Nani anastahili Tuzo za Mhamasishaji Bora Ligi Kuu?

Nani anastahili Tuzo za Mhamasishaji Bora Ligi Kuu?

Tff na bodi ya ligi wanajichanganya sana, haiwezekani timu inayosemekana ndio iliingiza washabiki wengi mhamasishajiwa wao akosekane kwenye 3 bora, inavyoonekana tuzo wameshapanga wampe nani tangu zamani.
Tff na bodi ni kichefu chefu kwakweli, wengi wao ni watu wa maslahi binafsi sana.
Labda waneona kuingia kwa mashabiki wa yanga sana uwanjani hakutokani na hamasa za Nugaz Bali ni uzalendo wa wananchi wenyewe
 
Labda waneona kuingia kwa mashabiki wa yanga sana uwanjani hakutokani na hamasa za Nugaz Bali ni uzalendo wa wananchi wenyewe
Sio kweli, Nugaz kafanya kazi kubwa sana kuhamasisha watu, amefungua matawi mengi nchi nzima, amezungu mikoani, wilayani, mpaka katani kuhamasisha na kufungua matawi.
 
Sio kweli, Nugaz kafanya kazi kubwa sana kuhamasisha watu, amefungua matawi mengi nchi nzima, amezungu mikoani, wilayani, mpaka katani kuhamasisha na kufungua matawi.
Je kabla ya Nugaz kufungua matawi hayo usemayo miaka minne iliyopita yanga walikuwa hawajazi viwanjani?
 
Masau Bwire is the best! Anaongea with facts, anakupa all details na anaongea kwa hamasa.

Kwa Tanzania sijaona msemaji wa kufikia viwango vyake.
 
TFF wanachekesha sana bongo zozo hahahahahah
 
Mhamasishaji Bora kwa kiingereza anaitwaje. Shughuli zingine hazina kabisa maana ni njia watu wanajitungia tu pale wanapokuwa wamepigika kimaisha ili wapate pa kushika. Bure kabisa.
 
Je kabla ya Nugaz kufungua matawi hayo usemayo miaka minne iliyopita yanga walikuwa hawajazi viwanjani?
Mashabiki wa Yanga, hamasa ilishuka sana miaka ya katikati hapa, baada ya kuja GSM na Nugaz ndo hamasa ikaanza tena kurudi, kwa sapoti ya GSM ilimuwezesha Nugaz kuzunguka sehemu kubwa ya nchi kuhamasisha watu
 
TFF wameandaa tuzo na ambao wanagombea tuzo ya mhamasishaji bora wapo watatu.

1. Masau Bwire
2 .Haji Manara
3. Bongozozo

Mnaona nani anastahili hapo?
Mimi ni mshabiki na mwanachama wa simba ila jamaa Nugaz alipaswa kuwa kwenye hiyo orodha. Sioni mchango wa Zozo kwenye ligi yetu
 
Sasa timu iliyo ongoza kuingiza mashabiki msimu ulopita kwa mujibu wao aliekua mhamasishaji wao nae hayupo apo
 
Bongo zozo kwenye timu ya taifa sawa ila kwenye ligi tunamuonea kwa kweli walau popat
Sasa bongo zozo na ligi yetu wapi na wapi.....
Wachambuzi Uchwara wametoa taarifa ambazo SIO SAHIHI...

Hizi sio Tuzo za Ligi Kuu bali Tuzo za TFF!!

Unlike tuzo za miaka ya nyuma ambazo ndo hizo za Ligi Kuu, za mwaka huu zinahusisha hadi Ligi ya Wanawake, ya Azam na matukio mengine ya soka!!

Na hapo katika matukio mengine, ndipo inapoingia Taifa Stars ambayo Boli Zozo ni Mhamasishaji kwa upande huo!!!
 
Mashabiki wa Yanga, hamasa ilishuka sana miaka ya katikati hapa, baada ya kuja GSM na Nugaz ndo hamasa ikaanza tena kurudi, kwa sapoti ya GSM ilimuwezesha Nugaz kuzunguka sehemu kubwa ya nchi kuhamasisha watu
Na kauli yake Vimba mwananchi tembea kifua mbele
 
Mimi ni mshabiki na mwanachama wa simba ila jamaa Nugaz alipaswa kuwa kwenye hiyo orodha. Sioni mchango wa Zozo kwenye ligi yetu
Wangeshindanishwa Manara ,nugaz na masau bwire kwenye hicho kipengele ,Ila bongo zozo kwa vile anahamasisha kwa upande wa taifa stars angepewa tu tuzo ya heshima siyo ya kushindania ,maana kwa hamasa ya taifa stars bongo zozo amehamasisha sana na kwenda kila nchi wanayoenda taifa stars kwa nauli yake mwenyewe huku ameshika bendera ,hao wengine wangepigiwa kura Ila bongo zozo apewe tuzo ya heshima kwa upande wa taifa stars
 
Sasa timu iliyo ongoza kuingiza mashabiki msimu ulopita kwa mujibu wao aliekua mhamasishaji wao nae hayupo apo
Jamaa kahamasisha Simba ,akakimbia kuwahi tuzo akahamasisha na upande wa yanga ,kajitahidi
 
TFF wameandaa tuzo na ambao wanagombea tuzo ya mhamasishaji bora wapo watatu.

1. Masau Bwire
2 .Haji Manara
3. Bongozozo

Mnaona nani anastahili hapo?
Hawajamtendea haki nugaz kwa kutum nominated ila pamoja na yoote Mimi simba ila domo LA manara linastahili hio sifa.
Sema bwire anahitaji awepo simba amfunge bakuli manara
 
Back
Top Bottom