sajo
JF-Expert Member
- Nov 8, 2010
- 3,474
- 6,195
Ndugu wanajukwaa salam, ama baada ya salam, niende moja kwa moja kwenye mada.
Niliwahi kusikia kurusha matangazo ya LIVE kwa nusu ni shilingi 4 million kunako TV (Japo sina uhakika kuhusu hiyo bei - ila point ya msingi ni kurusha matangazo LIVE via TV kwa saa ni gharama).
Sote tunafahamu vyobo vya habari vya serikali TBC na vya chama (Channel 10, Magic FM na Uhuru FM - CCM) vinapewa ruzuku kufanya hizo kazi za "kuiiongelea Serikali".
Lakini, hivi karibuni kumekuwa na wimbi kubwa kwa vyombo vya habari visivyo vya serikali kama AZAM MEDIA ( Azam tv na U-fm), WASAFI MEDIA (Wasafi fm na Wasafi Tv), CLOUDS MEDIA (Clouds FM and Clouds TV) na IPP MEDIA (EATV, EA Radio, ITV, Radio One, Capital Radio) na vinginevyo, kujihusishwa na urushaji wa matangazo mubarashara ya shughuli za chama (CCM) na serikali hasa Raisi akiwa katika ziara zake huko mikoani.
Pia, sasa hivi katika maombolezo ya Msiba wa Hayati Benjamin Mkapa pia naona nao wako mstari wa mbele katika kutoa matangazo ya huu msiba tena LIVE kwa siku kama ya nne mfululizo sasa.
Swali langu ni je, ni nani anagharamia hizo gharama kubwa na kufanya coverage za hizo LIVE? Na vipi mboona hakuna chombo hata kimoja cha habari kinarusha LIVE shughuli za wapinzani huko kwenye mikutano yao mikuu ya vyama vyao ya kupitisha wagombea wao hasa katika kipindi hiki cha uchaguzi?
Katika kesi ya ATTORNEY GENERAL AND TWO OTHERS v WALID KABOUROU (1996) TLR 156 Mahakama ya Rufaa ya Tanzania chini ya Jaji Mkuu Nyalali, na majaji wengine wawili, Kisanga (JJA) na Mfalila (JJA) ilifuta matokeo ya uchaguzi mdogo wa Ubunge wa jimbo la Kigoma mjini kwa sababu mbalimbali, moja ikiwa ni upendeleo wa chombo cha Taifa, Radio Tanzania Dar es Salaam (RTD) kumpendelea mgombea wa CCM kuliko wa vyama vingine katika kipindi cha uchaguzi.
Sehemu ya hukumu ilisema hivi, “RTD ni redio ya serikali, katika kufanya uchaguzi uwe wa haki, ilikuwa na wajibu wa kutoa muda sawa wa hewani kwa vyama vyote vya siasa na kuviacha viutumie vitakavyo. Mahakama imejiridhisha kuwa jambo hilo halikufanyika na hivyo CCM ilipata muda mwingi hewani kuliko vyama vingine, na hilo likachangia katika kukipa ushindi CCM.”
Tuliangalie sasa tangazo la RTD lililotumika kama sehemu ya ushahidi kuonesha upendeleo wake kwa CCM na mgombea wake, lilikuwa hivi,
“Ukweli wa kwanza na wa dhahiri kabisa ni kwamba CCM bado ni chama chenye nguvu kubwa sana na chenye wapenzi wengi walio wanachama na wasio wanachama. Tunasema CCM ina wapenzi ambao hata siyo wanachama wake kwa sababu kuna baadhi ya watu wanafanya makosa kwa kufikiria tu kuhusu namba ya wanachama wa CCM wenye kadi na kupiga hesabu zao zote za kisiasa kwa kuzingatia nambari hiyo ambayo haijafikia hata milioni tano.”
Likaendelea,
“Kosa jingine kubwa wanalofanya ni kudhani kwamba WATANZANIA wote wasio wana-CCM lazima watavipigia kura vyama vingine. Hiyo siyo kweli hata kidogo...., CCM tokea awali imekuwa chama cha Umma badala ya wateule wachache. Tena imekuwa na sera nzuri ambazo zimeitikia matakwa ya wananchi wote kwa wakati wote ambao imekuwa katika uongozi.”
Makosa hayo yaliyokatazwa na Mahakama ya Rufaa ya Tanzania miaka 25 iliyopita yanaendelea kufanywa na TBC na hivi sasa tayari wameanza tena, kwa kuanza kupiga kampeni za CCM kabla ya muda wa kampeni, kwa kuonesha mikutano ya chama LIVE na kucheza nyimbo za kuomba iaka 5 tena nk.