Nani anakibarua kizito hapo mbele kati ya Simba, Yanga, Azam na Singida huko CAF

Mhaya

JF-Expert Member
Joined
Aug 20, 2023
Posts
2,818
Reaction score
7,940
Timu zote za Zanzibar zatolewa katika michuano ya Shirikisho na Klabu bingwa barani Afrika.

Huku timu za Tanzania Bara (Tanganyika) zikibaki na kuendelea na raundi ya pili ya mtoano kabla ya makundi.

Simba atakutana na 15 De Agosto kutokea huko Equatorial Guinea (Guinea ya Ikweta) ambayo ndio timu iliyochukua ubingwa wa ligi kuu kwa msimu wa mwaka jana hapo Equatorial Guinea.

Yanga Africans atakutana na CFFA Andoharanofotsy kutokea kisiwa cha Madagascar, na hawa wamekuwa mabingwa katika ligi kuu ya Madagascar kwa kuchukua kikombe katika msimu wa mwaka jana.

Azam FC hakuanza katika hatua ya kwanza, lakini atakutana na ZED katika hatua ya mtoano. ZED ilifuzu kushiriki Kombe la Shirikisho la CAF msimu wa 2026/27 kupitia mashindano ya Kombe la Misri (Egypt Cup). ZED ilifika hadi fainali ya Kombe la Misri, ambapo ilipoteza dhidi ya Pyramids. Kufanya iwe mara yao ya kwanza kushiriki michuano hii ya kimataifa.

Singida Black Stars atakutana na Tusker FC kutokea Kenya. Walifuzu kushiriki Kombe la Shirikisho la CAF msimu wa 2026/27 baada ya kushinda FKF Cup ya mwaka 2026 (Mozzart Bet Cup). Tusker FC imewai kushiriki mara kadhaa michuano hii

Je nani ana kazi nzito ya kufuzu?
 
Simba tumepata timu ngumu inabidi icheze kwa akili kubwa na kujituma kweli kweli lakini naamini tutavuka salaam.
 
Nina wasiwasi na Azam pamoja na Singida Black Star hawako siriasi wanaweza kuaga mashindano, Yanga bado hawako vizuri watashinda kwa mbinde wakatie aibu kwenye makundi, Simba mechi ngumu ila watashinda
 
Timu zote za Zanzibar zatolewa katika michuano ya Shirikisho na Klabu bingwa barani Afrika.

Huku timu za Tanzania Bara (Tanganyika) zikibaki na kuendelea na raundi ya pili ya mtoano kabla ya makundi.

Simba atakutana na 15 De Agosto kutokea huko Equatorial Guinea (Guinea ya Ikweta) ambayo ndio timu iliyochukua ubingwa wa ligi kuu kwa msimu wa mwaka jana hapo Equatorial Guinea.

Yanga Africans atakutana na CFFA Andoharanofotsy kutokea kisiwa cha Madagascar, na hawa wamekuwa mabingwa katika ligi kuu ya Madagascar kwa kuchukua kikombe katika msimu wa mwaka jana.

Azam FC hakuanza katika hatua ya kwanza, lakini atakutana na ZED katika hatua ya mtoano. ZED ilifuzu kushiriki Kombe la Shirikisho la CAF msimu wa 2026/27 kupitia mashindano ya Kombe la Misri (Egypt Cup). ZED ilifika hadi fainali ya Kombe la Misri, ambapo ilipoteza dhidi ya Pyramids. Kufanya iwe mara yao ya kwanza kushiriki michuano hii ya kimataifa.

Singida Black Stars atakutana na Tusker FC kutokea Kenya. Walifuzu kushiriki Kombe la Shirikisho la CAF msimu wa 2026/27 baada ya kushinda FKF Cup ya mwaka 2026 (Mozzart Bet Cup). Tusker FC imewai kushiriki mara kadhaa michuano hii

Je nani ana kazi nzito ya kufuzu?
Singida na Azam
 
Back
Top Bottom