Mohamed Said
JF-Expert Member
- Nov 2, 2008
- 21,967
- 32,074
- Thread starter
- #41
Idu...Mzee Mohamed, kabla hatujapata ukweli halisi juu ya nchi kuaminishwa historia ambayo sio, tunatakiwa tujue ukweli. Je, hawa ndugu zetu ambao wengi walijitolea kupigania uhuru huku wakiwa na imani ya Kiislamu walipigania uhuru kwa misingi ya dini?
Mzee Mohamed pamoja kuwa unadai tumekaririshwa historia ambayo sio, lakini watanzania mpaka leo wanatambua ndio historia sahihi
Muhimu kwangu ilikuwa kuandika historia ya wazee wangu.
Hili nimelifanya na ukweli umejulikana.
Wasomaji wangu wengi sana wamejifunza mengi ambayo hawakuwa wanayajua kabla.
Kitabu cha Abdul Sykes kinanunuliwa sana na wanunuzi wangu karibu wote huanza hapa jamvini kwa kusikiliza mazungumzo yangu.
Baada ya hapo huenda kununua kitabu.
Naamini wewe ni mmoja wa wanafunzi wangu niliowasomesha historia hii.