Nani anakumbuka David Wakati?

Umeuliza nani anamkumbuka David Wakati. Mimi ni mmojawapo. Ni kweli kabisa kwamba hata kipindi David Wakati akiwa Mkurugenzi Mkuu wa Radio Tanzania, bado alikuwa akishiriki kufanya kazi za kawaida za utangazaji. Kipindi cha 'Nipe Habari' hakikuwa na mtangazaji mwingine, mbali na David Wakati; labda awe na udhuru. Asilimia 90 ya vipindi hivyo alikuwa anavitangaza yeye mwenyewe. Ilikuwa kama mtangazaji mwingine akishika zamu inakuwa kama kipindi hakikuwepo siku hiyo. Kinapooza sana. Sawasawa na kipindi cha Majira kutangazwa na mwingine zaidi ya Ben Kiko. Msikilizaji huridhiki. David Wakati pia alikuwa akisoma taarifa za habari za Kiingereza ikijulikana kama Idhaa ya Nje. Nahisi walikuwepo watangazaji wachache tu Radio Tanzania waliokuwa wakikimudu Kiingereza ya kutosha, kama Rochus Matipa. Kwa hiyo ilibidi wapeane zamu hao wachache waliokuwa wanaimanya hiyo lugha. Matangazo kwenye ibaada za Kikristu wakati wa Noeli au Pasaka nayo alikuwa akiyamudu vizuri sana. Yeye alikuwa Anglikana. Lakini alikuwa akienda po pote pale ibaada inapofanyika na anafanya vizuri kabisa; iwe Kanisa Katoliki au la Kiluteri. Mola amlaze pema.
 
Mzee Mohamed Kwa nini walirudi mara ya pili?
 
Mzee Mohamed Kwa nini walirudi mara ya pili?
Idu...

Tuliishia pale mwisho wa kipindi nilipoulizwa kama mtangazaji anaweza kutafuta ithibati kwa Rais kwa yale niloyosema.

Kwanza kuhusu mchango Waislam katika kupigania uhuru wa Tanganyika.

Pili kama kuna ubaguzi dhidi ya Waislamu katika elimu na fursa zilizoko katika serikali na kwengineko.

Na mengineyo mfano wa hayo.

Baadae nikapata taarifa kuwa Al Jazeera walipokuwa Zanzibar vipindi vyoye walivyokuwa wamefanya vilipotea hotelini walipofikia.

Baada ya mwaka karibu wakaja Tanga tukafanya kipindi kingine.
Kipindi hiki hakikurushwa hadi leo na hawakuniambia kwa nini.
 
Mzee Mohamed unastori nzuri sana ila linapokuja suala la uonevu juu ya waislamu na ubaguzi dhidi ya waislamu hapa Tanzania ndio ukakasi unataokea.
 
Naona sasa ukiwa kwenye vijiwe vya kahawa mapipa unakenua mpaka jino la mwisho,Samia anateua viongozi wa nchi utasema anateua viongozi wa misikiti na madrasa!

Rais wa hovyo kutokea tangu uhuru,nchi imemshinda inapoelekea Mabeyo achukue nchi!
 
Mzee Mohamed unastori nzuri sana ila linapokuja suala la uonevu juu ya waislamu na ubaguzi dhidi ya waislamu hapa Tanzania ndio ukakasi unataokea.
Idu...
Labda nikuulize swali.

Unadhani haya nisemayo hayana umuhimu au ni uongo?

Nimeweka hapa hotuba ya Kitwana Kondo kuhusu ubaguzi katika elimu.

Nimeweka pia aliyoandika Aboud Jumbe kuhusu udini katika serikali.

Bahati mbaya hili limekuwa jambo nyeti serikali inasikia lakini inaona bora kubaki kimya.

Wewe si wa kuwajibu Waislam kuhusu hili.

Hili ni jukumu la serikali yenyewe kutoa majibu.

Ikiwa hupendi kusikia Waislam wakieleza dhulma iliyodumu dhidi yao toka uhuru hii ni bahati mbaya kwako.

Mimi hili sitaacha kulisema.

Sinong'oni nimasema na nyote mnasoma tena nikitumia jina langu.

Sijajificha kama vile Kitwana Kondo hakujificha na Aboud Jumbe hakujificha.

Allah anawaasa Waislam katika Qur'an anatuambia tusidhulumu na tusikubali kudhulumiwa.
 

No comment.
 
Idu...
Nafurahi kufanya mjadala nawe.
Mzee Mohamed, kuhusu akina Sykes kama unavyoeleza ni kweli walitoa mchango mkubwa kwenye kupigania uhuru wa taifa letu na kisha TANU ikaanzishwa. Ni kweli pia walikuwa waislamu lakini walijitoa kwa taifa lao sio kwa sababu ni waislamu. Walijitoa kama watanzania kwa nia njema kusaidia taifa lao.

Kama kuna makosa yalitokea wakabaguliwa basi iwekwe wazi walibaguliwa kama akina Sykes na sio sababu ni waislamu.

Hayo mengine weka kando kwanza.
 
Idu...
Historia nzima ya Waislam katika kupigania uhuru imefutwa na ilikuwa mtafiti akiwa anakuja Tanzania na akaleza kuwa nia ya utafiti wake inahusu Uislam alikuwa hapati kibali cha utafiti.

Unawajua ni masheikh wangapi walikuwa mstari wa mbele katika TANU?

Hata mmoja hayuko katika historia ilyochapwa mwaka wa 1981 na Chuo Cha CCM Kivukoni.

Unajua historia ya Sheikh Hassan bin Ameir Mufti wa Tanganyika?

Sheikh Suleiman Takadir Mwenyekiti wa Baraza la Wazee wa TANU, Sheikh Yusuf Badi wa Lindi, Sheikh Abdallah Rashid Sembe wa Tanga kwa kukutajia wachache.

Hii ndiyo sababu ya mimi kutafiti na kuandika kitabu cha Abdul Sykes.
 
Naomba ueleweshe umma wa watanzania ili tupate picha kamili
Hawa ndugu zetu walipigania uhuru walipigania uhuru kwa misingi ya dini? Au walishiriki kwa nia njema tupate uhuru?

Na kwa nini historia yao ifutwe?
 
Naomba ueleweshe umma wa watanzania ili tupate picha kamili
Hawa ndugu zetu walipigania uhuru walipigania uhuru kwa misingi ya dini? Au walishiriki kwa nia njema tupate uhuru?

Na kwa nini historia yao ifutwe?
Idu...
Labda ujiulize wewe mwenyewe.

Kimetokea nini nchi ikaaminishwa historia siyo?

Ukipata majibu hayo yaliyobakia yatakuwa mepesi kueleweka.
 
Idu...
Labda ujiulize wewe mwenyewe.

Kimetokea nini nchi ikaaminishwa historia siyo?

Ukipata majibu hayo yaliyobakia yatakuwa mepesi kueleweka.
Mzee Mohamed, kabla hatujapata ukweli halisi juu ya nchi kuaminishwa historia ambayo sio, tunatakiwa tujue ukweli. Je, hawa ndugu zetu ambao wengi walijitolea kupigania uhuru huku wakiwa na imani ya Kiislamu walipigania uhuru kwa misingi ya dini?

Mzee Mohamed pamoja kuwa unadai tumekaririshwa historia ambayo sio, lakini watanzania mpaka leo wanatambua ndio historia sahihi
 
Nakumbuka siku aliyomrithi mtangulizi na akiwa bosi wake Paulo Sozigwa ndiyo siku ambayo wanawake walianza kutangaza taarifa ya habari RTD.

Paulo Sozigwa hakutaka wanawake wasome taarifa ya habari.
 

Mkuu ulifundisha UDSM miaka gani na idara ipi? Just out of interest!
 
Nilifundisha engineering kuanzia 1987 hadi 1994; mimi siyo mtoto wa jana!

Nimeamini wewe sio wa jana ulifundisha na professors Awadh Mawenya na Silas Lwakabanba!!!!
Afadhali, vijana watambue kuwa humu wako na babu zao!!!
 
Nimeamini wewe sio wa jana ulifundisha na professors Awadh Mawenya na Silas Lwakabanba!!!!
Afadhali, vijana watambue kuwa humu wako na babu zao!!!
Lwakabamba alikuwa anafundisha Thermodynamics wakati Mawenya alikuwa anafundisha Foundation Engineering; Lwakabamba wakati anaondoka kwenda Nigeria ndiye aliyemwachia Masuha (RIP) nafasi ya kuwa Dean wa FoE.
 
Si utani,,,Maplatinum.......
Floppy disks....... 😂
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…