Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
nimesoma najikuta napata uchungu wa hali y juu n nchi yangu
nimesoma najikuta napata uchungu wa hali y juu n nchi yangu
sizani edo kumwembe ana akili amesahau alivyokuwa akioga mchana kweupe kwenye kisima cha kuchotea maji bila kujali alikuwa akiwaathiri kisaikolojia wanafunzi ambao madarasa yao yalikuwa karibu na hostel hiyo ya jitegemee,amesahau alivyokuwa akiwalaghai form 1 na akifanya nao mapenzi darasani usiku,amesahau alivyo kuwa akisaidiwa nadhani atanielewa,mtu wa namna hii hawezi kuirubuni fikra nzima ya tanzania kwa misemo ya kitoto ,poor eddo kumwembeNa edo kumwembe
Ni nchi ya ajabu kwa mwanadamu
makini kuweza kuishi. Ni nchi
inayoshangaza sana, ingawa raia wake
hawaonyeshi kushangazwa na matukio
kadhaa yanayotokea.
Naizungumzia Tanzania nchi
niliyoishi kwa miongo kadhaa tangu
nizaliwe. Baada ya nyimbo nyingi za
matatizo, dhiki, wizi, rushwa, tabu,
magonjwa na kila aina ya shida
ambayo mwanadamu wa kawaida
anapitia, jawabu kubwa linapatika
kwa swali; nani anajali?Ndio, nani
anajali? Hili ni swali ambalo kila
Mtanzania anapaswa kuulizwa.
Ni kwa kiasi gani, mwananchi wa
kawaida, kiongozi au muhusika yeyote
wa nchi hii anajali matatizo ya nchi
yetu.Nimejaribu kwa kiasi kikubwa
kutazama sura za viongozi wetu,
mawaziri, wabunge, Wakurugenzi,
Mameneja na kila kiongozi. Sioni
anayejali.Wengi wanaongea
wasichofikiria kukifanya kwa dhati
na nchi imezidi kuoza. Akili zao
ziko katika wizi kwa sababu na
wananchi wenyewe wala viongozi
wengine hawajali.Nchi inatafunwa
kila jua linapochomoza na kuzama.
Hakuna anayejali na kila mtu
anaangalia maisha yake.
Msukuma mkokoteni haoni ni kwa namna
gani anahusika na Waziri mwizi wala
Mkurugenzi wa Manispaa mla
rushwa.Atajihusisha vipi? Kwa nini
atumie muda wake mwingi kujali? Kama
watu wanaomzunguka hawajali kula
yake kwa nini na yeye awe anajali
maisha ya wengine.Siwezi kusema
nilifaidi matunda ya utawala wa
Mwalimu Nyerere. Sijui mengi
yaliyotokea wakati wa Utawala wake,
lakini tangu nilipopata akili timamu
sijawahi kusikia Rais wa nchi yangu
akimfukuza kazi Waziri wake kwa
rushwa wala wizi.
Je ni kweli kwamba marais wangu
hawawaoni Mawaziri wezi na wala
rushwa? Kama wangekuwa watiifu na
waadilifu basi nchi yetu ingekuwa
mbali. Lakini naamini wanawaona,
kikubwa ni kwa vile hawajali
kinachotokea.
Hawajali kwa sababu hawana sababu ya
kujali. Kwa kuwa wananchi hawajali
basi na wao hawajali kama ambavyo
wananchi hawajali. Wanaendelea
kutojali na daima tunaendelea kupata
vizazi vya Watanzania
wasiojali.Kwani tukifungua mikataba
ya ajabu ya Madini hatuwaoni
walioweka saini hizo? Tunawaona,
lakini nani anajali? Nchi inasonga
mbele na maisha yanaendelea.
Huyu anajaribu kuandika gazetini kwa
uchungu na yule anatamka lile katika
kipindi cha redio kwa uchungu,
lakini nani anajali? Kina mama na
watoto wanafungulia michezo ya
maigizo ITV na kwingineko. Nani
atawalaumu wakati watu makini
wenyewe hawajali? Si afadhali nao
wasijali!Kwani yuko wapi yule Waziri
aliyesema yuko tayari kuona wananchi
wanakula majani ili ndege ya Rais
inunuliwe? Ndege ambayo ni mbovu!.
Si amechaguliwa tena kuwa Waziri?
Nani anajali kama Rais wa sasa
hakujali? Mimi nitajali nini?
Ni mwananchi gani anajali? Walio
wengi wanafanya maaandamano katika
mikasa ya kidini au ile ya
kumpongeza Rais aliyefutiwa madeni
ambayo fedha zake zilitumiwa kununua
mashangingi.Kuna anayejali kwenda
katika maandamano ya kupinga kupanda
kwa bei ya umeme? Kuna anayejali
kuandamana baada ya kusikia Nesi
amesababisha kichanga kufa sekunde
chache baada ya mama mjamzito
kujifungua?
Hakuna anayejali kwa sababu hata
akiandamana kwa uchungu mkubwa, Rais
hawezi kumwajibisha Waziri wa Afya!.
Ndivyo nchi ilivyo na watu wengi
wamekwenda jela baada ya kutoa
taarifa njema kwa jeshi la Polisi.
Lakini nani anajali kuwepo kwao
jela? Ukitoa taarifa kuhusiana na
mkubwa fulani anayepokea rushwa,
kesho yake Kamanda wa Polisi wa Mkoa
anakuonya na kukwambia uachane
naye.Kwa nini niendelee kujali kwa
watu ambao hawajali? Watu wangapi
walishikwa na madawa ya kulevya
katika Uwanja wa ndege wa kimataifa
wa Dar es salaam lakini wapo nje kwa
madai kwamba uchunguzi unaendelea?
Uchunguzi upi wakati madawa
yalitolewa tumboni na tukaonyeshwa
katika taarifa za habari za
Televisheni mbalimbali? Kwa nini
niendelee kujali kuwepo nje kwa
mtuhumiwa wakati Kamanda wa Polisi
wa mkoa haonyeshi kujali?Yuko wapi
dada machachari Mbunge wa kike
aliyedai kwamba ana majina ya wauza
madawa wa kulevya? Ni kweli kwamba
alizungumza jambo jipya katika jamii
yetu ya watu wasiojali?
Tunao watu wengi wanaouza madawa na
kwa bahati wanajulikana, lakini nani
anajali? Dada yule alionyesha
kujali, lakini baada ya hapo nani
amejali? Mbona hatujasikia mtu
amekwenda ndani kutokana na mdomo
wake?Tangu baada ya mauaji ya basi
ya Buffalo, magari yanazidi kwenda
kasi barabarani. Nani anajali? Si
mpaka watu wengine wafe ndio tusikie
tamko jingine la kinafiki?Kuna meli
ngapi mbovu pale Ziwa Victoria na
sehemu nyingine zenye vyombo vya
usafiri wa majini? Kwa sababu hakuna
anayekufa kwa sasa wahusika na
wananchi hawajali mpaka litokee
janga.
Ili mradi asubuhi inafika, mchana
unapita na jioni inawadia basi
hakuna anayejali mpaka litokee
janga. Nani anajali?Mchele mbovu
unahalalishwa, watu wanatengeza maji
ya kufoji na kuuza, nani anajali?
Nikienda kusema Polisi wananitazama
kwa jicho la chuki lakini tayari
nimeshawaachia mianya ya rushwa.
Keshokutwa nakutana na mkubwa wa
Polisi niliyemshtua akiwa pamoja na
mkuu wa Kiwanda nilichokishtaki.
Wanakula kitimoto pamoja na
wanacheka vilivyo, nani anajali?Kuna
watu wachache walikiweka mikononi
Chama cha soka nchini FAT,enzi hizo.
Nani alijali? Kama si kuvurugana
wenyewe kwa wenyewe wangeweza kuwepo
mpaka leo.Ndio, Rais wa nchi
alikuwepo, lakini hakuwa na muda wa
kujali. Kipaza sauti kilikuwa
kinamwambia asijali mambo hayo ila
aelekeze macho katika Utandawazi.
Ndio, utandawazi ambao unaruhusu
tupeleke makontena ya mchanga
uliochanganyika na dhahabu nje ya
mipaka yetu. Nani anajali?Wachache
wanajaribu kujali lakini nani
anawasikia? Wenyewe wanakutana
Golden Tulip wakila firigisi na
kupeana ruhusa hizo. Mimi na wewe
tujali nini wakati hatuna uhakika wa
kesho?
Tukipata watoto nao wanaingia katika
mkumbo huo huo wa kutojali. Kizazi
hiki ambacho watoto wengi wamegeukia
hisia za kimagharibi ni yupi kati
yao anaweza kujali?Wa kiume
anakazania kusuka, wa kike anatamani
kuvaa kama Beyonce. Hakuna hata
mmoja mwenye hisia na nchi. Hawezi
kujali kwa sababu hajafundishwa
kujali.
Ukisikiliza maoni ya wengi kuhusiana
na kesi ya Justine Kasusura, wengi
wanamlaumu kwa nini hakutoweka nje
ya nchi. Hakuna anayesikitika kwa
kitendo chake cha kuiba fedha. Kwa
nini?Watu hawajali alichokifanya.
Yeye alifanya hadharani lakini kuna
wanaoiba kwa karatasi? Hawa akina
Kasusura wa mezani nani anawazuia?
Nani anawajali?Iko wapi Kampuni ya
Richmond? Mbona kimya? Nani anajali?
Kwa sasa umeme upo na watu hawajali
tena. Wanataka ije Richmond
nyingine ya Maji au huduma za Afya.
Nani anajali?
Ndio, sijawahi na wala sitaki kupiga
kura. Yupo atakayesema napoteza haki
yangu ya msingi. Simuoni wa kunijali
na hata kama akiamua kunijali basi
mfumo hauwezi kumsapoti
anijali.Wakati wananchi wengine
wakipiga kura mimi naangalia vipindi
vya soka katika Televisheni, kwa
nini uniambie sijali wakati
atakayechaguliwa hatanijali?
Katika kituo cha wapiga kura chenye
wakazi 1000 lakini mshindi ameshinda
kwa kura 1200, kwa nini nijali
kusumbuka juani huku FFU wakinighasi
wakati waliopanga matokeo hawaijali
kura yangu?Nijali nini hasa kwa
kutompigia kura mtu atakayekwenda
bungeni kupitisha sheria ya Takrima?
Acha nifuatilie Ligi kuu ya England
na utamu wake.
Soma magazeti yetu ya leo. Watu
wameamua kuandika mambo laini ambayo
si sehemu ya mapambano yetu.Makala
za leo ni zile zile zinazoelezea kwa
undani Habari za Theolojia, Ulokole,
na mambo mengine. Mwananchi asiye na
uhakika na machweo ataelewa nini na
kupata tumaini jema katika makala
hizi? Wanaoziandika hawajali
kinachotokea kwa sasa.
Kwetu, kiongozi kutajwa anamiliki
hiki na kile kwa jina la mwanae, si
kashfa. Kwetu, mtoto wa mkubwa au
mkubwa mwenyewe kuua si jambo la
ajabu sana. Nani anajali? Wao na
Kamanda wa Polisi wanakutana
Kilimanjaro Kempsky katika dhifa
mbalimbali, unajua wanaongea nini?
Kwa nini ujitie kimbelembele cha
kujali? Ili mradi unapumua, iangalie
siku yako ya kesho.Tanzania ya leo
imejaa watu wanaozijali familia zao.
Nani atawalaumu watu hawa? Kwani
viongozi wetu wanawajali kina nani?
Si wanajali elimu za watoto wao pale
Oxford, Havard na kwingineko?Kama
unabisha, mbona sasa hivi ndio
wanatuongoza? Nani anajali? Tuna
uhakika gani kama baadaye wajukuu
hawataongoza? Si ndio wanapewa
ukamanda wa vijana wakijiandaa
kumtawala mwanangu ambaye ni mnyonge
wa baadaye? Nani anajali?Sina hasira
na mtu.
Nina furaha na maisha yangu kwa
sababu napata ninachokitaka kwa
uhalali. Kama maisha yataendelea
kuwa hivi basi nisilaumiwe kwa
kutojali. Nina uhakika gani kama
wenzangu wanajali?Kilio kama changu
kimetamkwa mara ngapi na watu
makini? Nani amejali? Kelele za
mchanga wa dhahabu nani amezijali?
Waliongia mikabata mibovu ya madini
nani anawajali? Wangekuwa
Chini,Japan, Uingereza na
kwingineko, wangekuwa wapi watu hawa
kama si katika kuta za Gereza? Hapa
kwetu nani anajali?Lakini nijali
nini zaidi wakati Rais wa nchi
aliwahi kuwatamkia watu walioelezea
hisia zao kwa Waziri Mkuu wake
kuhusu umilione wake wa mashaka,
kwamba wana wivu? Kama yeye mtu wa
juu kabisa hakujali, nani atajali?
Utawala ule ulikumbana na migomo ya
wanafunzi, huu nao unakumbana na
migomo hiyo hiyo, nani anajali? Kuna
njia za kudumu za kumaliza migomo
hiyo ambayo nimeisikia tangu utotoni
mwangu?Huyu anakabiliana nayo leo,
akihamishiwa anahama na hisia zake.
Yule anakuja na hisia nyingine na
wala hajali kutazama alipoishia
mwenzake.
Leo, kuna watu wengi wanapiga kelele
kuhusiana na hatari ya kujiunga na
Jumuiya ya Afrika Mashariki. Nani
anawasikiliza? Mimi naweza kuwa
sehemu ya maamuzi hayo?Wanaotoa
tahadhari ni watu wasomi. Afadhali
ingekuwa kwangu mtu nisiye na elimu,
lakini wanaotoa tahadhari hizi ni
watu wanaoheshimika kwa elimu na
upeo wao.
Najua hawasikilizwi lakini nani
anajali? Kama wenzao hawajali, nani
atanisikiliza mimi nisiye na lolote?
Acha waamue nami nitatii kwani
waliamua mangapi ya hatari na
nimeendelea kutii? SijaliLakini kwa
nini nimewangangania wasiojali
wakati hata wenyewe wakifa au
kuondoka madarakani hakuna
anayewajali?
Wako wapi waliojali ambao familia
zao zinaishi kama vile baba zao
hawakujali? Ndio, familia za akina
Edward Sokoine. Nina uhakika watoto
wao watajuta kwa kitendo cha baba
yao kujali sana wakati wa utawala
wake.Ndio, na hata ninapomaliza
kuandika makala hii, wengi wataelewa
ninachomaanisha. Wakubwa wengi na
watu wa kawaida wataisoma na
kuielewa. Lakini nani atajali?
CHANZO:edo kumwembe
Malalamiko tu kila kona njoo na solution tukusome kama keli wew ni mzalendo.
sizani edo kumwembe ana akili amesahau alivyokuwa akioga mchana kweupe kwenye kisima cha kuchotea maji bila kujali alikuwa akiwaathiri kisaikolojia wanafunzi ambao madarasa yao yalikuwa karibu na hostel hiyo ya jitegemee,amesahau alivyokuwa akiwalaghai form 1 na akifanya nao mapenzi darasani usiku,amesahau alivyo kuwa akisaidiwa nadhani atanielewa,mtu wa namna hii hawezi kuirubuni fikra nzima ya tanzania kwa misemo ya kitoto ,poor eddo kumwembe
Good thinking.
Mwanzishq mada tafadhali tambulisha chanzo. Huyu ni eddo kumwembe
umelalamika sana..nini chakufanya? ilibidi mwisho wa makala yako angalau utoe nini watu wafanye???