Nani anajali hatima ya Tanzania?

Nani anajali hatima ya Tanzania?

Na Edo Kumwembe

Ni nchi ya ajabu kwa mwanadamu makini kuweza kuishi. Ni nchi inayoshangaza sana, ingawa raia wake hawaonyeshi kushangazwa na matukio kadhaa yanayotokea.

Naizungumzia Tanzania nchi niliyoishi kwa miongo kadhaa tangu nizaliwe. Baada ya nyimbo nyingi za matatizo, dhiki, wizi, rushwa, tabu, magonjwa na kila aina ya shida ambayo mwanadamu wa kawaida anapitia, jawabu kubwa linapatika kwa swali; nani anajali?Ndio, nani anajali? Hili ni swali ambalo kila Mtanzania anapaswa kuulizwa.

Ni kwa kiasi gani, mwananchi wa kawaida, kiongozi au muhusika yeyote wa nchi hii anajali matatizo ya nchi yetu.Nimejaribu kwa kiasi kikubwa kutazama sura za viongozi wetu, mawaziri, wabunge, Wakurugenzi, Mameneja na kila kiongozi. Sioni anayejali.Wengi wanaongea wasichofikiria kukifanya kwa dhati na nchi imezidi kuoza.

Akili zao ziko katika wizi kwa sababu na wananchi wenyewe wala viongozi wengine hawajali.Nchi inatafunwa kila jua linapochomoza na kuzama. Hakuna anayejali na kila mtu anaangalia maisha yake. Msukuma mkokoteni haoni ni kwa namna gani anahusika na Waziri mwizi wala Mkurugenzi wa Manispaa mla rushwa.

Atajihusisha vipi? Kwa nini atumie muda wake mwingi kujali? Kama watu wanaomzunguka hawajali kula yake kwa nini na yeye awe anajali maisha ya wengine.Siwezi kusema nilifaidi matunda ya utawala wa Mwalimu Nyerere. Sijui mengi yaliyotokea wakati wa Utawala wake, lakini tangu nilipopata akili timamu sijawahi kusikia Rais wa nchi yangu akimfukuza kazi Waziri wake kwa rushwa wala wizi.

Je ni kweli kwamba marais wangu hawawaoni Mawaziri wezi na wala rushwa? Kama wangekuwa watiifu na waadilifu basi nchi yetu ingekuwa mbali. Lakini naamini wanawaona, kikubwa ni kwa vile hawajali kinachotokea. Hawajali kwa sababu hawana sababu ya kujali. Kwa kuwa wananchi hawajali basi na wao hawajali kama ambavyo wananchi hawajali.

Wanaendelea kutojali na daima tunaendelea kupata vizazi vya Watanzania wasiojali.Kwani tukifungua mikataba ya ajabu ya Madini hatuwaoni walioweka saini hizo? Tunawaona, lakini nani anajali? Nchi inasonga mbele na maisha yanaendelea. Huyu anajaribu kuandika gazetini kwa uchungu na yule anatamka lile katika kipindi cha redio kwa uchungu, lakini nani anajali?

Kina mama na watoto wanafungulia michezo ya maigizo ITV na kwingineko. Nani atawalaumu wakati watu makini wenyewe hawajali? Si afadhali nao wasijali!Kwani yuko wapi yule Waziri aliyesema yuko tayari kuona wananchi wanakula majani ili ndege ya Rais inunuliwe? Ndege ambayo ni mbovu!. Si amechaguliwa tena kuwa Waziri? Nani anajali kama Rais wa sasa hakujali? Mimi nitajali nini?

Ni mwananchi gani anajali? Walio wengi wanafanya maaandamano katika mikasa ya kidini au ile ya kumpongeza Rais aliyefutiwa madeni ambayo fedha zake zilitumiwa kununua mashangingi.Kuna anayejali kwenda katika maandamano ya kupinga kupanda kwa bei ya umeme? Kuna anayejali kuandamana baada ya kusikia Nesi amesababisha kichanga kufa sekunde chache baada ya mama mjamzito kujifungua?

Hakuna anayejali kwa sababu hata akiandamana kwa uchungu mkubwa, Rais hawezi kumwajibisha Waziri wa Afya!. Ndivyo nchi ilivyo na watu wengi wamekwenda jela baada ya kutoa taarifa njema kwa jeshi la Polisi. Lakini nani anajali kuwepo kwao jela?

Ukitoa taarifa kuhusiana na mkubwa fulani anayepokea rushwa, kesho yake Kamanda wa Polisi wa Mkoa anakuonya na kukwambia uachane naye.Kwa nini niendelee kujali kwa watu ambao hawajali? Watu wangapi walishikwa na madawa ya kulevya katika Uwanja wa ndege wa kimataifa wa Dar es salaam lakini wapo nje kwa madai kwamba uchunguzi unaendelea?

Uchunguzi upi wakati madawa yalitolewa tumboni na tukaonyeshwa katika taarifa za habari za Televisheni mbalimbali? Kwa nini niendelee kujali kuwepo nje kwa mtuhumiwa wakati Kamanda wa Polisi wa mkoa haonyeshi kujali?Yuko wapi dada machachari Mbunge wa kike aliyedai kwamba ana majina ya wauza madawa wa kulevya?

Ni kweli kwamba alizungumza jambo jipya katika jamii yetu ya watu wasiojali? Tunao watu wengi wanaouza madawa na kwa bahati wanajulikana, lakini nani anajali? Dada yule ‘alionyesha’ kujali, lakini baada ya hapo nani amejali? Mbona hatujasikia mtu amekwenda ndani kutokana na mdomo wake?

Tangu baada ya ‘mauaji’ ya basi ya Buffalo, magari yanazidi kwenda kasi barabarani. Nani anajali? Si mpaka watu wengine wafe ndio tusikie tamko jingine la kinafiki?Kuna meli ngapi mbovu pale Ziwa Victoria na sehemu nyingine zenye vyombo vya usafiri wa majini? Kwa sababu hakuna anayekufa kwa sasa wahusika na wananchi hawajali mpaka litokee janga.

Ili mradi asubuhi inafika, mchana unapita na jioni inawadia basi hakuna anayejali mpaka litokee janga. Nani anajali?Mchele mbovu unahalalishwa, watu wanatengeza maji ya ‘kufoji’ na kuuza, nani anajali? Nikienda kusema Polisi wananitazama kwa jicho la chuki lakini tayari nimeshawaachia mianya ya rushwa. Keshokutwa nakutana na mkubwa wa Polisi niliyemshtua akiwa pamoja na mkuu wa Kiwanda nilichokishtaki.

Wanakula ‘kitimoto’ pamoja na wanacheka vilivyo, nani anajali?Kuna watu wachache walikiweka mikononi Chama cha soka nchini FAT,enzi hizo. Nani alijali? Kama si kuvurugana wenyewe kwa wenyewe wangeweza kuwepo mpaka leo.Ndio, Rais wa nchi alikuwepo, lakini hakuwa na muda wa kujali. Kipaza sauti kilikuwa kinamwambia asijali mambo hayo ila aelekeze macho katika Utandawazi.

Ndio, utandawazi ambao unaruhusu tupeleke makontena ya mchanga uliochanganyika na dhahabu nje ya mipaka yetu. Nani anajali?Wachache wanajaribu kujali lakini nani anawasikia? Wenyewe wanakutana Golden Tulip wakila firigisi na kupeana ruhusa hizo. Mimi na wewe tujali nini wakati hatuna uhakika wa kesho? Tukipata watoto nao wanaingia katika mkumbo huo huo wa kutojali.

Kizazi hiki ambacho watoto wengi wamegeukia hisia za kimagharibi ni yupi kati yao anaweza kujali?Wa kiume anakazania kusuka, wa kike anatamani kuvaa kama Beyonce. Hakuna hata mmoja mwenye hisia na nchi. Hawezi kujali kwa sababu hajafundishwa kujali. Ukisikiliza maoni ya wengi kuhusiana na kesi ya Justine Kasusura, wengi wanamlaumu kwa nini hakutoweka nje ya nchi.

Hakuna anayesikitika kwa kitendo chake cha kuiba fedha. Kwa nini?Watu hawajali alichokifanya. Yeye alifanya hadharani lakini kuna wanaoiba kwa karatasi? Hawa akina ‘Kasusura’ wa mezani nani anawazuia? Nani anawajali?Iko wapi Kampuni ya Richmond? Mbona kimya? Nani anajali? Kwa sasa umeme upo na watu hawajali tena. Wanataka ije ‘Richmond’ nyingine ya Maji au huduma za Afya.

Nani anajali? Ndio, sijawahi na wala sitaki kupiga kura. Yupo atakayesema napoteza haki yangu ya msingi. Simuoni wa kunijali na hata kama akiamua kunijali basi mfumo hauwezi kumsapoti anijali.Wakati wananchi wengine wakipiga kura mimi naangalia vipindi vya soka katika Televisheni, kwa nini uniambie sijali wakati atakayechaguliwa hatanijali?

Katika kituo cha wapiga kura chenye wakazi 1000 lakini mshindi ameshinda kwa kura 1200, kwa nini nijali kusumbuka juani huku FFU wakinighasi wakati waliopanga matokeo hawaijali kura yangu?Nijali nini hasa kwa kutompigia kura mtu atakayekwenda bungeni kupitisha sheria ya Takrima? Acha nifuatilie Ligi kuu ya England na utamu wake.

Soma magazeti yetu ya leo. Watu wameamua kuandika mambo laini ambayo si sehemu ya mapambano yetu. Makala za leo ni zile zile zinazoelezea kwa undani Habari za Theolojia, Ulokole, na mambo mengine. Mwananchi asiye na uhakika na machweo ataelewa nini na kupata tumaini jema katika makala hizi? Wanaoziandika hawajali kinachotokea kwa sasa.

Kwetu, kiongozi kutajwa anamiliki hiki na kile kwa jina la mwanae, si kashfa. Kwetu, mtoto wa mkubwa au mkubwa mwenyewe kuua si jambo la ajabu sana. Nani anajali? Wao na Kamanda wa Polisi wanakutana Kilimanjaro Kempsky katika dhifa mbalimbali, unajua wanaongea nini? Kwa nini ujitie kimbelembele cha kujali? Ili mradi unapumua, iangalie siku yako ya kesho.

Tanzania ya leo imejaa watu wanaozijali familia zao. Nani atawalaumu watu hawa? Kwani viongozi wetu wanawajali kina nani? Si wanajali elimu za watoto wao pale Oxford, Havard na kwingineko?Kama unabisha, mbona sasa hivi ndio wanatuongoza? Nani anajali? Tuna uhakika gani kama baadaye wajukuu hawataongoza? Si ndio wanapewa ukamanda wa vijana wakijiandaa kumtawala mwanangu ambaye ni mnyonge wa baadaye?

Nani anajali?Sina hasira na mtu. Nina furaha na maisha yangu kwa sababu napata ninachokitaka kwa uhalali. Kama maisha yataendelea kuwa hivi basi nisilaumiwe kwa kutojali. Nina uhakika gani kama wenzangu wanajali?Kilio kama changu kimetamkwa mara ngapi na watu makini? Nani amejali? Kelele za mchanga wa dhahabu nani amezijali? Waliongia mikabata mibovu ya madini nani anawajali? Wangekuwa Chini, Japan, Uingereza na kwingineko, wangekuwa wapi watu hawa kama si katika kuta za Gereza?

Hapa kwetu nani anajali?Lakini nijali nini zaidi wakati Rais wa nchi aliwahi kuwatamkia watu walioelezea hisia zao kwa Waziri Mkuu wake kuhusu umilione wake wa mashaka, kwamba wana wivu? Kama yeye mtu wa juu kabisa hakujali, nani atajali? Utawala ule ulikumbana na migomo ya wanafunzi, huu nao unakumbana na migomo hiyo hiyo, nani anajali? Kuna njia za kudumu za kumaliza migomo hiyo ambayo nimeisikia tangu utotoni mwangu?

Huyu anakabiliana nayo leo, akihamishiwa anahama na hisia zake.

Yule anakuja na hisia nyingine na wala hajali kutazama alipoishia mwenzake. Leo, kuna watu wengi wanapiga kelele kuhusiana na hatari ya kujiunga na Jumuiya ya Afrika Mashariki. Nani anawasikiliza? Mimi naweza kuwa sehemu ya maamuzi hayo?Wanaotoa tahadhari ni watu wasomi. Afadhali ingekuwa kwangu mtu nisiye na elimu, lakini wanaotoa tahadhari hizi ni watu wanaoheshimika kwa elimu na upeo wao.

Najua hawasikilizwi lakini nani anajali? Kama wenzao hawajali, nani atanisikiliza mimi nisiye na lolote? Acha waamue nami nitatii kwani waliamua mangapi ya hatari na nimeendelea kutii? SijaliLakini kwa nini nimewang’angania wasiojali wakati hata wenyewe wakifa au kuondoka madarakani hakuna anayewajali? Wako wapi waliojali ambao familia zao zinaishi kama vile baba zao hawakujali? Ndio, familia za akina Edward Sokoine.

Nina uhakika watoto wao watajuta kwa kitendo cha baba yao kujali sana wakati wa utawala wake.Ndio, na hata ninapomaliza kuandika makala hii, wengi wataelewa ninachomaanisha. Wakubwa wengi na watu wa kawaida wataisoma na kuielewa.

Lakini nani atajali?

kuna hii na hii hapa

Anayeuza meno ya Tembo anapomlaumu Ngassa

NA EDO KUMWEMBE
WAKATI mwingine hakuna unachoweza kufanya zaidi ya kucheka. Hata kama haucheki usoni. Unacheka moyoni na kujiuliza, ni namna gani Kigogo anayehusika na wizi wa Meno wa Tembo anavyokandia uwezo wa Mrisho Ngassa.

Ndio, unakutana na Mbunge Kigogo. Jina lake linatajwa katika wizi wa Meno ya Tembo. Anakwambia “Hivi Edo unataka kuniambia niache kushangilia Manchester nije kutazama Taifa Stars. Hatujui mpira sisi Watanzania”. Moyoni namjibu, kweli hatujui mpira, lakini kulinda Rasilimali zetu kama Meno ya Tembo unayoiba ndio tumeweza?

Unajiuliza, sawa sisi hatujui mpira, lakini tumefanikiwa katika nini hasa? Barabara? Madini? Kilimo? Siasa? Elimu? Hapana. Hatimaye tumefika katika nyakati ambazo Taifa kama Taifa limekwama. Ni kitu gani kingine cha kujivunia wakati unapoponda soka la Tanzania? Hakuna.

Aliyempa tenda mkandarasi mbovu kujenga barabara mbovu ya Kilwa, naye anauponda mpira wa Tanzania.

Aliyesaini mkataba mbovu wa Madini ambao unaruhusu Mzungu kuchota Madini yetu atakavyo, naye anamponda kocha wa Taifa Stars na wachezaji wake.

Anayeongeza sifuri katika hesabu ya safari za Rais Ulaya naye akikutana na Watanzania wanaoshi nje anauponda mpira wa Tanzania. Yeye ni Mwizi mzuri tu, lakini wala haoni hesabu za wizi wake zinavyoshindwa kusomesha walimu wa soka nje ya nchi.

Umewahi kumsikia Mbunge wa kile Chama akiponda wachezaji wa Tanzania? Lakini ndiye huyo huyo aliyegonga meza na wenzake kupitisha bajeti ya Wizara ya Elimu na Michezo na wakaipa shilingi 600 milioni. Huo ni mshahara wa wiki moja wa mchezaji anayetoka nchi ya Afrika anayecheza Ulaya, Yaya Toure. Bajeti hii ya mshahara wa wiki wa Yaya Toure inainuaje soka?

Anayepaswa kutatua tatizo la foleni jiji la Dar es salaam akashindwa na kujiongezea posho za kijinga kila siku naye analaumu matokeo mabovu ya timu ya Taifa na viwango vibovu vya Simba, Yanga, Azam katika michuano ya Caf.

Kigogo wa TRA ni shabiki mzuri wa Arsenal. Anamsaidia yule Mfanyabiashara maarufu kukwepa kodi. Hajui kwamba pesa tunayopoteza ingesaidia uchumi wa nchi na michezo wa ujumla. Hapa huwa ananiacha hoi kweli kweli.

Lakini anauchekaje mchezo wa soka? Kama mchezo wa soka umefeli, kwani hajui ni kwa kiasi gani Tanzania imefeli katika kukusanya kodi nyingi miongoni mwa nchi za Afrika? Hapa si ndio nchi ambayo Mfanyabiashara anapewa miaka mitano ya kutolipa kodi mpaka ajue faida ya biashara yake? Wenyewe wanaita kwa kizungu Tax Holiday.

Kigogo wa Wizara nyeti ya ulinzi anamlinda Kigogo mwenzake aliyebaka mtoto wa kiume. Wakiimaliza kesi kituo cha Polisi wanaitana Serena Hoteli kupongezana kwa kula mishkaki huku wanacheki mechi ya Taifa Stars dhidi ya Ivory Coast TBC. Tukifungwa wanasema hatujui mpira na wachezaji wetu ni duni.

Unajiuliza, kwani mchezaji wa Tanzania si anatokana na mtoto wa Kitanzania? Mbona wametoka kumkandamiza mtoto wa Kitanzania? Naishia kucheka taratibu kwa uchungu.

Mchezaji mwenye kipaji kama Haruna Moshi ‘Boban’ hajaweza kung’ara Ulaya. Kuna tofauti gani na Mlima Kilimanjaro kushindwa kusaidia uchumi wa Taifa lake zaidi ya ilivyo sasa. Kuna tofauti gani na Mtanzania kufa njaa wakati ana ardhi kilomita nyingi zenye rutuba?

Mwisho wa yote tunaishi katika Taifa lililooza. Taifa lisilo na maadili katika uchumi, jamii na siasa. Kila unapowaza unakubali kwamba soka la Tanzania lipo chini na limeoza. Hatuonyeshi matumaini. Lakini niambieni ni wapi kuna matumaini na nidhamu?

Tatizo limebaki kwa Mtanzania mwenyewe. Hana uzalendo, ubunifu na umakini. Niambieni ni nani halaumiwi? Mwandishi wa habari? Mchezaji? Polisi? Rais? Mbunge? Mwanajeshi? Daktari? Mmachinga? Mfanyabiashara? Mkulima? Kila mtu haifanyi kazi yake sawa sawa.

Ni kweli. Tumekosa dira kama taifa. Hatujui tulipo wala tunapokwenda. Kabla haujamlaumu mwenzako jiulize, wewe unaifanyia nini nchi yako. je wewe Sekta yako ina maendeleo yanayostahili kabla ya kumnyooshea kidole mwingine?
Huwa nawaza sana.

Daktari aliyemfanyia operesheni ya kichwa mtu anayestahili kufanyiwa operesheni ya goti, naye anamlaumu Polisi aliyechukua rushwa jana Kariakoo.

Na yule polisi naye analaumu matokeo mabovu ya timu ya taifa. Na hata wachezaji wa timu ya taifa wanalalamika kuwa Rais anaendesha nchi hovyo. Rais naye ana malalamiko yake mengi kwa wananchi wa Mtwara kukataa gesi kutoka kusini.

kila mtu anamlaumu mwingine. Cheni ya lawama inakuwa ndefu, lakini mwisho wa siku ukweli unabakia pale pale kwamba Taifa limekosa maadili. Nani yuko salama na nani anafanya kazi yake kwa maadili makubwa?. Hakuna.

Kigogo anayeongoza Bandari anajifanya analaumu kwanini wachezaji wa Tanzania hawachezi Ulaya. Wala hajiulizi kwanini chini ya Bandari yake uchumi wa Tanzania usiongoze Afrika Mashariki na kati na baadhi ya nchi za Ulaya zisizo na Bandari.

Wabrazil wanakosea kwingine, lakini mpira wanajua. Wachina wanakosea katika mpira, lakini uchumi wanajua. Wamarekani wanakosea katika moja kidogo, lakini jingine wanafahamu. Ethiopia wana umaskini, lakini katika riadha wanapatia. Katika soka wanajitokeza.

Tanzania tunafahamu nini zaidi? Tumepatia wapi hadi tuseme mpira ni tatizo sana? wasomi na wananchi wa kawaida tuanze kuitafakari nchi kwa pamoja. Tusitafakari kwa mapande mapande. Tuna tatizo kila sehemu. Nani hajawahi kulaumiwa au kulaumu? Kila mtu tatizo nchi hii…

aisee...!!
 
Naamin maskini akichoka ni mtu mbaya sana... kuna siku watu watachoka na hizi habar. ... thats y siipend siasa ya tanzania.
 
Na Edo Kumwembe

Ni nchi ya ajabu kwa mwanadamu makini kuweza kuishi. Ni nchi inayoshangaza sana, ingawa raia wake hawaonyeshi kushangazwa na matukio kadhaa yanayotokea.

Leo nimeona trafiki anakamata daladala kiukweli bila sababu ya msingi kwa maana daladala nyingi ni mbovu. Basi akawa anamwandikia faini na nikawa najaribu kuwaza ni kiasi gani daladala anapata mpaka aweze kulipa faini ya 30,000/-!
Sasa ndani ya gari wamejaa abiria hata pa kujigeuzia hamna lakini hakuna hata mmoja anayeonekana kupinga ule uonevu, na hata mama mmoja aliyejaribu kuongea unaona kabisa ni kujitutumua kwa woga wa hali ya juu usio na matendo. Ndio niakjua kuwa kwa mtaji huu katiba ya Chenge haina kizuizi!

Kapten Komba anasema Mzee Joseph Sinde Warioba hana maadili ndani ya BMK, wenzake wanashangilia kama mazuzu
 
kaka edo angalia kaka...punguza spidi...dakika sifuri tu unaweza kumfuata AMINA. Tulia na endelea kutojali...!! Ngoja tuwahi mechi ya Liverpool na Everton.
 
Nchi iko mikononi mwa mapanya na mafisi waeamua kuingamiza kwa kila namna huku wakisaidiwa na vitengo vyao vya maharamia wenyewe wakiviita vyombo vya dola ikiwemo mahakama, polisi na jeshi.

Nani anajali ??
 
Na Edo Kumwembe

Ni nchi ya ajabu kwa mwanadamu makini kuweza kuishi. Ni nchi inayoshangaza sana, ingawa raia wake hawaonyeshi kushangazwa na matukio kadhaa yanayotokea.

Naizungumzia Tanzania nchi niliyoishi kwa miongo kadhaa tangu nizaliwe. Baada ya nyimbo nyingi za matatizo, dhiki, wizi, rushwa, tabu, magonjwa na kila aina ya shida ambayo mwanadamu wa kawaida anapitia, jawabu kubwa linapatika kwa swali; nani anajali?Ndio, nani anajali? Hili ni swali ambalo kila Mtanzania anapaswa kuulizwa.

Ni kwa kiasi gani, mwananchi wa kawaida, kiongozi au muhusika yeyote wa nchi hii anajali matatizo ya nchi yetu.Nimejaribu kwa kiasi kikubwa kutazama sura za viongozi wetu, mawaziri, wabunge, Wakurugenzi, Mameneja na kila kiongozi. Sioni anayejali.Wengi wanaongea wasichofikiria kukifanya kwa dhati na nchi imezidi kuoza.

Akili zao ziko katika wizi kwa sababu na wananchi wenyewe wala viongozi wengine hawajali.Nchi inatafunwa kila jua linapochomoza na kuzama. Hakuna anayejali na kila mtu anaangalia maisha yake. Msukuma mkokoteni haoni ni kwa namna gani anahusika na Waziri mwizi wala Mkurugenzi wa Manispaa mla rushwa.

Atajihusisha vipi? Kwa nini atumie muda wake mwingi kujali? Kama watu wanaomzunguka hawajali kula yake kwa nini na yeye awe anajali maisha ya wengine.Siwezi kusema nilifaidi matunda ya utawala wa Mwalimu Nyerere. Sijui mengi yaliyotokea wakati wa Utawala wake, lakini tangu nilipopata akili timamu sijawahi kusikia Rais wa nchi yangu akimfukuza kazi Waziri wake kwa rushwa wala wizi.

Je ni kweli kwamba marais wangu hawawaoni Mawaziri wezi na wala rushwa? Kama wangekuwa watiifu na waadilifu basi nchi yetu ingekuwa mbali. Lakini naamini wanawaona, kikubwa ni kwa vile hawajali kinachotokea. Hawajali kwa sababu hawana sababu ya kujali. Kwa kuwa wananchi hawajali basi na wao hawajali kama ambavyo wananchi hawajali.

Wanaendelea kutojali na daima tunaendelea kupata vizazi vya Watanzania wasiojali.Kwani tukifungua mikataba ya ajabu ya Madini hatuwaoni walioweka saini hizo? Tunawaona, lakini nani anajali? Nchi inasonga mbele na maisha yanaendelea. Huyu anajaribu kuandika gazetini kwa uchungu na yule anatamka lile katika kipindi cha redio kwa uchungu, lakini nani anajali?

Kina mama na watoto wanafungulia michezo ya maigizo ITV na kwingineko. Nani atawalaumu wakati watu makini wenyewe hawajali? Si afadhali nao wasijali!Kwani yuko wapi yule Waziri aliyesema yuko tayari kuona wananchi wanakula majani ili ndege ya Rais inunuliwe? Ndege ambayo ni mbovu!. Si amechaguliwa tena kuwa Waziri? Nani anajali kama Rais wa sasa hakujali? Mimi nitajali nini?

Ni mwananchi gani anajali? Walio wengi wanafanya maaandamano katika mikasa ya kidini au ile ya kumpongeza Rais aliyefutiwa madeni ambayo fedha zake zilitumiwa kununua mashangingi.Kuna anayejali kwenda katika maandamano ya kupinga kupanda kwa bei ya umeme? Kuna anayejali kuandamana baada ya kusikia Nesi amesababisha kichanga kufa sekunde chache baada ya mama mjamzito kujifungua?

Hakuna anayejali kwa sababu hata akiandamana kwa uchungu mkubwa, Rais hawezi kumwajibisha Waziri wa Afya!. Ndivyo nchi ilivyo na watu wengi wamekwenda jela baada ya kutoa taarifa njema kwa jeshi la Polisi. Lakini nani anajali kuwepo kwao jela?

Ukitoa taarifa kuhusiana na mkubwa fulani anayepokea rushwa, kesho yake Kamanda wa Polisi wa Mkoa anakuonya na kukwambia uachane naye.Kwa nini niendelee kujali kwa watu ambao hawajali? Watu wangapi walishikwa na madawa ya kulevya katika Uwanja wa ndege wa kimataifa wa Dar es salaam lakini wapo nje kwa madai kwamba uchunguzi unaendelea?

Uchunguzi upi wakati madawa yalitolewa tumboni na tukaonyeshwa katika taarifa za habari za Televisheni mbalimbali? Kwa nini niendelee kujali kuwepo nje kwa mtuhumiwa wakati Kamanda wa Polisi wa mkoa haonyeshi kujali?Yuko wapi dada machachari Mbunge wa kike aliyedai kwamba ana majina ya wauza madawa wa kulevya?

Ni kweli kwamba alizungumza jambo jipya katika jamii yetu ya watu wasiojali? Tunao watu wengi wanaouza madawa na kwa bahati wanajulikana, lakini nani anajali? Dada yule ‘alionyesha’ kujali, lakini baada ya hapo nani amejali? Mbona hatujasikia mtu amekwenda ndani kutokana na mdomo wake?

Tangu baada ya ‘mauaji’ ya basi ya Buffalo, magari yanazidi kwenda kasi barabarani. Nani anajali? Si mpaka watu wengine wafe ndio tusikie tamko jingine la kinafiki?Kuna meli ngapi mbovu pale Ziwa Victoria na sehemu nyingine zenye vyombo vya usafiri wa majini? Kwa sababu hakuna anayekufa kwa sasa wahusika na wananchi hawajali mpaka litokee janga.

Ili mradi asubuhi inafika, mchana unapita na jioni inawadia basi hakuna anayejali mpaka litokee janga. Nani anajali?Mchele mbovu unahalalishwa, watu wanatengeza maji ya ‘kufoji’ na kuuza, nani anajali? Nikienda kusema Polisi wananitazama kwa jicho la chuki lakini tayari nimeshawaachia mianya ya rushwa. Keshokutwa nakutana na mkubwa wa Polisi niliyemshtua akiwa pamoja na mkuu wa Kiwanda nilichokishtaki.

Wanakula ‘kitimoto’ pamoja na wanacheka vilivyo, nani anajali?Kuna watu wachache walikiweka mikononi Chama cha soka nchini FAT,enzi hizo. Nani alijali? Kama si kuvurugana wenyewe kwa wenyewe wangeweza kuwepo mpaka leo.Ndio, Rais wa nchi alikuwepo, lakini hakuwa na muda wa kujali. Kipaza sauti kilikuwa kinamwambia asijali mambo hayo ila aelekeze macho katika Utandawazi.

Ndio, utandawazi ambao unaruhusu tupeleke makontena ya mchanga uliochanganyika na dhahabu nje ya mipaka yetu. Nani anajali?Wachache wanajaribu kujali lakini nani anawasikia? Wenyewe wanakutana Golden Tulip wakila firigisi na kupeana ruhusa hizo. Mimi na wewe tujali nini wakati hatuna uhakika wa kesho? Tukipata watoto nao wanaingia katika mkumbo huo huo wa kutojali.

Kizazi hiki ambacho watoto wengi wamegeukia hisia za kimagharibi ni yupi kati yao anaweza kujali?Wa kiume anakazania kusuka, wa kike anatamani kuvaa kama Beyonce. Hakuna hata mmoja mwenye hisia na nchi. Hawezi kujali kwa sababu hajafundishwa kujali. Ukisikiliza maoni ya wengi kuhusiana na kesi ya Justine Kasusura, wengi wanamlaumu kwa nini hakutoweka nje ya nchi.

Hakuna anayesikitika kwa kitendo chake cha kuiba fedha. Kwa nini?Watu hawajali alichokifanya. Yeye alifanya hadharani lakini kuna wanaoiba kwa karatasi? Hawa akina ‘Kasusura’ wa mezani nani anawazuia? Nani anawajali?Iko wapi Kampuni ya Richmond? Mbona kimya? Nani anajali? Kwa sasa umeme upo na watu hawajali tena. Wanataka ije ‘Richmond’ nyingine ya Maji au huduma za Afya.

Nani anajali? Ndio, sijawahi na wala sitaki kupiga kura. Yupo atakayesema napoteza haki yangu ya msingi. Simuoni wa kunijali na hata kama akiamua kunijali basi mfumo hauwezi kumsapoti anijali.Wakati wananchi wengine wakipiga kura mimi naangalia vipindi vya soka katika Televisheni, kwa nini uniambie sijali wakati atakayechaguliwa hatanijali?

Katika kituo cha wapiga kura chenye wakazi 1000 lakini mshindi ameshinda kwa kura 1200, kwa nini nijali kusumbuka juani huku FFU wakinighasi wakati waliopanga matokeo hawaijali kura yangu?Nijali nini hasa kwa kutompigia kura mtu atakayekwenda bungeni kupitisha sheria ya Takrima? Acha nifuatilie Ligi kuu ya England na utamu wake.

Soma magazeti yetu ya leo. Watu wameamua kuandika mambo laini ambayo si sehemu ya mapambano yetu. Makala za leo ni zile zile zinazoelezea kwa undani Habari za Theolojia, Ulokole, na mambo mengine. Mwananchi asiye na uhakika na machweo ataelewa nini na kupata tumaini jema katika makala hizi? Wanaoziandika hawajali kinachotokea kwa sasa.

Kwetu, kiongozi kutajwa anamiliki hiki na kile kwa jina la mwanae, si kashfa. Kwetu, mtoto wa mkubwa au mkubwa mwenyewe kuua si jambo la ajabu sana. Nani anajali? Wao na Kamanda wa Polisi wanakutana Kilimanjaro Kempsky katika dhifa mbalimbali, unajua wanaongea nini? Kwa nini ujitie kimbelembele cha kujali? Ili mradi unapumua, iangalie siku yako ya kesho.

Tanzania ya leo imejaa watu wanaozijali familia zao. Nani atawalaumu watu hawa? Kwani viongozi wetu wanawajali kina nani? Si wanajali elimu za watoto wao pale Oxford, Havard na kwingineko?Kama unabisha, mbona sasa hivi ndio wanatuongoza? Nani anajali? Tuna uhakika gani kama baadaye wajukuu hawataongoza? Si ndio wanapewa ukamanda wa vijana wakijiandaa kumtawala mwanangu ambaye ni mnyonge wa baadaye?

Nani anajali?Sina hasira na mtu. Nina furaha na maisha yangu kwa sababu napata ninachokitaka kwa uhalali. Kama maisha yataendelea kuwa hivi basi nisilaumiwe kwa kutojali. Nina uhakika gani kama wenzangu wanajali?Kilio kama changu kimetamkwa mara ngapi na watu makini? Nani amejali? Kelele za mchanga wa dhahabu nani amezijali? Waliongia mikabata mibovu ya madini nani anawajali? Wangekuwa Chini, Japan, Uingereza na kwingineko, wangekuwa wapi watu hawa kama si katika kuta za Gereza?

Hapa kwetu nani anajali?Lakini nijali nini zaidi wakati Rais wa nchi aliwahi kuwatamkia watu walioelezea hisia zao kwa Waziri Mkuu wake kuhusu umilione wake wa mashaka, kwamba wana wivu? Kama yeye mtu wa juu kabisa hakujali, nani atajali? Utawala ule ulikumbana na migomo ya wanafunzi, huu nao unakumbana na migomo hiyo hiyo, nani anajali? Kuna njia za kudumu za kumaliza migomo hiyo ambayo nimeisikia tangu utotoni mwangu?

Huyu anakabiliana nayo leo, akihamishiwa anahama na hisia zake.

Yule anakuja na hisia nyingine na wala hajali kutazama alipoishia mwenzake. Leo, kuna watu wengi wanapiga kelele kuhusiana na hatari ya kujiunga na Jumuiya ya Afrika Mashariki. Nani anawasikiliza? Mimi naweza kuwa sehemu ya maamuzi hayo?Wanaotoa tahadhari ni watu wasomi. Afadhali ingekuwa kwangu mtu nisiye na elimu, lakini wanaotoa tahadhari hizi ni watu wanaoheshimika kwa elimu na upeo wao.

Najua hawasikilizwi lakini nani anajali? Kama wenzao hawajali, nani atanisikiliza mimi nisiye na lolote? Acha waamue nami nitatii kwani waliamua mangapi ya hatari na nimeendelea kutii? SijaliLakini kwa nini nimewang’angania wasiojali wakati hata wenyewe wakifa au kuondoka madarakani hakuna anayewajali? Wako wapi waliojali ambao familia zao zinaishi kama vile baba zao hawakujali? Ndio, familia za akina Edward Sokoine.

Nina uhakika watoto wao watajuta kwa kitendo cha baba yao kujali sana wakati wa utawala wake.Ndio, na hata ninapomaliza kuandika makala hii, wengi wataelewa ninachomaanisha. Wakubwa wengi na watu wa kawaida wataisoma na kuielewa.

Lakini nani atajali?

Muda utaamua!
 
Kaka Edo nimekuelewa sana, ukiisoma lazma ujawe na simanz, labda akina naniliu........................: wale wanapatikan jengo la kijana lumumba.
I appreciate u Edo
 
Kwa kinachoendelea nchini namuona zitto bonge la mjanja,watanzania tumelala tunaamshwa ila inaonekana hatuamki leo wala kesho kwa nini asichukue chake mapema.Wapinzani wamefanya kazi kubwa sana kilichobaki ni sisi kufanya maamuzi.
 
kuna kitu kibaya sana kinainyemelea nchi yetu lakini cha kusikitisha si kikwete si pinda wala usalama wa taifa wanakiona, watu wamechoka kuvumilia madudu yanayoendelea uoga polepole unatoweka ni km wanasubiria kengele walianzishe coz tension inaongezeka kila siku miongoni mwa wananchi
 
Nani anajali wakati polisi wenyewe wanawaogopa CCM kama vile ndio waliowaajiri? Nani anajali kuhusu katiba mpya kuchezewa?Nani anajali kama Chadema wanaandamana kwa haki?Nani anajali kama kuandamana ni haki ya msingi?Nani anajali kama wakuliama wetu wananyonywa sana na serikali inayosema ni sikivu?Wacha wee wenye meno wataendelea kutafuna sana nchi hii.
 
nimesoma najikuta napata uchungu wa hali y juu n nchi yangu
 
Back
Top Bottom