Nani anastahili tuzo ya Nobel katika marais 6 tuliowahi kuwa nao Tanzania?

Jk
 
Ni J K Nyerere tu ndiye angestahili kuipata hata kabla ya Nelson Mandela ila hakupata kutokana na msimamo wake dhidi ya ukoloni na ukoloni mamboleo. Kilichomkosesha hiyo tuzo ni namna alivyosimama kidete dhidi ya ubaguzi wa SA mwaka 1960, msimamo wake dhidi ya Ian Smith wa kujitangazia uhuru wa Southern Rhodesia mwaka 1967 na finally kuunga mkono harakati za ukombozi wa nchi za Kusini mwa Afrika kupitia Frontline Satates.

Kimsingi JK Nyerere ndiye aliyemuunda Nelson Mandela mwaka 1964 alipompatia passport ya Tanzania na jina la Kitanzania ili aweze kusafiri nje ya Afrika Kusini kwenda kukutana na viongozi wa OAU akina Sekou Toure, Kwame Nkrumah, Haile Selassie, Kenneth Kaunda etc. Mapambano ya ANC dhidi ya ubaguzi yalianzia hapo kwa Zambia kutoa Makao Makuu na Tanzania kutoa kambi za wakimbizi na mafunzo. Huku Libya, Nigeria na Ethiopia wakitoa fedha
 
Hii migogoro ya majirani, karibu kila rais wa Tz ameshiriki utatuzi wake pale alipoingia Ikulu labda isipokuwa Mzee Ruksa na SSH tu:-

1. Burundi imesuluhishwa na Mwl, Mkapa, Kikwete na Magufuli.

2. Kenya imesuluhishwa na Mkapa, Kikwete, Magufuli na Mwl Nyerere enzi zile za MWAKENYA ambapo kundi la Raila lilituhumiwa kutaka kumpindua Moi 1980 likiwa na madai 21 dhidi ya utawala wa KANU. Mwl ndiyo alimpa Raila hati ya safari ya Tz kwenda UN na UN kumpa hati ya safari ya nchi zote duniani isipokuwa Kenya.

3. DR Congo imesuluhishwa na Mkapa, Kikwete, Magufuli.

4. Comoros imesuluhishwa na Kikwete, Mkapa na Nyerere kupitia SADC.

5. Rwanda ilisuluhishwa na Mkapa, Kikwete kupitia mwamvuli wa EAC na GLR.

So hii sifa ya usuluhishi ni standard kwa safu ya marais hao wa Tz except Mwinyi na SSH ambaye huenda kama atapenda atasuluhisha Kenya 2022.
 
Nyerere the unsung hero who made Africa.

Alimshauri Sam Nujoma kusafiri kwa punda toka Namibia kupitia Kalahari (Trans Kalahari) kama mbinu ya kivita ya kumkwepa Mreno hadi Mbeya ikamchukuwa miezi porini, ndipo Mwl akampa pasi ya kidiplomasia ya safari ya Tz kwenda kuhutubia/kumshitaki Mreno UN.
 
1. Commoro ni kisiwa kisicho na jina katika uso wa dunia, hakina maslahi makubwa kwa wazungu na sehemu kubwa ya dunia
2. Uasi wa Congo ni zaidi ya waasi wa M23, matatizo ya DRC hayatakaa yaweze kutatuliwa na mtu wa nje, ni uongo kusema JK ameleta amani Congo, Congo bado ina vikundi vingi vya uasis
3. Watu wazito katika utatuzi wa Mgogoro wa Kenya walikuwa ni Pamoja na Obasanjo ambaye alikuwa mjumbe maalum wa UN, Koffi Annan, Mkapa na Condeleza Rice, JK alikuwa ni sehemu ya timu tu.
4.Mgogoro wa Madagascar haujawahi kutatuliwa hadi leo aliyefanya mapinduzi ya umma bado ni Rais mpaka leo, mapinduzi ni kitu cha kawaida katika historia ya Madagascar, mwaka huu kuna General amekamatwa kwa tuhuma za kutaka kumuua Rais wao.
5.Hakuna mtu anayeweza kuthamini Kurudishwa madarakani kwa Nkurunziza ambaye alikuwa dikteta katili.
 
Kwenye demokrasia Imara Jecha asingefanya kile alichofanya wala dola haiwezi kutumika kukiwezesha chama kuendelea kubaki madarakani.Uchaguzi wa 2015 ilishuhudiwa rasimali za dola zikutumika sawa sawa upande wa chama kimoja.
Demokrasia chini ya Kikwete ilikuwa Strong.
 
Mkuu Yoda Nakupongeza kwa kuwa umeliweka vizuri. Kwenye hoja ya mtoa mada kumuingiza JK kama candidate ni ukosefu wa uelewa. JK ni WA kawaida sana, huyu ni wa kupewa hizo PhD za UDOM tu
 
Kwenye demokrasia Imara Jecha asingefanya kile alichofanya wala dola haiwezi kutumika kukiwezesha chama kuendelea kubaki madarakani.Uchaguzi wa 2015 ilishuhudiwa rasimali za dola zikutumika sawa sawa upande wa chama kimoja.
Ninaongelea kwa Standard zetu, Kikwete alikuwa mpenda Demokrasia kuliko Maraisi wengine.
 
Kumbe unasema kweli, wachina wanaenzi sana mawazo ya Nyerere, sis tunayakanyaga

 
Ninaongelea kwa Standard zetu, Kikwete alikuwa mpenda Demokrasia kuliko Maraisi wengine.
Inawezekana hujui maana halisi ya "demokrasi", unachukulia kuwa kuwa kuwavumilia wanaovunja sheria ndiyo demokrasi. Kikwete alikabidhiwa ripoti ya Katiba mpya mwaka mwaka 2013, alifanya nini kwa kipindi cha miaka miwili yote aliyokuwa nayo?
 
Bila kupepesa macho Wala maneno na tukiweka pembeni michuki chuki
Mh.KIKWETE anastahili
 
Ulichoandika ni kweli kwa maana zote ninazofahamu. Yote hayo uliyoandika yalifanyika reactively kwa kuombwa, siyo proactively. Failure ya kutokuwa proactive kwa matatizo ya jamii ndiyo inayomnyima sifa!, ambayo ni tofauti kabisa na Nyerere
 
Sir George Kahama (RIP).
 
Ulichoandika ni kweli kwa maana zote ninazofahamu. Yote hayo uliyoandika yalifanyika reactively kwa kuombwa, siyo proactively. Failure ya kutokuwa proactive kwa matatizo ya jamii ndiyo inayomnyima sifa!, ambayo ni tofauti kabisa na Nyerere
Sasa hapa umeandika kichekesho.

Sasa umetambua kuwa alifanya vitu vizuri tofauti na mwanzo ulivyodai kuwa hakufanya kitu ila tu eti alikula nchi, lakini unabadili magoli sasa baada ya kuonyeshwa evidence kuwa kweli alifanya mambo mazuri sana kwenye medani ya Amani barani Afrika, unadai oooh lakini kwa kuombwa. Nonsense!

Alipoombwa angeweza kukataa!, so what!.
Na kwa nini utie pua kwenye shughuli za watu kama hawajaonyesha kukuhitaji?.

Ulitaka apeleke majeshi Anjuan Comoro bila kuombwa msaada na serikali husika, huo si ungekuwa ni uvamizi?.

Eti reactive vs proactive, nonsense hata Nyerere hakua chizi kujipeleka kimbelembele kwenye ishu za wengine bila wenye shida zao kuhitaji msaada wake, angekuwa hivyo angekuwa bogus sana na kimbelembele.

You are a great hater wa JK.
 
All in all, JK ni WA kawaida sana, siyo wa kwenye Nobel prize. Huyu mpeni ma PhD ya heshima tu
 
All in all, JK ni WA kawaida sana, siyo wa kwenye Nobel prize. Huyu mpeni ma PhD ya heshima tu
unamuona wa kawaida, si ni kwa sababu ni mswahili mtu wa pwani, umezoea kumuona akitabasamu sana LAKINI mambo yake kwenye medani ya diplomasia na Amani barani Afrika ni makubwa.

Koffi Annaan na Mzee Mkapa walishafeli kwenye mediation yao huko Kenya, yaani mchakato wao ulishastall. Alipoingia JK kwenye hiyo process, mambo yalikwenda kama kumsukuma mlevi, Amani ikapatikana. Sasa unadhani huyo ni mtu wa mchezomchezo?

JK ni kichwa smart sana ambacho haters wanakichukulia poa
 
Nje ya mada. Atakayeleta Katiba mpya
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…