Nani Anawadharau WCB?

Sasa hio siyo tatizo la entertainment industry bali ni tatizo la serikali yako kutotengeneza mfumo rasmi wa kuwafanya hao vijana walipe kodi. Na hata kama hawalipi kodi ya paye hao vijana bado vipato wanavitumia kununua bidhaa amabzo zina VAT ambayo nayo ni kodi kwa serikali. Bado wanapata vipato ambavyo vinawafanya wasiwe tegemezi na kuwa mzigo kwa familia maana Afrika hatuendelei kwakuwa unakuta mtu ana ajira lakini ana mzigo wa watu tegemezi wengi.
Kuna TBC radio ndiyo kazi yake hizi redio ni redio za watu binafsi na zimeanzishwa kwa marengo tofauti usiforce mambo. Halafu wewe hapo zaidi ya kulalamika umefanya nini kati ya hayo unayosema ili wengine waige? Au wewe hufai kufanya hayo inabidi wafanye wengine?
 
Hivi huu upuuzi wa matamasha kwa nini badala ya matamasha ifnyike harambee kwa ajili ya kuchangie elimu na afya?.inasikitisha serikali bado inavumilia huu upuuzi wa matamasha.
Kodi zetu zifanye kazi gani sasa..
 
K
Kukusanya wajinga kwenye matamasha yanayopiga nyimbo za mapenzi tu ndio taaluma ?
Ndiyo burudani yenyewe hiyo hao vijana uzuri hawaja kuomba kiingilio ina maana wamefanya kazi mwisho wakalipa kiingilio kurelax. Wewe umefanya nini mbona hujaanzisha redio au harambee ya kuchangia elimu uko hapa unalalamika wengine waanzishe? Toka nje ya box fikiria kwa upana hiki kiwanda cha michezo na burudani ni kiwanda chenye uwigo mpanda kinaajiri vijana na watu wengi na ni kiwinda ambacho kikisimamiwa vizuri na kusaidiwa na serikali itapata mapato mengi na watu wengi watabadirisha maisha. Entertainment industry kwa nchi za wenzetu inaingiza ela nyingi sana, music, hollywood, NBA, ligi ya american football, hata wachina now wamewekeza sana kwenye michezo na burudani huko kwao.
watu wote hawawezi kuwa wanasheria, wahasibu, madaktari nakadhalika hiyo haiwezekani hata kale ndiyo maana watu wote walikuwa hawawezi kuwa wanajeshi, watawala kulikuwa na wahunzi wachuzi n.k.
 
Si jukumu langu kukueleza nimefanya nini bali ni jukumu langu kukemea uovu wote unaofanywa na haya matamashi kwa kisingizio kuwa ni burudani ,burudani gani hiyo asilimia tisini nyimbo ni za matumsi tu?
 
Si jukumu langu kukueleza nimefanya nini bali ni jukumu langu kukemea uovu wote unaofanywa na haya matamashi kwa kisingizio kuwa ni burudani ,burudani gani hiyo asilimia tisini nyimbo ni za matumsi tu?
Sasa kama siyo jukumu lako kutueleza ulichofanya basi siyo jukumu lao kufanya harambee za elimu. Fanya wewe burudani waachie wafanye wao siku wakijisikia kuhamia kwenye elimu watahama usipangie watu vya kufanya maana hawajakuomba mchango wakat wa kufanya hivyo.
 
Lazimq Lazima utakuwa na tatizo la akili si bure,hivi unawezaje kufananisha entertaiment industry ya usa na ya Tanzania?ulishawahi hudhuria tamasha hapa USA ?
 
Lazimq
Lazima utakuwa na tatizo la akili si bure,hivi unawezaje kufananisha entertaiment industry ya usa na ya Tanzania?ulishawahi hudhuria tamasha hapa USA ?
Wewe ndiyo una tatizo ndiyo maana nimekwambia ni kazi ya serikali kuijengea entertainment industry ya Tanzania mfumo rasmi ili hao waliomo walipe kodi, huwezi kulipa kodi kama serikali haijakudai hiyo kodi. Na narudia vipato vyao wanavitumia kununua bidhaa na huduma ambazo zina VAT bado serikali inanasa kodi toka kwao kwa upande mwingine japo inakosa PAYE. Halafu kwa kuongeza ni kwamba kuna wasanii wanalipa kodi hiyo ya PAYE mfano diamond juzi alisema akipiga show akalipwa 170 million TRA hawakosi kodi ya 48 mls na aliandika wakati ana waadress BASATA na TRA hawakupinga hilo.
Hata hiyo entertainment industry ya Marekani haikuanza vuup ikawa ilipo kwa sasa ilianza taratibu na mfumo ukajengwa na serikali sasa wewe na akili yako ya kwenye box unawaza kufunga tu huo unaitwa uzwazwa na kuona kwa urefu wa pua yako.
 
Hivi huu upuuzi wa matamasha kwa nini badala ya matamasha ifnyike harambee kwa ajili ya kuchangie elimu na afya?.inasikitisha serikali bado inavumilia huu upuuzi wa matamasha.
Wewe umechangia shingapi kwenye elimu na afya?
 
Haya matamasha yapigwe marufuku kwa maana hayajengi kizazi kijacho bali ni kubomoa kizazi kuanzia fikra hadi maadlili
mbona wanajenga steji za kufanyia matamasha ?
 
WCF na bosi wao waache kudhalilisha wanawake.
 
Mnaishi kwa kiki,zimeisha hadi mmeanza kumtumia dudu baya,kufananisha wasafi na clouds ni umama,wasafi ndo wanaanza safari,clouds ni habari nyingine
Huna jipya zaidi ya chuki ...
 
Wasifi + Clouds = baba mmoja, mama mmoja
Wanajua kucheza na akili zetu hawa wanatengeneza hela tuu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…