Nani anajali hatima ya Tanzania?

Nani anajali hatima ya Tanzania?

Sasa naona kwa mbaaali tunaanza kustuka mwakani kampeni zinaaanza tisijisahau tena.
 
"Siku moja akatokea kiongozi wa
Taifa letu, akatuambia huko nje
kuna hela nyingi kuliko hapa
nyumbani, mwambieni wewe ni
mpumbavu" Mwalimu J.K.
Nyerere.
"Kama kuna mtu ambaye
anaamini nchi hii inaweza
kuendelea kwa kusaidiwa,
anajidanganya, Narudiia tena,
Katika nchi hii kama kuna kiongozi
anaamini nchi inaweza kuendelea
kwa kupewa misaada,
anajidanganya" Benjamin Mkapa.
"Unapoenda kuomba siyo
kwamba wewe unapenda tu
kuomba. Huko nje kuna mataifa
yenye hela nyingi tu,
unachotakiwa ni kujieleza,
wakikuelewa, watakupa" Jakaya
Kikwete.
 
Edo makala nzuri inasisimua ubongo. A thousand mile journey starts with a foot step! Kutambua kuwa kama nchi tuna matatizo makubwa ya kiuchumi na kijamii ni hatua awali muhimu. Hakuna mabadiliko mepesi duniani kote. Hata kwenda mbinguni Kwanza sharti ufe. Hata hivyo hakuna kitu au hali yoyote ile iliyo na mwanzo isio na mwisho hata kama binadamu hatafanya chochote. Mabadiliko yatatokea tuu wise people say all empires wither with time! So will ccm.
 
Last edited by a moderator:
Na edo kumwembe
Ni nchi ya ajabu kwa mwanadamu
makini kuweza kuishi. Ni nchi
inayoshangaza sana, ingawa raia wake
hawaonyeshi kushangazwa na matukio
kadhaa yanayotokea.
Naizungumzia Tanzania nchi
niliyoishi kwa miongo kadhaa tangu
nizaliwe. Baada ya nyimbo nyingi za
matatizo, dhiki, wizi, rushwa, tabu,
magonjwa na kila aina ya shida
ambayo mwanadamu wa kawaida
anapitia, jawabu kubwa linapatika
kwa swali; nani anajali?Ndio, nani
anajali? Hili ni swali ambalo kila
Mtanzania anapaswa kuulizwa.
Ni kwa kiasi gani, mwananchi wa
kawaida, kiongozi au muhusika yeyote
wa nchi hii anajali matatizo ya nchi
yetu.Nimejaribu kwa kiasi kikubwa
kutazama sura za viongozi wetu,
mawaziri, wabunge, Wakurugenzi,
Mameneja na kila kiongozi. Sioni
anayejali.Wengi wanaongea
wasichofikiria kukifanya kwa dhati
na nchi imezidi kuoza. Akili zao
ziko katika wizi kwa sababu na
wananchi wenyewe wala viongozi
wengine hawajali.Nchi inatafunwa
kila jua linapochomoza na kuzama.
Hakuna anayejali na kila mtu
anaangalia maisha yake.
Msukuma mkokoteni haoni ni kwa namna
gani anahusika na Waziri mwizi wala
Mkurugenzi wa Manispaa mla
rushwa.Atajihusisha vipi? Kwa nini
atumie muda wake mwingi kujali? Kama
watu wanaomzunguka hawajali kula
yake kwa nini na yeye awe anajali
maisha ya wengine.Siwezi kusema
nilifaidi matunda ya utawala wa
Mwalimu Nyerere. Sijui mengi
yaliyotokea wakati wa Utawala wake,
lakini tangu nilipopata akili timamu
sijawahi kusikia Rais wa nchi yangu
akimfukuza kazi Waziri wake kwa
rushwa wala wizi.
Je ni kweli kwamba marais wangu
hawawaoni Mawaziri wezi na wala
rushwa? Kama wangekuwa watiifu na
waadilifu basi nchi yetu ingekuwa
mbali. Lakini naamini wanawaona,
kikubwa ni kwa vile hawajali
kinachotokea.
Hawajali kwa sababu hawana sababu ya
kujali. Kwa kuwa wananchi hawajali
basi na wao hawajali kama ambavyo
wananchi hawajali. Wanaendelea
kutojali na daima tunaendelea kupata
vizazi vya Watanzania
wasiojali.Kwani tukifungua mikataba
ya ajabu ya Madini hatuwaoni
walioweka saini hizo? Tunawaona,
lakini nani anajali? Nchi inasonga
mbele na maisha yanaendelea.
Huyu anajaribu kuandika gazetini kwa
uchungu na yule anatamka lile katika
kipindi cha redio kwa uchungu,
lakini nani anajali? Kina mama na
watoto wanafungulia michezo ya
maigizo ITV na kwingineko. Nani
atawalaumu wakati watu makini
wenyewe hawajali? Si afadhali nao
wasijali!Kwani yuko wapi yule Waziri
aliyesema yuko tayari kuona wananchi
wanakula majani ili ndege ya Rais
inunuliwe? Ndege ambayo ni mbovu!.
Si amechaguliwa tena kuwa Waziri?
Nani anajali kama Rais wa sasa
hakujali? Mimi nitajali nini?
Ni mwananchi gani anajali? Walio
wengi wanafanya maaandamano katika
mikasa ya kidini au ile ya
kumpongeza Rais aliyefutiwa madeni
ambayo fedha zake zilitumiwa kununua
mashangingi.Kuna anayejali kwenda
katika maandamano ya kupinga kupanda
kwa bei ya umeme? Kuna anayejali
kuandamana baada ya kusikia Nesi
amesababisha kichanga kufa sekunde
chache baada ya mama mjamzito
kujifungua?
Hakuna anayejali kwa sababu hata
akiandamana kwa uchungu mkubwa, Rais
hawezi kumwajibisha Waziri wa Afya!.
Ndivyo nchi ilivyo na watu wengi
wamekwenda jela baada ya kutoa
taarifa njema kwa jeshi la Polisi.
Lakini nani anajali kuwepo kwao
jela? Ukitoa taarifa kuhusiana na
mkubwa fulani anayepokea rushwa,
kesho yake Kamanda wa Polisi wa Mkoa
anakuonya na kukwambia uachane
naye.Kwa nini niendelee kujali kwa
watu ambao hawajali? Watu wangapi
walishikwa na madawa ya kulevya
katika Uwanja wa ndege wa kimataifa
wa Dar es salaam lakini wapo nje kwa
madai kwamba uchunguzi unaendelea?
Uchunguzi upi wakati madawa
yalitolewa tumboni na tukaonyeshwa
katika taarifa za habari za
Televisheni mbalimbali? Kwa nini
niendelee kujali kuwepo nje kwa
mtuhumiwa wakati Kamanda wa Polisi
wa mkoa haonyeshi kujali?Yuko wapi
dada machachari Mbunge wa kike
aliyedai kwamba ana majina ya wauza
madawa wa kulevya? Ni kweli kwamba
alizungumza jambo jipya katika jamii
yetu ya watu wasiojali?
Tunao watu wengi wanaouza madawa na
kwa bahati wanajulikana, lakini nani
anajali? Dada yule ‘alionyesha’
kujali, lakini baada ya hapo nani
amejali? Mbona hatujasikia mtu
amekwenda ndani kutokana na mdomo
wake?Tangu baada ya ‘mauaji’ ya basi
ya Buffalo, magari yanazidi kwenda
kasi barabarani. Nani anajali? Si
mpaka watu wengine wafe ndio tusikie
tamko jingine la kinafiki?Kuna meli
ngapi mbovu pale Ziwa Victoria na
sehemu nyingine zenye vyombo vya
usafiri wa majini? Kwa sababu hakuna
anayekufa kwa sasa wahusika na
wananchi hawajali mpaka litokee
janga.
Ili mradi asubuhi inafika, mchana
unapita na jioni inawadia basi
hakuna anayejali mpaka litokee
janga. Nani anajali?Mchele mbovu
unahalalishwa, watu wanatengeza maji
ya ‘kufoji’ na kuuza, nani anajali?
Nikienda kusema Polisi wananitazama
kwa jicho la chuki lakini tayari
nimeshawaachia mianya ya rushwa.
Keshokutwa nakutana na mkubwa wa
Polisi niliyemshtua akiwa pamoja na
mkuu wa Kiwanda nilichokishtaki.
Wanakula ‘kitimoto’ pamoja na
wanacheka vilivyo, nani anajali?Kuna
watu wachache walikiweka mikononi
Chama cha soka nchini FAT,enzi hizo.
Nani alijali? Kama si kuvurugana
wenyewe kwa wenyewe wangeweza kuwepo
mpaka leo.Ndio, Rais wa nchi
alikuwepo, lakini hakuwa na muda wa
kujali. Kipaza sauti kilikuwa
kinamwambia asijali mambo hayo ila
aelekeze macho katika Utandawazi.
Ndio, utandawazi ambao unaruhusu
tupeleke makontena ya mchanga
uliochanganyika na dhahabu nje ya
mipaka yetu. Nani anajali?Wachache
wanajaribu kujali lakini nani
anawasikia? Wenyewe wanakutana
Golden Tulip wakila firigisi na
kupeana ruhusa hizo. Mimi na wewe
tujali nini wakati hatuna uhakika wa
kesho?
Tukipata watoto nao wanaingia katika
mkumbo huo huo wa kutojali. Kizazi
hiki ambacho watoto wengi wamegeukia
hisia za kimagharibi ni yupi kati
yao anaweza kujali?Wa kiume
anakazania kusuka, wa kike anatamani
kuvaa kama Beyonce. Hakuna hata
mmoja mwenye hisia na nchi. Hawezi
kujali kwa sababu hajafundishwa
kujali.
Ukisikiliza maoni ya wengi kuhusiana
na kesi ya Justine Kasusura, wengi
wanamlaumu kwa nini hakutoweka nje
ya nchi. Hakuna anayesikitika kwa
kitendo chake cha kuiba fedha. Kwa
nini?Watu hawajali alichokifanya.
Yeye alifanya hadharani lakini kuna
wanaoiba kwa karatasi? Hawa akina
‘Kasusura’ wa mezani nani anawazuia?
Nani anawajali?Iko wapi Kampuni ya
Richmond? Mbona kimya? Nani anajali?
Kwa sasa umeme upo na watu hawajali
tena. Wanataka ije ‘Richmond’
nyingine ya Maji au huduma za Afya.
Nani anajali?
Ndio, sijawahi na wala sitaki kupiga
kura. Yupo atakayesema napoteza haki
yangu ya msingi. Simuoni wa kunijali
na hata kama akiamua kunijali basi
mfumo hauwezi kumsapoti
anijali.Wakati wananchi wengine
wakipiga kura mimi naangalia vipindi
vya soka katika Televisheni, kwa
nini uniambie sijali wakati
atakayechaguliwa hatanijali?
Katika kituo cha wapiga kura chenye
wakazi 1000 lakini mshindi ameshinda
kwa kura 1200, kwa nini nijali
kusumbuka juani huku FFU wakinighasi
wakati waliopanga matokeo hawaijali
kura yangu?Nijali nini hasa kwa
kutompigia kura mtu atakayekwenda
bungeni kupitisha sheria ya Takrima?
Acha nifuatilie Ligi kuu ya England
na utamu wake.
Soma magazeti yetu ya leo. Watu
wameamua kuandika mambo laini ambayo
si sehemu ya mapambano yetu.Makala
za leo ni zile zile zinazoelezea kwa
undani Habari za Theolojia, Ulokole,
na mambo mengine. Mwananchi asiye na
uhakika na machweo ataelewa nini na
kupata tumaini jema katika makala
hizi? Wanaoziandika hawajali
kinachotokea kwa sasa.
Kwetu, kiongozi kutajwa anamiliki
hiki na kile kwa jina la mwanae, si
kashfa. Kwetu, mtoto wa mkubwa au
mkubwa mwenyewe kuua si jambo la
ajabu sana. Nani anajali? Wao na
Kamanda wa Polisi wanakutana
Kilimanjaro Kempsky katika dhifa
mbalimbali, unajua wanaongea nini?
Kwa nini ujitie kimbelembele cha
kujali? Ili mradi unapumua, iangalie
siku yako ya kesho.Tanzania ya leo
imejaa watu wanaozijali familia zao.
Nani atawalaumu watu hawa? Kwani
viongozi wetu wanawajali kina nani?
Si wanajali elimu za watoto wao pale
Oxford, Havard na kwingineko?Kama
unabisha, mbona sasa hivi ndio
wanatuongoza? Nani anajali? Tuna
uhakika gani kama baadaye wajukuu
hawataongoza? Si ndio wanapewa
ukamanda wa vijana wakijiandaa
kumtawala mwanangu ambaye ni mnyonge
wa baadaye? Nani anajali?Sina hasira
na mtu.
Nina furaha na maisha yangu kwa
sababu napata ninachokitaka kwa
uhalali. Kama maisha yataendelea
kuwa hivi basi nisilaumiwe kwa
kutojali. Nina uhakika gani kama
wenzangu wanajali?Kilio kama changu
kimetamkwa mara ngapi na watu
makini? Nani amejali? Kelele za
mchanga wa dhahabu nani amezijali?
Waliongia mikabata mibovu ya madini
nani anawajali? Wangekuwa
Chini,Japan, Uingereza na
kwingineko, wangekuwa wapi watu hawa
kama si katika kuta za Gereza? Hapa
kwetu nani anajali?Lakini nijali
nini zaidi wakati Rais wa nchi
aliwahi kuwatamkia watu walioelezea
hisia zao kwa Waziri Mkuu wake
kuhusu umilione wake wa mashaka,
kwamba wana wivu? Kama yeye mtu wa
juu kabisa hakujali, nani atajali?
Utawala ule ulikumbana na migomo ya
wanafunzi, huu nao unakumbana na
migomo hiyo hiyo, nani anajali? Kuna
njia za kudumu za kumaliza migomo
hiyo ambayo nimeisikia tangu utotoni
mwangu?Huyu anakabiliana nayo leo,
akihamishiwa anahama na hisia zake.
Yule anakuja na hisia nyingine na
wala hajali kutazama alipoishia
mwenzake.
Leo, kuna watu wengi wanapiga kelele
kuhusiana na hatari ya kujiunga na
Jumuiya ya Afrika Mashariki. Nani
anawasikiliza? Mimi naweza kuwa
sehemu ya maamuzi hayo?Wanaotoa
tahadhari ni watu wasomi. Afadhali
ingekuwa kwangu mtu nisiye na elimu,
lakini wanaotoa tahadhari hizi ni
watu wanaoheshimika kwa elimu na
upeo wao.
Najua hawasikilizwi lakini nani
anajali? Kama wenzao hawajali, nani
atanisikiliza mimi nisiye na lolote?
Acha waamue nami nitatii kwani
waliamua mangapi ya hatari na
nimeendelea kutii? SijaliLakini kwa
nini nimewang’angania wasiojali
wakati hata wenyewe wakifa au
kuondoka madarakani hakuna
anayewajali?
Wako wapi waliojali ambao familia
zao zinaishi kama vile baba zao
hawakujali? Ndio, familia za akina
Edward Sokoine. Nina uhakika watoto
wao watajuta kwa kitendo cha baba
yao kujali sana wakati wa utawala
wake.Ndio, na hata ninapomaliza
kuandika makala hii, wengi wataelewa
ninachomaanisha. Wakubwa wengi na
watu wa kawaida wataisoma na
kuielewa. Lakini nani atajali?

CHANZO:edo kumwembe
 
Na edo kumwembe
Ni nchi ya ajabu kwa mwanadamu
makini kuweza kuishi. Ni nchi
inayoshangaza sana, ingawa raia wake
hawaonyeshi kushangazwa na matukio
kadhaa yanayotokea.
Naizungumzia Tanzania nchi
niliyoishi kwa miongo kadhaa tangu
nizaliwe. Baada ya nyimbo nyingi za
matatizo, dhiki, wizi, rushwa, tabu,
magonjwa na kila aina ya shida
ambayo mwanadamu wa kawaida
anapitia, jawabu kubwa linapatika
kwa swali; nani anajali?Ndio, nani
anajali? Hili ni swali ambalo kila
Mtanzania anapaswa kuulizwa.
Ni kwa kiasi gani, mwananchi wa
kawaida, kiongozi au muhusika yeyote
wa nchi hii anajali matatizo ya nchi
yetu.Nimejaribu kwa kiasi kikubwa
kutazama sura za viongozi wetu,
mawaziri, wabunge, Wakurugenzi,
Mameneja na kila kiongozi. Sioni
anayejali.Wengi wanaongea
wasichofikiria kukifanya kwa dhati
na nchi imezidi kuoza. Akili zao
ziko katika wizi kwa sababu na
wananchi wenyewe wala viongozi
wengine hawajali.Nchi inatafunwa
kila jua linapochomoza na kuzama.
Hakuna anayejali na kila mtu
anaangalia maisha yake.
Msukuma mkokoteni haoni ni kwa namna
gani anahusika na Waziri mwizi wala
Mkurugenzi wa Manispaa mla
rushwa.Atajihusisha vipi? Kwa nini
atumie muda wake mwingi kujali? Kama
watu wanaomzunguka hawajali kula
yake kwa nini na yeye awe anajali
maisha ya wengine.Siwezi kusema
nilifaidi matunda ya utawala wa
Mwalimu Nyerere. Sijui mengi
yaliyotokea wakati wa Utawala wake,
lakini tangu nilipopata akili timamu
sijawahi kusikia Rais wa nchi yangu
akimfukuza kazi Waziri wake kwa
rushwa wala wizi.
Je ni kweli kwamba marais wangu
hawawaoni Mawaziri wezi na wala
rushwa? Kama wangekuwa watiifu na
waadilifu basi nchi yetu ingekuwa
mbali. Lakini naamini wanawaona,
kikubwa ni kwa vile hawajali
kinachotokea.
Hawajali kwa sababu hawana sababu ya
kujali. Kwa kuwa wananchi hawajali
basi na wao hawajali kama ambavyo
wananchi hawajali. Wanaendelea
kutojali na daima tunaendelea kupata
vizazi vya Watanzania
wasiojali.Kwani tukifungua mikataba
ya ajabu ya Madini hatuwaoni
walioweka saini hizo? Tunawaona,
lakini nani anajali? Nchi inasonga
mbele na maisha yanaendelea.
Huyu anajaribu kuandika gazetini kwa
uchungu na yule anatamka lile katika
kipindi cha redio kwa uchungu,
lakini nani anajali? Kina mama na
watoto wanafungulia michezo ya
maigizo ITV na kwingineko. Nani
atawalaumu wakati watu makini
wenyewe hawajali? Si afadhali nao
wasijali!Kwani yuko wapi yule Waziri
aliyesema yuko tayari kuona wananchi
wanakula majani ili ndege ya Rais
inunuliwe? Ndege ambayo ni mbovu!.
Si amechaguliwa tena kuwa Waziri?
Nani anajali kama Rais wa sasa
hakujali? Mimi nitajali nini?
Ni mwananchi gani anajali? Walio
wengi wanafanya maaandamano katika
mikasa ya kidini au ile ya
kumpongeza Rais aliyefutiwa madeni
ambayo fedha zake zilitumiwa kununua
mashangingi.Kuna anayejali kwenda
katika maandamano ya kupinga kupanda
kwa bei ya umeme? Kuna anayejali
kuandamana baada ya kusikia Nesi
amesababisha kichanga kufa sekunde
chache baada ya mama mjamzito
kujifungua?
Hakuna anayejali kwa sababu hata
akiandamana kwa uchungu mkubwa, Rais
hawezi kumwajibisha Waziri wa Afya!.
Ndivyo nchi ilivyo na watu wengi
wamekwenda jela baada ya kutoa
taarifa njema kwa jeshi la Polisi.
Lakini nani anajali kuwepo kwao
jela? Ukitoa taarifa kuhusiana na
mkubwa fulani anayepokea rushwa,
kesho yake Kamanda wa Polisi wa Mkoa
anakuonya na kukwambia uachane
naye.Kwa nini niendelee kujali kwa
watu ambao hawajali? Watu wangapi
walishikwa na madawa ya kulevya
katika Uwanja wa ndege wa kimataifa
wa Dar es salaam lakini wapo nje kwa
madai kwamba uchunguzi unaendelea?
Uchunguzi upi wakati madawa
yalitolewa tumboni na tukaonyeshwa
katika taarifa za habari za
Televisheni mbalimbali? Kwa nini
niendelee kujali kuwepo nje kwa
mtuhumiwa wakati Kamanda wa Polisi
wa mkoa haonyeshi kujali?Yuko wapi
dada machachari Mbunge wa kike
aliyedai kwamba ana majina ya wauza
madawa wa kulevya? Ni kweli kwamba
alizungumza jambo jipya katika jamii
yetu ya watu wasiojali?
Tunao watu wengi wanaouza madawa na
kwa bahati wanajulikana, lakini nani
anajali? Dada yule ‘alionyesha’
kujali, lakini baada ya hapo nani
amejali? Mbona hatujasikia mtu
amekwenda ndani kutokana na mdomo
wake?Tangu baada ya ‘mauaji’ ya basi
ya Buffalo, magari yanazidi kwenda
kasi barabarani. Nani anajali? Si
mpaka watu wengine wafe ndio tusikie
tamko jingine la kinafiki?Kuna meli
ngapi mbovu pale Ziwa Victoria na
sehemu nyingine zenye vyombo vya
usafiri wa majini? Kwa sababu hakuna
anayekufa kwa sasa wahusika na
wananchi hawajali mpaka litokee
janga.
Ili mradi asubuhi inafika, mchana
unapita na jioni inawadia basi
hakuna anayejali mpaka litokee
janga. Nani anajali?Mchele mbovu
unahalalishwa, watu wanatengeza maji
ya ‘kufoji’ na kuuza, nani anajali?
Nikienda kusema Polisi wananitazama
kwa jicho la chuki lakini tayari
nimeshawaachia mianya ya rushwa.
Keshokutwa nakutana na mkubwa wa
Polisi niliyemshtua akiwa pamoja na
mkuu wa Kiwanda nilichokishtaki.
Wanakula ‘kitimoto’ pamoja na
wanacheka vilivyo, nani anajali?Kuna
watu wachache walikiweka mikononi
Chama cha soka nchini FAT,enzi hizo.
Nani alijali? Kama si kuvurugana
wenyewe kwa wenyewe wangeweza kuwepo
mpaka leo.Ndio, Rais wa nchi
alikuwepo, lakini hakuwa na muda wa
kujali. Kipaza sauti kilikuwa
kinamwambia asijali mambo hayo ila
aelekeze macho katika Utandawazi.
Ndio, utandawazi ambao unaruhusu
tupeleke makontena ya mchanga
uliochanganyika na dhahabu nje ya
mipaka yetu. Nani anajali?Wachache
wanajaribu kujali lakini nani
anawasikia? Wenyewe wanakutana
Golden Tulip wakila firigisi na
kupeana ruhusa hizo. Mimi na wewe
tujali nini wakati hatuna uhakika wa
kesho?
Tukipata watoto nao wanaingia katika
mkumbo huo huo wa kutojali. Kizazi
hiki ambacho watoto wengi wamegeukia
hisia za kimagharibi ni yupi kati
yao anaweza kujali?Wa kiume
anakazania kusuka, wa kike anatamani
kuvaa kama Beyonce. Hakuna hata
mmoja mwenye hisia na nchi. Hawezi
kujali kwa sababu hajafundishwa
kujali.
Ukisikiliza maoni ya wengi kuhusiana
na kesi ya Justine Kasusura, wengi
wanamlaumu kwa nini hakutoweka nje
ya nchi. Hakuna anayesikitika kwa
kitendo chake cha kuiba fedha. Kwa
nini?Watu hawajali alichokifanya.
Yeye alifanya hadharani lakini kuna
wanaoiba kwa karatasi? Hawa akina
‘Kasusura’ wa mezani nani anawazuia?
Nani anawajali?Iko wapi Kampuni ya
Richmond? Mbona kimya? Nani anajali?
Kwa sasa umeme upo na watu hawajali
tena. Wanataka ije ‘Richmond’
nyingine ya Maji au huduma za Afya.
Nani anajali?
Ndio, sijawahi na wala sitaki kupiga
kura. Yupo atakayesema napoteza haki
yangu ya msingi. Simuoni wa kunijali
na hata kama akiamua kunijali basi
mfumo hauwezi kumsapoti
anijali.Wakati wananchi wengine
wakipiga kura mimi naangalia vipindi
vya soka katika Televisheni, kwa
nini uniambie sijali wakati
atakayechaguliwa hatanijali?
Katika kituo cha wapiga kura chenye
wakazi 1000 lakini mshindi ameshinda
kwa kura 1200, kwa nini nijali
kusumbuka juani huku FFU wakinighasi
wakati waliopanga matokeo hawaijali
kura yangu?Nijali nini hasa kwa
kutompigia kura mtu atakayekwenda
bungeni kupitisha sheria ya Takrima?
Acha nifuatilie Ligi kuu ya England
na utamu wake.
Soma magazeti yetu ya leo. Watu
wameamua kuandika mambo laini ambayo
si sehemu ya mapambano yetu.Makala
za leo ni zile zile zinazoelezea kwa
undani Habari za Theolojia, Ulokole,
na mambo mengine. Mwananchi asiye na
uhakika na machweo ataelewa nini na
kupata tumaini jema katika makala
hizi? Wanaoziandika hawajali
kinachotokea kwa sasa.
Kwetu, kiongozi kutajwa anamiliki
hiki na kile kwa jina la mwanae, si
kashfa. Kwetu, mtoto wa mkubwa au
mkubwa mwenyewe kuua si jambo la
ajabu sana. Nani anajali? Wao na
Kamanda wa Polisi wanakutana
Kilimanjaro Kempsky katika dhifa
mbalimbali, unajua wanaongea nini?
Kwa nini ujitie kimbelembele cha
kujali? Ili mradi unapumua, iangalie
siku yako ya kesho.Tanzania ya leo
imejaa watu wanaozijali familia zao.
Nani atawalaumu watu hawa? Kwani
viongozi wetu wanawajali kina nani?
Si wanajali elimu za watoto wao pale
Oxford, Havard na kwingineko?Kama
unabisha, mbona sasa hivi ndio
wanatuongoza? Nani anajali? Tuna
uhakika gani kama baadaye wajukuu
hawataongoza? Si ndio wanapewa
ukamanda wa vijana wakijiandaa
kumtawala mwanangu ambaye ni mnyonge
wa baadaye? Nani anajali?Sina hasira
na mtu.
Nina furaha na maisha yangu kwa
sababu napata ninachokitaka kwa
uhalali. Kama maisha yataendelea
kuwa hivi basi nisilaumiwe kwa
kutojali. Nina uhakika gani kama
wenzangu wanajali?Kilio kama changu
kimetamkwa mara ngapi na watu
makini? Nani amejali? Kelele za
mchanga wa dhahabu nani amezijali?
Waliongia mikabata mibovu ya madini
nani anawajali? Wangekuwa
Chini,Japan, Uingereza na
kwingineko, wangekuwa wapi watu hawa
kama si katika kuta za Gereza? Hapa
kwetu nani anajali?Lakini nijali
nini zaidi wakati Rais wa nchi
aliwahi kuwatamkia watu walioelezea
hisia zao kwa Waziri Mkuu wake
kuhusu umilione wake wa mashaka,
kwamba wana wivu? Kama yeye mtu wa
juu kabisa hakujali, nani atajali?
Utawala ule ulikumbana na migomo ya
wanafunzi, huu nao unakumbana na
migomo hiyo hiyo, nani anajali? Kuna
njia za kudumu za kumaliza migomo
hiyo ambayo nimeisikia tangu utotoni
mwangu?Huyu anakabiliana nayo leo,
akihamishiwa anahama na hisia zake.
Yule anakuja na hisia nyingine na
wala hajali kutazama alipoishia
mwenzake.
Leo, kuna watu wengi wanapiga kelele
kuhusiana na hatari ya kujiunga na
Jumuiya ya Afrika Mashariki. Nani
anawasikiliza? Mimi naweza kuwa
sehemu ya maamuzi hayo?Wanaotoa
tahadhari ni watu wasomi. Afadhali
ingekuwa kwangu mtu nisiye na elimu,
lakini wanaotoa tahadhari hizi ni
watu wanaoheshimika kwa elimu na
upeo wao.
Najua hawasikilizwi lakini nani
anajali? Kama wenzao hawajali, nani
atanisikiliza mimi nisiye na lolote?
Acha waamue nami nitatii kwani
waliamua mangapi ya hatari na
nimeendelea kutii? SijaliLakini kwa
nini nimewang’angania wasiojali
wakati hata wenyewe wakifa au
kuondoka madarakani hakuna
anayewajali?
Wako wapi waliojali ambao familia
zao zinaishi kama vile baba zao
hawakujali? Ndio, familia za akina
Edward Sokoine. Nina uhakika watoto
wao watajuta kwa kitendo cha baba
yao kujali sana wakati wa utawala
wake.Ndio, na hata ninapomaliza
kuandika makala hii, wengi wataelewa
ninachomaanisha. Wakubwa wengi na
watu wa kawaida wataisoma na
kuielewa. Lakini nani atajali?

CHANZO:edo kumwembe
sizani edo kumwembe ana akili amesahau alivyokuwa akioga mchana kweupe kwenye kisima cha kuchotea maji bila kujali alikuwa akiwaathiri kisaikolojia wanafunzi ambao madarasa yao yalikuwa karibu na hostel hiyo ya jitegemee,amesahau alivyokuwa akiwalaghai form 1 na akifanya nao mapenzi darasani usiku,amesahau alivyo kuwa akisaidiwa nadhani atanielewa,mtu wa namna hii hawezi kuirubuni fikra nzima ya tanzania kwa misemo ya kitoto ,poor eddo kumwembe
 
sizani edo kumwembe ana akili amesahau alivyokuwa akioga mchana kweupe kwenye kisima cha kuchotea maji bila kujali alikuwa akiwaathiri kisaikolojia wanafunzi ambao madarasa yao yalikuwa karibu na hostel hiyo ya jitegemee,amesahau alivyokuwa akiwalaghai form 1 na akifanya nao mapenzi darasani usiku,amesahau alivyo kuwa akisaidiwa nadhani atanielewa,mtu wa namna hii hawezi kuirubuni fikra nzima ya tanzania kwa misemo ya kitoto ,poor eddo kumwembe

Those were the days when the young Edo was in his young-hood. Do you think those tales can stand any chance at these days? I would advise you to give appreciation to Edo for his 'unexpected' behavior change.
Wote tuna historia zetu, lakini tupongezane kwa kujitambua badala ya kuwa na hisia mgando. Nimalizie kwa kukuuliza swali dogo sana; Je unaweza kusimama pale anaposimama Edo kwa sasa?
 
Nani anaijali hatima ya Tanzania?


Ni nchi ya ajabu kwa mwanadamu makini kuweza kuishi. Ni nchi inayoshangaza sana, ingawa raia wake hawaonyeshi kushangazwa na matukio kadhaa yanayotokea.

Naizungumzia Tanzania nchi niliyoishi kwa miongo kadhaa tangu nizaliwe. Baada ya nyimbo nyingi za matatizo, dhiki, wizi, rushwa, tabu, magonjwa na kila aina ya shida ambayo mwanadamu wa kawaida anapitia, jawabu kubwa linapatika kwa swali; nani anajali?Ndio, nani anajali? Hili ni swali ambalo kila Mtanzania anapaswa kuulizwa.

Ni kwa kiasi gani, mwananchi wa kawaida, kiongozi au muhusika yeyote wa nchi hii anajali matatizo ya nchi yetu.Nimejaribu kwa kiasi kikubwa kutazama sura za viongozi wetu, mawaziri, wabunge, Wakurugenzi, Mameneja na kila kiongozi. Sioni anayejali.Wengi wanaongea wasichofikiria kukifanya kwa dhati na nchi imezidi kuoza. Akili zao ziko katika wizi kwa sababu na wananchi wenyewe wala viongozi wengine hawajali.Nchi inatafunwa kila jua linapochomoza na kuzama. Hakuna anayejali na kila mtu anaangalia maisha yake.

Msukuma mkokoteni haoni ni kwa namna gani anahusika na Waziri mwizi wala Mkurugenzi wa Manispaa mla rushwa.Atajihusisha vipi? Kwa nini atumie muda wake mwingi kujali? Kama watu wanaomzunguka hawajali kula yake kwa nini na yeye awe anajali maisha ya wengine.Siwezi kusema nilifaidi matunda ya utawala wa Mwalimu Nyerere. Sijui mengi yaliyotokea wakati wa Utawala wake, lakini tangu nilipopata akili timamu sijawahi kusikia Rais wa nchi yangu akimfukuza kazi Waziri wake kwa rushwa wala wizi.

Je ni kweli kwamba marais wangu hawawaoni Mawaziri wezi na wala rushwa? Kama wangekuwa watiifu na waadilifu basi nchi yetu ingekuwa mbali. Lakini naamini wanawaona, kikubwa ni kwa vile hawajali kinachotokea.

Hawajali kwa sababu hawana sababu ya kujali. Kwa kuwa wananchi hawajali basi na wao hawajali kama ambavyo wananchi hawajali. Wanaendelea kutojali na daima tunaendelea kupata vizazi vya Watanzania wasiojali.Kwani tukifungua mikataba ya ajabu ya Madini hatuwaoni walioweka saini hizo? Tunawaona, lakini nani anajali? Nchi inasonga mbele na maisha yanaendelea.

Huyu anajaribu kuandika gazetini kwa uchungu na yule anatamka lile katika kipindi cha redio kwa uchungu, lakini nani anajali? Kina mama na watoto wanafungulia michezo ya maigizo ITV na kwingineko. Nani atawalaumu wakati watu makini wenyewe hawajali? Si afadhali nao wasijali!Kwani yuko wapi yule Waziri aliyesema yuko tayari kuona wananchi wanakula majani ili ndege ya Rais inunuliwe? Ndege ambayo ni mbovu!. Si amechaguliwa tena kuwa Waziri? Nani anajali kama Rais wa sasa hakujali? Mimi nitajali nini?

Ni mwananchi gani anajali? Walio wengi wanafanya maaandamano katika mikasa ya kidini au ile ya kumpongeza Rais aliyefutiwa madeni ambayo fedha zake zilitumiwa kununua mashangingi.Kuna anayejali kwenda katika maandamano ya kupinga kupanda kwa bei ya umeme? Kuna anayejali kuandamana baada ya kusikia Nesi amesababisha kichanga kufa sekunde chache baada ya mama mjamzito kujifungua?

Hakuna anayejali kwa sababu hata akiandamana kwa uchungu mkubwa, Rais hawezi kumwajibisha Waziri wa Afya!. Ndivyo nchi ilivyo na watu wengi wamekwenda jela baada ya kutoa taarifa njema kwa jeshi la Polisi.

Lakini nani anajali kuwepo kwao jela? Ukitoa taarifa kuhusiana na mkubwa fulani anayepokea rushwa, kesho yake Kamanda wa Polisi wa Mkoa anakuonya na kukwambia uachane naye.Kwa nini niendelee kujali kwa watu ambao hawajali? Watu wangapi walishikwa na madawa ya kulevya katika Uwanja wa ndege wa kimataifa wa Dar es salaam lakini wapo nje kwa madai kwamba uchunguzi unaendelea?

Uchunguzi upi wakati madawa yalitolewa tumboni na tukaonyeshwa katika taarifa za habari za Televisheni mbalimbali? Kwa nini niendelee kujali kuwepo nje kwa mtuhumiwa wakati Kamanda wa Polisi wa mkoa haonyeshi kujali?Yuko wapi dada machachari Mbunge wa kike aliyedai kwamba ana majina ya wauza madawa wa kulevya? Ni kweli kwamba alizungumza jambo jipya katika jamii yetu ya watu wasiojali?

Tunao watu wengi wanaouza madawa na kwa bahati wanajulikana, lakini nani anajali? Dada yule ?alionyesha? kujali, lakini baada ya hapo nani amejali? Mbona hatujasikia mtu amekwenda ndani kutokana na mdomo wake?Tangu baada ya ?mauaji? ya basi ya Buffalo, magari yanazidi kwenda kasi barabarani. Nani anajali? Si mpaka watu wengine wafe ndio tusikie tamko jingine la kinafiki?Kuna meli ngapi mbovu pale Ziwa Victoria na sehemu nyingine zenye vyombo vya usafiri wa majini? Kwa sababu hakuna anayekufa kwa sasa wahusika na wananchi hawajali mpaka litokee janga.

Ili mradi asubuhi inafika, mchana unapita na jioni inawadia basi hakuna anayejali mpaka litokee janga. Nani anajali?Mchele mbovu unahalalishwa, watu wanatengeza maji ya ?kufoji? na kuuza, nani anajali? Nikienda kusema Polisi wananitazama kwa jicho la chuki lakini tayari nimeshawaachia mianya ya rushwa.

Keshokutwa nakutana na mkubwa wa Polisi niliyemshtua akiwa pamoja na mkuu wa Kiwanda nilichokishtaki. Wanakula ?kitimoto? pamoja na wanacheka vilivyo, nani anajali?Kuna watu wachache walikiweka mikononi Chama cha soka nchini FAT,enzi hizo. Nani alijali? Kama si kuvurugana wenyewe kwa wenyewe wangeweza kuwepo mpaka leo.Ndio, Rais wa nchi alikuwepo, lakini hakuwa na muda wa kujali. Kipaza sauti kilikuwa kinamwambia asijali mambo hayo ila aelekeze macho katika Utandawazi.

Ndio, utandawazi ambao unaruhusu tupeleke makontena ya mchanga uliochanganyika na dhahabu nje ya mipaka yetu. Nani anajali?Wachache wanajaribu kujali lakini nani anawasikia? Wenyewe wanakutana Golden Tulip wakila firigisi na kupeana ruhusa hizo. Mimi na wewe tujali nini wakati hatuna uhakika wa kesho?

Tukipata watoto nao wanaingia katika mkumbo huo huo wa kutojali. Kizazi hiki ambacho watoto wengi wamegeukia hisia za kimagharibi ni yupi kati yao anaweza kujali?Wa kiume anakazania kusuka, wa kike anatamani kuvaa kama Beyonce. Hakuna hata mmoja mwenye hisia na nchi. Hawezi kujali kwa sababu hajafundishwa kujali.

Ukisikiliza maoni ya wengi kuhusiana na kesi ya Justine Kasusura, wengi wanamlaumu kwa nini hakutoweka nje ya nchi. Hakuna anayesikitika kwa kitendo chake cha kuiba fedha. Kwa nini?Watu hawajali alichokifanya. Yeye alifanya hadharani lakini kuna wanaoiba kwa karatasi? Hawa akina ?Kasusura? wa mezani nani anawazuia? Nani anawajali?Iko wapi Kampuni ya Richmond? Mbona kimya? Nani anajali? Kwa sasa umeme upo na watu hawajali tena. Wanataka ije ?Richmond? nyingine ya Maji au huduma za Afya. Nani anajali?

Ndio, sijawahi na wala sitaki kupiga kura. Yupo atakayesema napoteza haki yangu ya msingi. Simuoni wa kunijali na hata kama akiamua kunijali basi mfumo hauwezi kumsapoti anijali.Wakati wananchi wengine wakipiga kura mimi naangalia vipindi vya soka katika Televisheni, kwa nini uniambie sijali wakati atakayechaguliwa hatanijali?

Katika kituo cha wapiga kura chenye wakazi 1000 lakini mshindi ameshinda kwa kura 1200, kwa nini nijali kusumbuka juani huku FFU wakinighasi wakati waliopanga matokeo hawaijali kura yangu?Nijali nini hasa kwa kutompigia kura mtu atakayekwenda bungeni kupitisha sheria ya Takrima? Acha nifuatilie Ligi kuu ya England na utamu wake.

Soma magazeti yetu ya leo. Watu wameamua kuandika mambo laini ambayo si sehemu ya mapambano yetu.Makala za leo ni zile zile zinazoelezea kwa undani Habari za Theolojia, Ulokole, na mambo mengine. Mwananchi asiye na uhakika na machweo ataelewa nini na kupata tumaini jema katika makala hizi? Wanaoziandika hawajali kinachotokea kwa sasa.

Kwetu, kiongozi kutajwa anamiliki hiki na kile kwa jina la mwanae, si kashfa. Kwetu, mtoto wa mkubwa au mkubwa mwenyewe kuua si jambo la ajabu sana. Nani anajali? Wao na Kamanda wa Polisi wanakutana Kilimanjaro Kempsky katika dhifa mbalimbali, unajua wanaongea nini? Kwa nini ujitie kimbelembele cha kujali? Ili mradi unapumua, iangalie siku yako ya kesho.Tanzania ya leo imejaa watu wanaozijali familia zao.

Nani atawalaumu watu hawa? Kwani viongozi wetu wanawajali kina nani? Si wanajali elimu za watoto wao pale Oxford, Havard na kwingineko?Kama unabisha, mbona sasa hivi ndio wanatuongoza? Nani anajali? Tuna uhakika gani kama baadaye wajukuu hawataongoza? Si ndio wanapewa ukamanda wa vijana wakijiandaa kumtawala mwanangu ambaye ni mnyonge wa baadaye? Nani anajali?Sina hasira na mtu.

Nina furaha na maisha yangu kwa sababu napata ninachokitaka kwa uhalali. Kama maisha yataendelea kuwa hivi basi nisilaumiwe kwa kutojali. Nina uhakika gani kama wenzangu wanajali?Kilio kama changu kimetamkwa mara ngapi na watu makini? Nani amejali? Kelele za mchanga wa dhahabu nani amezijali?Waliongia mikabata mibovu ya madini nani anawajali? Wangekuwa Chini,Japan, Uingereza na kwingineko, wangekuwa wapi watu hawa kama si katika kuta za Gereza? Hapa kwetu nani anajali?Lakini nijali nini zaidi wakati Rais wa nchi aliwahi kuwatamkia watu walioelezea hisia zao kwa Waziri Mkuu wake kuhusu umilione wake wa mashaka, kwamba wana wivu? Kama yeye mtu wa juu kabisa hakujali, nani atajali?Utawala ule ulikumbana na migomo ya wanafunzi, huu nao unakumbana na migomo hiyo hiyo, nani anajali? Kuna njia za kudumu za kumaliza migomo hiyo ambayo nimeisikia tangu utotoni mwangu?Huyu anakabiliana nayo leo, akihamishiwa anahama na hisia zake. Yule anakuja na hisia nyingine na wala hajali kutazama alipoishia mwenzake.

Leo, kuna watu wengi wanapiga kelele kuhusiana na hatari ya kujiunga na Jumuiya ya Afrika Mashariki. Nani anawasikiliza? Mimi naweza kuwa sehemu ya maamuzi hayo?Wanaotoa tahadhari ni watu wasomi. Afadhali ingekuwa kwangu mtu nisiye na elimu, lakini wanaotoa tahadhari hizi ni watu wanaoheshimika kwa elimu na upeo wao.

Najua hawasikilizwi lakini nani anajali? Kama wenzao hawajali, nani atanisikiliza mimi nisiye na lolote? Acha waamue nami nitatii kwani waliamua mangapi ya hatari na nimeendelea kutii? SijaliLakini kwa nini nimewang?angania wasiojali wakati hata wenyewe wakifa au kuondoka madarakani hakuna anayewajali?

Wako wapi waliojali ambao familia zao zinaishi kama vile baba zao hawakujali? Ndio, familia za akina Edward Sokoine. Nina uhakika watoto wao watajuta kwa kitendo cha baba yao kujali sana wakati wa utawala wake.Ndio, na hata ninapomaliza kuandika makala hii, wengi wataelewa ninachomaanisha. Wakubwa wengi na watu wa kawaida wataisoma na kuielewa. Lakini nani atajali?
 
Good thinking.
Mwanzishq mada tafadhali tambulisha chanzo. Huyu ni eddo kumwembe
 
Ngoja niende beach kwenye kaupepo mwanana nitulie nikusome vizuri!
 
Nani anaijali hatima ya Tanzania?

Na George E Mwaipungu

Ni Nchi ya ajabu kwa Mwanadamu makini kuweza kuishi. Ni Nchi inayoshangaza sana, ingawa raia wake hawaonyeshi kushangazwa na matukio kadhaa yanayotokea.

Naizungumzia Tanzania Nchi niliyoishi kwa miongo kadhaa tangu nizaliwe. Baada ya Nyimbo nyingi za Matatizo, Dhiki, Wizi, Rushwa, Taabu, Magonjwa na kila aina ya Shida ambayo Mwanadamu wa kawaida anapitia, Jawabu kubwa linapatika kwa Swali;
Nani wa Kujali? Ndio, Nani anajali? Hili ni Swali ambalo kila Mtanzania anapaswa kuulizwa.

Ni kwa kiasi gani, Mwananchi wa Kawaida, Kiongozi au Muhusika yeyote wa Nchi hii anajali matatizo ya Nchi yetu?.
Nimejaribu kwa kiasi kikubwa kutazama Sura za Viongozi wetu, Mawaziri, Wabunge, Wakurugenzi, Mameneja na kila Kiongozi, Sioni anayejali, Wengi wanaongea wasichofikiria kukifanya kwa dhati toka Rohoni. Na Nchi imezidi kuoza. Akili zao ziko katika Wizi tu, kwa sababu na Wananchi wenyewe na Viongozi wao hawajali.
Nchi inatafunwa kila jua linapochomoza na kuzama. Hakuna anayejali na kila mtu anaangalia maisha yake.

Msukuma Mkokoteni haoni ni kwa namna gani anahusika na Waziri Mwizi wala Mkurugenzi wa Manispaa mla Rushwa. Atajihusisha vipi? Kwa nini atumie muda wake mwingi kujali? Kama watu wanaomzunguka hawajali kula yake!! kwa nini na yeye awe anajali maisha ya wengine?
Siwezi kusema nilifaidi matunda ya utawala wa Mwalimu Nyerere.
Sijui mengi yaliyotokea wakati wa Utawala wake, lakini tangu nilipopata akili timamu sijawahi kusikia Rais wa Nchi Yangu akimfukuza kazi Waziri wake kwa Rushwa wala Wizi.

Je ni kweli kwamba Ma-Rais wangu hawawaoni Mawaziri Wezi na wala Rushwa?
Kama wangekuwa Watiifu na Waadilifu basi Nchi yetu ingekuwa mbali sana. Lakini naamini wanawaona, kikubwa ni kwa vile Hawajali kinachotokea.

Hawajali kwa sababu hawana sababu ya kujali' Kwa kuwa Wananchi hawajali basi na wao Hawajali kama ambavyo wananchi hawajali. Wanaendelea kutojali na daima tunaendelea kupata Vizazi vya Wa-Tanzania wasiojali.
Kwani tukifungua Mikataba ya ajabu ya Madini hatuwaoni walioweka saini? Tunawaona, lakini nani anajali? Nchi inasonga mbele na maisha yanaendelea.

Huyu anajaribu kuandika gazetini kwa uchungu na yule anatamka lile katika kipindi cha Radio kwa Uchungu, lakini nani Anajali? Kina Mama na Watoto wanafungulia Michezo ya Maigizo ITV na kwingineko. Nani atawalaumu wakati watu makini wenyewe Hawajali? Si afadhali nao wasijali!Kwani yuko wapi yule Waziri aliyesema yuko tayari kuona Wananchi wanakula Majani ili Ndege ya Rais inunuliwe? Ndege ambayo ni Mbovu!. Si amechaguliwa tena kuwa Waziri? Nani anajali kama Rais wa sasa hakujali? Mimi nitajali nini?

Ni Mwananchi gani anajali? Walio wengi wanafanya Maandamano katika Mikasa ya Kidini au ile ya kumpongeza Rais aliyefutiwa Madeni ambayo Fedha zake zilitumiwa kununua Mashangingi.
Kuna anayejali kwenda katika maandamano ya kupinga kupanda kwa bei ya umeme?
Kuna anayejali kuandamana baada ya kusikia Nesi amesababisha kichanga Kufa Sekunde chache baada ya mama Mjamzito kujifungua?

Hakuna anayejali kwa Sababu hata akiandamana kwa Uchungu Mkubwa, Rais hawezi kumwajibisha Waziri wa Afya!.
Ndivyo Nchi ilivyo na watu wengi wamekwenda Jela baada ya kutoa taarifa Njema kwa Jeshi la Polisi.

Lakini nani anajali kuwepo kwao Jela?
Ukitoa Taarifa kuhusiana na Mkubwa fulani anayepokea Rushwa, kesho yake Kamanda wa Polisi wa Mkoa anakuonya na kukwambia uachane naye.
Kwa nini niendelee kujali kwa watu ambao hawajali?
Watu wangapi walishikwa na Madawa ya Kulevya katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Dar Es Salaam lakini wapo nje kwa madai kwamba Uchunguzi unaendelea?

Uchunguzi upi wakati Madawa yalitolewa Tumboni na tukaonyeshwa katika Taarifa za Habari za Televisheni mbalimbali? Kwa nini niendelee kujali kuwepo nje kwa mtuhumiwa wakati Kamanda wa Polisi wa mkoa haonyeshi kujali?
Yuko wapi Dada machachari Mbunge wa Kike aliyedai kwamba ana majina ya Wauza Madawa ya kulevya?
Ni kweli kwamba alizungumza jambo jipya katika jamii yetu ya watu wasiojali?

Tunao watu wengi wanaouza Madawa na kwa Bahati wanajulikana, lakini nani anajali? Dada yule ?alionyesha? Kujali, lakini baada ya hapo nani Amejali?
Mbona hatujasikia mtu amekwenda ndani kutokana na mdomo wake.
Tangu baada ya ?mauaji? ya basi ya Buffalo, magari yanazidi kwenda kasi barabarani, Nani anajali?
Si mpaka watu wengine wafe ndipo tusikie tamko jingine la kinafiki?
Kuna meli ngapi mbovu pale Ziwa Victoria na sehemu nyingine zenye vyombo vya usafiri wa majini?
Kwa sababu hakuna anayekufa kwa sasa wahusika na Wananchi hawajali mpaka litokee Janga.

Ili mradi asubuhi inafika, mchana unapita na jioni inawadia basi hakuna anayejali mpaka litokee janga.
Nani anajali Mchele mbovu unahalalishwa?
Watu wanatengeza Maji ya ?Feki? na kuuza, nani anajali?
Nikienda kusema Polisi wananitazama kwa jicho la Chuki lakini tayari nimeshawaachia mianya ya Rushwa.

Keshokutwa nakutana na mkubwa wa Polisi niliyemshtua akiwa pamoja na Mkuu wa Kiwanda nilichokishtaki.
Wanakula ?Kitimoto? pamoja na wanacheka vilivyo, nani anajali?
Kuna watu wachache walikiweka mikononi Chama cha soka nchini FAT,enzi hizo Nani alijali?
Kama si kuvurugana wenyewe kwa wenyewe wangeweza kuwepo mpaka leo.
Rais wa nchi alikuwepo, lakini hakuwa na muda wa kujali. Kipaza sauti kilikuwa kinamwambia asijali mambo hayo ila aelekeze macho katika Utandawazi.

Ndio, utandawazi ambao unaruhusu tupeleke Makontena ya Mchanga uliochanganyika na Dhahabu Nje ya Mipaka yetu. Nani anajali?
Watu Wachache wanajaribu kujali lakini Nani anawasikia?
Wenyewe wanakutana Golden Tulip wakila Firigisi na kupeana ruhusa hizo. Mimi na wewe tujali nini wakati hatuna uhakika wa kesho?

Tukipata watoto nao wanaingia katika mkumbo huo huo wa kutojali. Kizazi hiki ambacho watoto wengi wamegeukia hisia za Kimagharibi ni yupi kati yao anaweza kujali?
Wa Kiume anakazania Kusuka, wa Kike anatamani kuvaa kama Beyonce.
Hakuna hata mmoja mwenye hisia na nchi. Hawezi kujali kwa sababu hajafundishwa kujali.

Ukisikiliza maoni ya wengi kuhusiana na kesi ya Justine Kasusura, wengi wanamlaumu kwa nini hakutoweka nje ya Nchi. Hakuna anayesikitika kwa kitendo chake cha kuiba Fedha. Unafikiri ni Kwa nini?
Watu hawajali alichokifanya. Yeye alifanya hadharani lakini kuna wanaoiba kwa karatasi?
Hawa akina ?Kasusura? wa Mezani nani anawazuia? Nani anawajali? Iko wapi Kampuni ya Richmond? Mbona kimya? Nani anajali? Kwa sasa umeme upo na watu hawajali tena Wanataka ije ?Richmond? nyingine ya Maji au huduma za Afya. Nani anajali?

Ndio Maana hakuna umuhimu wa kupiga Kura wala sitaki kupiga kura. Yupo atakayesema napoteza haki yangu ya msingi. Simuoni wa kunijali na hata kama akiamua kunijali basi mfumo hauwezi kumsapoti anijali.
Wakati Wananchi wengine wakipiga Kura mimi naangalia vipindi vya soka katika Televisheni, kwa nini uniambie sijali wakati atakayechaguliwa hatanijali?

Katika kituo cha wapiga kura chenye wakazi 1000 lakini mshindi ameshinda kwa kura 1200. Kwa nini nijali? kusumbuka juani huku FFU wakinighasi wakati waliopanga matokeo hawaijali kura yangu?
Nijali nini hasa kwa kutompigia kura mtu atakayekwenda bungeni kupitisha sheria ya Takrima?
Acha nifuatilie Ligi kuu ya England na utamu wake.

Soma Magazeti yetu ya leo. Watu wameamua kuandika mambo laini ambayo si sehemu ya Mapambano yetu.
Makala za leo ni zile zile zinazoelezea kwa undani Habari za Theolojia, Ulokole, na mambo mengine. Mwananchi asiye na uhakika na machweo ataelewa nini na kupata tumaini jema katika makala hizi? Wanaoziandika hawajali kinachotokea kwa sasa.

Kwetu, Kiongozi kutajwa anamiliki hiki na kile kwa Jina la Mwanae, si Kashfa.
Kwetu, Mtoto wa Mkubwa au Mkubwa Mwenyewe kuua si jambo la ajabu sana. Nani anajali?
Wao na Kamanda wa Polisi wanakutana Kilimanjaro Kempsky katika dhifa mbalimbali, unajua wanaongea nini?
Kwa nini ujitie kimbelembele cha kujali?
Ili Mradi unapumua, iangalie siku yako ya kesho.Tanzania ya leo imejaa watu wanaozijali familia zao.

Nani atawalaumu watu hawa? Kwani viongozi wetu wanawajali kina nani? Si wanajali Elimu za Watoto wao pale Oxford, Havard na kwingineko?
Kama Unabisha, mbona sasa hivi ndio wanatuongoza? Nani anajali? Tuna uhakika gani kama baadaye wajukuu hawataongoza? Si ndio wanapewa Ukamanda wa Vijana Wakijiandaa ku-mtawala Mwanangu ambaye ni mnyonge wa baadaye? Nani anajali? Sina hasira na mtu.

Nina Furaha na Maisha Yangu kwa Sababu napata ninachokitaka kwa uhalali. Kama maisha yataendelea kuwa hivi basi nisilaumiwe kwa kutojali.
Nina uhakika gani kama nzangu wanajali?Kilio kama changu kimetamkwa mara ngapi na watu makini? Nani amejali? Kelele za mchanga wa dhahabu nani amezijali?Waliongia mikabata mibovu ya madini nani anawajali? Wangekuwa China, Japan, Uingereza na Kwingineko, wangekuwa wapi watu hawa kama si katika kuta za Gereza? Hapa kwetu nani anajali?
Lakini nijali nini zaidi wakati Rais wa Nchi aliwahi kuwatamkia watu walioelezea hisia zao kwa Waziri Mkuu wake kuhusu Umilione wake wa Mashaka, kwamba wana Wivu? Kama yeye mtu wa juu kabisa Hakujali, nani Atajali?
Utawala ule ulikumbana na migomo ya Wanafunzi, huu nao unakumbana na migomo hiyo hiyo, nani anajali? Kuna njia za kudumu za kumaliza migomo hiyo ambayo nimeisikia tangu utotoni mwangu? Huyu anakabiliana nayo leo, akihamishiwa anahama na hisia zake. Yule anakuja na hisia nyingine na wala hajali kutazama alipoishia mwenzake.

Leo, kuna watu wengi wanapiga kelele kuhusiana na hatari ya kujiunga na Jumuiya ya Afrika Mashariki. Nani anawasikiliza?
Mimi naweza kuwa sehemu ya maamuzi hayo?
Wanaotoa tahadhari ni watu wasomi. Afadhali ingekuwa kwangu mtu nisiye na elimu, lakini wanaotoa tahadhari hizi ni watu wanaoheshimika kwa elimu na upeo wao.

Najua hawasikilizwi lakini nani anajali? Kama wenzao hawajali, nani atanisikiliza mimi nisiye na lolote? Acha waamue nami nitatii kwani waliamua Mangapi ya Hatari na hivyo na nimeendelea Kutii? SijaliLakini kwa nini nimewang?angania wasiojali wakati hata wenyewe wakifa au kuondoka madarakani hakuna anayewajali?

Wako wapi waliojali ambao Familia zao zinaishi kama vile Baba zao hawakujali?
Ndio, familia za akina Edward Sokoine. Nina uhakika Watoto wao watajuta kwa kitendo cha Baba yao kujali sana wakati wa Utawala wake, na hata ninapomaliza kuandika makala hii, Wengi wataelewa ninachomaanisha. Wakubwa Wengi na Watu wa Kawaida wataisoma na kuielewa. Lakini nani atajali?
 
umelalamika sana..nini chakufanya? ilibidi mwisho wa makala yako angalau utoe nini watu wafanye???
 
Tanzania ina IQ ya chini kuliko nchi yo yote duniani.
 
Back
Top Bottom