Manabii na mitume wa ukweli waliishia pale Bible ilipofika mwisho wa kuandikwa the rest ni wezi,matapeli,wahuni,wenye tamaa ya vitu vya dunia taja na mengine unayoyajua wewe.
Watu wanafanyiwa maigizo hawaelewi,Mungu alikuwa hana sababu ya kuweka mlemavu kama siyo kwa ajili ya kuwajaribu wale aliowapa viungo vyote,mf,kipofu yupo ili mimi mwenye macho yanayoona vizuri nimsaidie kula pale asipoweza kutafuta kula yake kama mimi au nimsaidie pale anapohangaika kufanya kitu eg;kuvuka barabara au kumuepusha na mashimo lakini anatokea kijana mmoja mvaa suit na mawani ya jua kwa sababu anajua kucheza na maandiko anamleta kwenye banda lake la mabati mtu kama huyu na kusema "nguvu zake za kinabii zimempa uoni" watu na akili zao wanashangilia.
Yaani watu wanapingana na jinsi Mungu alivyoipanga dunia,maskini Mungu amewaweka ili dunia iwe balanced na kupitia wao watu wafike kwake ila waokota sadaka so called prophet wanaita umaskini ni laana huku wakiwaambia hao maskini wawape sadaka (na wao maskini wanatoa hawajui kama hao wanaowaita walaaniwa ilibidi wapokee kutoka kwao).
Wengine wanafikia hatua ku-act kufufua maiti,Mungu mwenyewe alimuonyesha mwanadamu pale alipokaa katikati yake akijifanya mtu kupitia Yesu kwamba baada ya mishe zote duniani kuna kifo lakini leo mtu anasema amefufua mfu huyu ni nani anapingana na Mungu?wakipewa homework waende Muhimbili au Ocean Road kwenye wagonjwa wa ukweli wanaingilia huku wanatokea huku mbona huko hawathubutu kwenda kuonyesha unabii wao?
Mtaibiwa sana.