Nani anamkumbuka James Dandu (Cool James)?

Dandu!!!

Mke wake si ndiyo aliyekuwepo kwenye wimbo mmjoa wa Lady Jay dee?!
 
Kumbe uliishi Sinza?

Kipindi hicho miaka ya 2002 nilienda kushangaa nyumba ya Mrema. Baa ya delux (sijui inaandikwa hivi) kwa nyuma hivi ukipiga hatua kadhaa!

Nakumbuka nilidhani eneo hilo ndiyo mwisho wa mawingu. Nilitembea karibia na nyumba ya Mrema kwa mbele kidogo nikaamua kurudi nyumbani....muda mwengine utoto bhana!

Umenikumbusha vatican "disco toto" aisee! Nikipita njia karibia na hotel ya lion kwa nyuma kidogo ikiwa umenyooka na barabara kuu ya lami kulikuwa na bar ya Mangwea! Tulikuwa tunashangaa wasanii Prof. Jay, Noorah, Ferooz...tukitoka shule wale wenzangu na mimi tunaotembea kwa miguu kutoka shule ya SIA na Mashujaa. Aisee! Huu utoto bhana!
 
Miaka 18

Miaka 18 now kabaki mifupa tu huko chini
Nakumbuka 2005 sijui 2007 alikuwa anasoma shule ya Perfect vision alikuwa kituoni anasubiri usafiri kama sijasahau kituo cha Lego sijui mi nilikuwa kwenye usafiri mwengine kwa ghafla nikamkuta kituoni mi mwenyewe dogo kwa kipindi hicho ila nilimzidi umri nikajisemea yule si ndiye anayeigiza? mdomoni mwake kulikuwa na lollipop! Aluu alivyokuwa anainyonya! Nikawa najiuliza anaiona tamu sana au ni vipi?
 
Hahaha!

Naikumbuka hii nyimbo!
 
Yah Sinta kwa kizazi cha 90s mwishoni na 2000s mwanzoni alikuwa mkali.

Mkali hasa,hivi yupo wapi sasa?atakuwa amezeeka sasa
Sinta sa hivi ni HR Manager wa hospitali moja kubwa sana hapa Dar es Salaam.. Ni hospitali aliyojifungulia mke wa Majizo

Wapo wengi tu walishtuka mapema wakaongeza elimu na sa hivi wana mashavu makubwa tu ndo maana hawaonekani tena.
 
[emoji848][emoji848][emoji848][emoji848]
 
Amezaliwa 1992....Ila si unajua bongo muvi kwa ku_fake age!
 
Aisee kumbe nami muhenga… hivi miaka 18 imepita.. Hizi ngoma tulikuwa tunazicheza shule enzi hizo…
 
Aisee kumbe nami muhenga… hivi miaka 18 imepita.. Hizi ngoma tulikuwa tunazicheza shule enzi hizo…
 
Alitoa ngoma moja ilishika namba moja kwenye billboard kwa muda mrefu sana. Jamaa aliupeleka muziki wake kimataifa long time na ameomba na wasanii wakubwa muda mrefu sasa unakutana na hawa walamba midomo anasema ameupeleka muziki kimataifa unamuangalia unatamani kumkata makofi..
 
Huyu mwam
Huyu mwamba alitaka kuleta mapinduzi makubwa kwenye bongofleva,alitoka ulaya akaja nchini kuwekeza,lengo ilikuwa kuwainua wengine,naweza kusema kwa ujuzi wa mziki,na kuwa na mkwanja mrefu,ndio Diamond wa kipindi kile 2000,
Tofauti kubwa iliyopo na kina Mond wa leo,ni kwamba Hawa wasasa wanapiga hela ndeefu,wanamafanikio makubwa,lakini hawana nia Wala hawataki kuuinua mziki na wasanii wengine,wasasa wanapiga one man show,wawe na hela,Dunia iwatambue,wakifa leo,hawaachi chochote
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…