Nani anamdai Marehemu Lemutuz?

Nani anamdai Marehemu Lemutuz?

Pinto kafata taratibu za kiislam ambapo kabla marehemu hajazikwa ..anatakiwa mtu asimame na kuuliza Nani anamdai marehemu na nani anadaiwa na marehemu...
Le mutuz alikuwa na mikataba na DStv,Asas na kampuni zingine na kampuni yake alioajiri watu watano ...
Lazima kama kuna sintofaham ya Mali zake iwekwe wazi kabla hajazikwa
 
Kwahiyo ni lazima zisemwe hadharani vile,sio Kwa Wana familia?
 
Aisee nimemsikiliza yule kaka kanishangaza🤔
Hivi kulikuwa na haja gani ya kuongea Yale pale Kwenye kadamnasi?
Si angewafuata familia tu ?
Mpk nikaona Kuna watu km 3 hivi wanamfuata km walikuwa wanamnong'oneza aache kuongea hivi ,aisee kanishangaza sn
Halafu ni mtu mzima, alivyoanza ongea habari za sijui mtandaoni sijui gari, alafu yupo serious nikaona aibu kumsikiliza.
 
Walioweka utaratibu wa mtu kabla ya kuzikwa, kuorodhesha madeni na madai hawakukosea; kiubinadamu, bila huu utaratibu unaweza kuzungushwa na kuambiwa umejibambikizia madai na mwisho wa siku usipate stahiki.

Ndio maana ata bank, kama ulichukua mkopo na wewe muhusika ukafa, huwa hawasamehi deni, bali bima ndio itakayolipa deni n.k
Maisha ndivyo yalivyo.​
 
Huwa munampa sifa Sana huyo jamaa aliyekulia nyumba ya mboga nne ugali robo

Sijaona ushujaa wowote labda km watz ni wajinga , ushujaa wa kula bata mjini huku akiwa na back up ya mzee wake!!

Pia anatajwa kuwa ni Njagu msela ..

Acheni akina Malcolm X wabaki na ushujaa ..Bongo michosho Sana.
Embu mfwatilie vizuri.
 
hakuna kijana yeyote tanzania ambaye anaweza fanana na

Lemutuz​

Lemutuz​

jamaa ni shujaa ambaye hata story yake ya maisha naweza kuwa hadithia wanangu na nina hakika wataipenda

chukua maua yako Mkuu mungu akuweke mahali safi sana

Marehemu asemwi vibaya ila kusema ukwel mnampa maua ambayo hayamfai ..eti shujaa? Kwel kabisa kijana mwenye akili unaweza kumuita Le mutuz shujaa ? Shujaa kwa lip labda wakat tumeona ad nyumba aliyokuwa anakaa si kwake hata gari alilokuwa anahendesha sio lake … Ebu muachen marehem apumzike msije kutuchumisha zambi sisi
 
Ila kuna watu mna ungumbaru uliopitiliza. Sasa kichwa cha uzi unauliza nani anamdai le mutuz, afu kwenye habari yenyewe unamtaja anayemdai ambaye ni huyo pinto, hivi huko upstairs pako salama kweli? Au ndo bolts zinazoshikilia dish ziko loose?
 
Aisee nimemsikiliza yule kaka kanishangaza🤔
Hivi kulikuwa na haja gani ya kuongea Yale pale Kwenye kadamnasi?
Si angewafuata familia tu ?
Mpk nikaona Kuna watu km 3 hivi wanamfuata km walikuwa wanamnong'oneza aache kuongea hivi ,aisee kanishangaza sn
Mpaka wakamuondolea sauti kwenye kipaaza sauti Ila baadaye wakamrushishia. He spoke shit. Pinto popote ulipo hufai kuitwa mwanaume kabisa. Kwani hiyo Noah nzee kabisa ni shilingi ngapi? Hiyo nyumba aliyomwachia ndiyo ya kupanga Kariakoo? Yaani kumdhalilisha marehemu kuwa alikuwa dependant wa Pinto. Yaani mkuu Tayana-wog ningekuwa karibu ningemzaba Pinto Kofi la uso.
 
Aisee nimemsikiliza yule kaka kanishangaza🤔
Hivi kulikuwa na haja gani ya kuongea Yale pale Kwenye kadamnasi?
Si angewafuata familia tu ?
Mpk nikaona Kuna watu km 3 hivi wanamfuata km walikuwa wanamnong'oneza aache kuongea hivi ,aisee kanishangaza sn
Labda swali liliulizwa kwenye Kadamnasi na jibu lilihitajika kutolewa kwenye kadamnasi? Angelijibia wapi?
 
Aisee nimemsikiliza yule kaka kanishangaza🤔
Hivi kulikuwa na haja gani ya kuongea Yale pale Kwenye kadamnasi?
Si angewafuata familia tu ?
Mpk nikaona Kuna watu km 3 hivi wanamfuata km walikuwa wanamnong'oneza aache kuongea hivi ,aisee kanishangaza sn
Mbinu za kale kadada kenye mufupa, huyo kalipwa kumchgafua ila sisi tutamtetea. Kama kari akachukuwe duniani tunapita majumba na magari tunaacha. Yule baba ni mjinga tu mbona hakusema hayo yote lemutuzi akiwa hai?

Kama nyumba lemutuz alikuwa nayo kinyelezi, pesa ya kula alikuwa nayo.coz alikuwa na ofisi sasa hayo maneno yooote ya kazi gani? Ni ujinga tu hana lolote.

Am just saying you know northing personal, boma liwanza.
 
Huwa munampa sifa Sana huyo jamaa aliyekulia nyumba ya mboga nne ugali robo

Sijaona ushujaa wowote labda km watz ni wajinga , ushujaa wa kula bata mjini huku akiwa na back up ya mzee wake!!

Pia anatajwa kuwa ni Njagu msela ..

Acheni akina Malcolm X wabaki na ushujaa ..Bongo michosho Sana.
Njagu msela ndio nini mkuu?
 
Naona Wajane na Machawa wa Lemutuz wamekasirika kweri kweri [emoji1787][emoji1787] kulia kupokezana, kuishi kwa maigizo jua kifo kitakuumbua tu, kuna mmoja anauliza Noah shi ngapi ingekua rahisi si angemiliki yake [emoji1787] mwingine anasema hakuna kijana atakayeishi maisha ya Lemutuz kwanza tuwakumbushe alikua ni Mzee wa miaka 60+ hakua kijana, pili vijana sisi tuna akili tunawekeza kwa kidogo tunachopata gari na nyumba tutaviacha atleast hatutaaibishwa kwenye misiba kama huyo mzee wetu [emoji2960]

Continue to Rest in Heaven Milembe, at 40's umeacha Majumba na Magari na Mayatima uliokua unawasomesha na Walemavu uliokua unawatunza.
 
Kuna muda huwa tunapishana na wazee halafu ukute mzee Ni mtata na anamkwanja anaamua kukupitisha kwenye tanuru la Moto ,akili ikitulia anaamua kukuinua ,,,Le ni kama vijana wa mjini tu aliyeamua kuishi maisha yake na mzee malecela akaamua kumuacha apendavyo...Kuna upande wa simulizi hatukupata scene.
Kweli hatukupata scene lakini wewe binafsi ushaipata.
 
Amekula wapi mboga 4? [emoji28] Aisee laiti ungejua hata hayo maisha hajayaonja kaishi Kwa tabu usingesema!
Haya mambo yasikie tu aisee
kuna watu hamjui le Mutuz vizuri wakisikia jina la malecela (waziri mkuu mstaafu) basi wanaamini jamaa alikuwa mboga saba.

kumbe uhalisia wa jambo hauko hivyo.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Pinto amefanya la maana! Alikuwa anamsuta Mzee Malecela maana angemsaidia kijana wake akiwa hai. Sisi wazazi lazima tuwe na vifua vya kusamehe. Kama hatusamehi vijana wetu wakiwa hai, tusijifanye waungwana wanapokufa. Mtoto ni mtoto kwa mzazi wake ujue. Aibu ya Malecela kuhangaika na Watoto wa kufikia wa kipare na kusahau wako!
 
Pinto kafata taratibu za kiislam ambapo kabla marehemu hajazikwa ..anatakiwa mtu asimame na kuuliza Nani anamdai marehemu na nani anadaiwa na marehemu...
Le mutuz alikuwa na mikataba na DStv,Asas na kampuni zingine na kampuni yake alioajiri watu watano ...
Lazima kama kuna sintofaham ya Mali zake iwekwe wazi kabla hajazikwa
Naweka ukweli, Pinto alikuwa anasimulia

Sawa Kaka lkn ukweli ubaki kuwa mzee wake hukumuacha asote ,Le mwenyewe aliamuwa kuishi maisha aliyochagua ,,hawezi kufanana na Mimi niliyepambana kubomoa nyumba ya nyasi ya mzee wangu ili kumjengea yenye nafuu
Kwenye maisha ni virahisi kuona au kumuona mwingine kama mpuuzi fulani mpaka upitie magumu yake. Le Mutuz aliwahi kuandika ktk simulizi ya maisha yake kuwa kivuli cha ugomvi wa Mama zake wawili ndicho kilichokuwa kinamuandana maisha yake yote na mpaka kufikia kulelewa na dingi yake mkubwa na hilo tumelishuhudia ktk familia nyingi na familia yake haikuwa na tofauti.

By the way mkuu achana na kubomoa nyumba ya dingi yako na kuisimamisha upya. Je uliwahi kuishi na mama wa kambo akawa hakupendi kabisa halafu baba yako akashikwa akili na mama yako wa kambo?.
 
Back
Top Bottom