini.
Pia hutoa vitu kama vile shule, huduma za afya na huduma za kijamii katika maeneo ya Lebanon yenye jamii kubwa za WaShia.
Vyama vingine nchini Lebanon pia vinatoa huduma kama hizo kwa wapiga kura wao, lakini Hezbollah inaaminika kuwa na mtandao mpana kuliko wote.
Nguvu kubwa ya Hezbollah ipo kwa wanamgambo wake. Inasema ina wapiganaji 100,000, ingawa makadirio huru yanaweka idadi hiyo kati ya 20,000 na 50,000.
Hezbollah pia ina silaha kati ya roketi 120,000 na 200,000 na makombora, kulingana na shirika lenye makao yake nchini Marekani, Kituo cha Mafunzo ya Kimkakati na Kimataifa.
Hili linasemekana kuwa mojawapo ya majeshi yasiyo ya serikali yenye nguvu zaidi duniani. Inachukuliwa kuwa na nguvu zaidi kuliko jeshi la kitaifa la Lebanon.
Pia imefaidika kutokana na udhaifu wa serikali ya kitaifa ya Lebanon. Kwa mfano, nchi imekuwa bila rais tangu 2022, kwa sababu vyama vya siasa haviwezi kukubaliana nani awe rais wa nchi hiyo. Serikali kuu haijawa na nguvu za kutosha kuzuia Hezbollah kutekeleza ajenda yake yenyewe.
Source: BBC SWAHILI
Wanamgambo wa Hezbollah wana nguvu zaidi kuliko jeshi la kitaifa la Lebanon na wanaungwa mkono na watu wengi, haswa miongoni mwa Waislamu wa Shia wa nchi hiyo.
Sio shirika rasmi la serikali, lakini limekuwa jeshi kubwa ndani ya Lebanon katika miongo minne iliyopita.
Nani aniaongoza Lebanon?
Nchini Lebanon, mamlaka ya kisiasa yamegawanywa kati ya madhehebu mbalimbali ya kidini ndani yake.Kwa mujibu wa mkataba uliokubaliwa mwaka 1943, wakati Lebanon ilipopata uhuru kutoka kwa Ufaransa, rais alitakiwa kuwa Mkristo kutoka madhehebu ya Wamaroni, waziri mkuu Muislamu wa Sunni na spika wa bunge Muislamu wa Shia.
Hii ilionyesha ukubwa wa vikundi tofauti vya kidini huko Lebanon wakati huo.Wakati huo Wakristo walikuwa zaidi ya nusu ya idadi ya watu, zaidi ya Waislamu wa Sunni na Shia.
Hata hivyo, wengi wanasema makubaliano hayo yamepitwa na wakati kwa vile Wakristo, Waislamu wa Sunni na Waislamu wa Shia sasa wanakadiriwa kuwa zaidi ya asilimia 30 ya watu wote kila mmoja.
Kwa makubaliano, Wakristo na Waislamu pia wana idadi sawa ya viti bungeni, ingawa Waislamu kwa jumla sasa ndio wanasheheni idadi kubwa ya watu.
Kiuhalisia, hakuna chama kimoja au madhehebu ya kidini yenye mamlaka ya jumla nchini Lebanon. Serikali zinaundwa na miungano ya wabunge, na maamuzi yote makubwa yanapaswa kuchukuliwa kwa makubaliano. Hii mara nyingi husababisha migogoro ya kisiasa.
Hezbollah ilianzishwa kama wanamgambo wa kiislamu wa madhehebu ya Shia mwaka 1982, wakati wa vita vya wenyewe kwa wenyewe vya Lebanon, ili kupinga majeshi ya Israel ambayo yalikuwa yameikalia kwa mabavu kusini mwa Lebanon mwaka huo.
Imekuwa na silaha nyingi na kufadhiliwa na Jamhuri ya Kiislamu ya Iran.
Hezbollah kwa Kiarabu ni "chama cha Mungu".
Hezbollah ilitangaza rasmi kuwepo kwake mwaka 1985, na kutangaza kuwa inataka kuanzisha taifa la Kiislamu nchini Lebanon, kama lile la Iran. Pia iliapa kukomesha ukaliaji wa Israel kusini mwa Lebanon na maeneo ya Palestina.
Mnamo 2009, ilitoa ilani mpya ambayo haikurejelea kuunda serikali ya Kiislamu. Hata hivyo, ilidumisha msimamo wake dhidi ya Israeli.
Vita vya wenyewe kwa wenyewe vya Lebanon vilipoisha mwaka wa 1990, pande zote zinazopigana zilivunja wanamgambo wao. Walakini, Hezbollah ilibaki. Ilisema ilihitaji kupambana na uvamizi wa Israel kusini.
Israel hatimaye iliondoa majeshi yake katika eneo hilo mwaka 2000, na Hezbollah ikadai kuibuka na ushindi.
eneo hilo mwaka 2000, na Hezbollah ikadai kuibuka na ushindi.
Chanzo cha picha,Getty Images
Mnamo 1992,
Hezbollah ilianza kuwasimamisha wagombea ubunge.
Sasa ina wabunge kadhaa, na kuna mawaziri wa Hezbollah serikalini.
Pia hutoa vitu kama vile shule, huduma za afya na huduma za kijamii katika maeneo ya Lebanon yenye jamii kubwa za WaShia.
Vyama vingine nchini Lebanon pia vinatoa huduma kama hizo kwa wapiga kura wao, lakini Hezbollah inaaminika kuwa na mtandao mpana kuliko wote.
Je, Hezbollah imekuaje na nguvu nchini Lebanon?