Nani anamuelewa Pastor Tony Kapola?

Kuna msichana mmoja anafanya kazi dukani kwangu. Lile duka liko mbali kidogo na lingine ambalo mara nyingi nakuwepo kumbe yule manzi kuna muda anafunga na kwenda kanisani mchana. Nilipojua nikamwambia achague kwenda kanisani au kufanya kazi na jibu nataka sasa hivi ili kama vipi tuachane kiroho safi. Naona hakuwa amezama sana akaamua kubaki kazini na upuuzi kaacha. Haya makanisa yana mchango mkubwa kwenye kuchochea umaskini.
 
Kuna wakati flani kwenye maisha yangu ya dhambi nilienda kwa mganga mida ya asubuhi sasa nikakuta mganga kama kachoka sana. Kumuuliza ndo akasema usiku mzima alikesha anahudumia wachungaji.
 
Nani anamfahamu vizuri pastor Tony kapola.

Kanisa lake liko wapi ?
Nilisikia liko morogoro kutwa yupo Dar,dodoma

Kwanini waumini wake na mke wanavaa nguo za ovyo ?

Inakuaje ameungana na hawa manabii wa uongo matapeli wa zimbabwe ?
ni wale wale tu. ukiona kuna nabii au mchungaji anahubiri hekima ya kibinadamu, huyo sio mchungaji, ni motivational speaker na asemacho hakitoki kwa Mungu. chochote cha kimwili hakiokoi roho. kama akili au hekima ya kidunia ingekuwa na uwezo kuokoa maprofessa na wasomi wengi wasingeenda church, na wachungaji wangekuwa ni wale tu waliosomea saikolojia kama kina chriss mauki n.k, na hao wanasaikolojia wasingekuwa na umuhimu wa kwenda church kwasababu saikolojia na elimu ya kimwili wanayo. ni kwa nguvu za Roho Mtakatifu pekee hata kwa tone moja tu mtu anaweza kubadilika, mtu aliyejazwa Roho Mtakatifu na anayeongea under the influence ya Roho Mtakatifu hata kwa kauli ya neno moja tu inapasua miamba ndani ya mioyo ya watu na wanabadilika ghafla. hao vijana wengi wanaotoa mahubiri ya sukari na wanaoongea kwa namna ya mwili ni wapiga pesa tu. wao wote pamoja na baba yao nabii.
 
Unaweza kunitajia manabii wa ukweli?
Manabii na mitume wa ukweli waliishia pale Bible ilipofika mwisho wa kuandikwa the rest ni wezi,matapeli,wahuni,wenye tamaa ya vitu vya dunia taja na mengine unayoyajua wewe.

Watu wanafanyiwa maigizo hawaelewi,Mungu alikuwa hana sababu ya kuweka mlemavu kama siyo kwa ajili ya kuwajaribu wale aliowapa viungo vyote,mf,kipofu yupo ili mimi mwenye macho yanayoona vizuri nimsaidie kula pale asipoweza kutafuta kula yake kama mimi au nimsaidie pale anapohangaika kufanya kitu eg;kuvuka barabara au kumuepusha na mashimo na kupitia haya napata thwawabu nisipofanya haya napata dhambi lakini anatokea kijana mmoja mvaa suit na mawani ya jua kwa sababu anajua kucheza na maandiko anamleta kwenye banda lake la mabati mtu anaefanana na huyu akiwa tayari ameshampanga namna ya ku-act na kusema "nguvu zake za kinabii zimempa uoni" watu na akili zao wanashangilia wanaenda kutoa shukrani ya hela wakidhani ni kweli.

Yaani watu wanapingana na jinsi Mungu alivyoipanga dunia,maskini Mungu amewaweka ili dunia iwe balanced na kupitia wao watu wafike kwake ila waokota sadaka so called prophet wanaita umaskini ni laana huku wakiwaambia hao maskini wawape sadaka (na hao maskini wanatoa hawajui kama hao wanaowaita walaaniwa ilibidi wapokee kutoka kwao).

Wengine wanafikia hatua ku-act kufufua maiti,Mungu mwenyewe alimuonyesha mwanadamu pale alipokaa katikati yake akijifanya mtu kupitia Yesu kwamba baada ya mishe zote duniani kuna kifo lakini leo mtu anasema amefufua mfu huyu ni nani anapingana na Mungu?wakipewa homework waende Muhimbili au Ocean Road kwenye wagonjwa wa ukweli wanaingilia huku wanatokea huku mbona huko hawathubutu kwenda kuonyesha unabii wao?


Mtaibiwa sana.
 
huyu shetani anakoelekea sasa ni mbali, anaona kama watanzania ni wajinga anaweza kuwafanya chochote. ifike mahali sasa kama nchi tusema enough is enough.
 
Kizazi cha nyoka kinapingana na injili ya kristo. Haha haha haha hahah hahah hahah halafu wanajiona wanauliza maswali ya hekima kumbe ni upumbavu machoni kwa Mungu.
Hahaha haha haha haha haha
Injili ipi? Hii ya mahubili ya utoaji
 
Akiangalia mavazi atasali mwenyew na mke wake then nani atalipa bills za kuendesha kanisa
 
Ni Kama mwakasege hawana tofauti
Hapana asee, kwa mwakasege nitapinga mpaka dakika ya mwisho, yule mzee naanza kumfahamu tangu anahubiri pale kwenye kiwanja cha shule ya Arusha meru secondary, baadae akahamia pale relini

Tafuta mfano mwingine hata wakina mzee wa upako lusekelo πŸ˜†πŸΊπŸ»
 
huyu shetani anakoelekea sasa ni mbali, anaona kama watanzania ni wajinga anaweza kuwafanya chochote. ifike mahali sasa kama nchi tusema enough is enough.
Nchi haina kipimo Cha kupima usahili wa Imani,Imani ni jambo binafsi
 
Ya sirini yaache yalivyo utaelewa kwann sedekia alitangulia
 
Kila penye feki original ipo.
Mitume na manabii wa kweli wapo wengi tu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…