Nani anajali Mradi wangu?

Nani anajali Mradi wangu?

Omar Msonga

New Member
Joined
Feb 6, 2021
Posts
0
Reaction score
3
1615390734857.png


Katika utafutaji wa fedha kwa ajili ya kutekeleza miradi ya maendeleo (grant support for community projects), vyanzo mbalimbali huweza kutumika, vyanzo hivyo hujumuisha;
  • Taasisi Binafsi (Private Foundations) mfano; Foundation for Civil Society, Women Fund Tanzania n.k.
  • Taasisi za Kifamilia (Family Foundations) mfano Bill and Melinda Gates Foundation, John Stewart Motto Foundation n.k
  • Taasisi za Umma (Public Foundations) mfano Tanzania Forest Fund, Baraza la Uwezeshaji Kiuchumi la Taifa, local Government Funds n.k
  • Taasisi za Makampuni (Corporate Foundations) mfano Vodacom Foundations, Dangote Foundations, Mo Foundations n.k
  • Program za kutoa katika kampuni za kibiashara (Corportae Giving Programs) hizi programu huwepo kwenye kampuni zote kubwa, mfano tiGO, NMB, Coca Cola n.k

Katika utafutaji wa msaada wa kifedha kwa ajili ya kutekeleza miradi ya kijamii (community projects), kwenye program za utoaji wa kampuni za kibiashara (Corporate Giving Programs) wahusika katika utafutaji wa fedha hizo kwa maana ya "fundraisers" wanapaswa kujiuliza, "Nani anajali?" mradi wetu katika kampuni hii. Hii inasaidia kujua ni nani anayeweza kuwa mtu sahihi ambae unapaswa kuwasiliana naye, si kila mtu ndani ya kampuni anaweza kuwa msaada kwako kila wakati. Kwa mfano, ikiwa unatafuta mdhamini kwa ajili ya mradi wa tamasha la sanaa, unapaswa kumtafuta mtu anayeshughulika na masuala ya "branding" ya kampuni husika . Na ikiwa mradi wako una lengo la kuwawezesha wanawake imma kiuchumi au kijamii; mtu kutoka idara ya jamii au maendeleo ya uchumi atakuwa sahihi kwako. Ili kumfahamu mtu sahihi "anaejali" mradi wako pindi uendapo kwenye kampuni za kibiashara kuomba msaada wa kifedha, zingatia idara zifuatazo na kuona kama malengo yao yanarandana na malengo ya mradi wako
  • Viongozi wa vitengo vya biashara(Business Unit Leaders): Vitengo vya biashara vya kampuni huwa na malengo tofauti. Jitajhidi kufahamu uwekezaji wa kimkakati (strategic investment) kwa kila kitengo, ikiwa malengo ya uwekezaji wa kitengo B kwa mfano unarandana kwa kiasi kikubwa na malengo ya mradi wako, basi mtu sahihi wa kumfuata atakuwa ni Kiongozi wa kitengo B.
  • Watu wa idara ya Masoko (Marketing Professionals): Lengo kubwa la watu wa masoko ni kuongeza uuzaji wa bidhaa au huduma za kampuni kwa kikundi fulani cha watu au kwa umma kwa jumla. Ikiwa mradi wako unaweza kuwasaidia kupata ufikiaji wa watu hawa au kutoa fursa za kuongeza muonekano wa bidhaa au huduma zao, basi watu hawa watakuwa ni sahihi kuwafuata kwa ajili ya mradi wako.
  • Watu wa idara ya maendeleo ya jamii na uchumi (Community and Economic Development Staff): Ikiwa utekelezaji wa mradi wako utaweza kusaidia ukuaji wa uchumi na kuchochea maendeleo ya jamii katika eneo ambalo kampuni husika inafanya shughuli zake (area of operation), basi watu wa idara hii wataweza kupendezwa na mradi wako, hivyo watakuwa ni watu sahihi wa kuwafuata.
  • Watu wa idara ya Mawasiliano (Communications Officers): Hawa ni sauti ya kampuni na wanahusika na uhusiano wa umma, wanapaswa kuhakikisha kampuni inakuwa na taswira nzuri mbele ya umma (good public image). Ikiwa mradi wako utailetea kampuni taswira nzuri, pia utaimarisha mahusiano kati ya kampuni husika na jamii, basi kwa kiasi kikubwa watu hawa wataupenda mradi wako, hivyo you have to consider them pindi utakapoi-approach kampuni husika.
AHSANTE

OMAR MSONGA
PPM Consultant
Grant Search, Grant Writing, Fundraising, Project Management and NGO Management.
E-mail: omarmsonga8@gmail.com
Call, Text & WhatsApp: +255 719 518 367
Dar es Salaam
 
Back
Top Bottom