Nani anayekagua na kudhibiti ofisi ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali(CAG)?

Kwa kukusaidi budget waliopatiwa ilikuwa ndogo kuliko waliomba na hivyo kupelekea ukaguzi kufanyika katika taasisi chache. Kwa maana hiyo unaweza ukaenda kuwakagua na ukakuta bado wamabakiza hata hicho kidogo walichopewa.
Chamsinga omba kwa mwaka unaokuja wa fedha wapewe nyingi ili waweze kukagua sehemu nyngi zaidi kama si zote.
Emu pitia kidogo ripoti uone mavitu ya Muhimbili, na ndo maana sasa naelewa kwa nini wale wa ndiyo mzee walikuwa wanatumia nguvu kubwa sana kujaribu kuzunguka mbuyu.
 
...external auditor wapo wengi tu
Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mkuu Hoja Yangu Haingalii Kwamba Amepewa Kiasi Gani Ninachotaka Kujua Kama Mwananchi Wa Kawaida Ni Matumizi Sahihi Ya Umma Ndani Ya Ofisi Yake Basi au Kaka Kwani Hata Ww hautaki Kujua Matumizi Yanavyotumika Ndani Ya Ofisi Hii Ya CAG?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
CAG hukaguliwa na kampuni binafsi na report hupelekwa kamati ya Bunge PAC
 
Naona mnajipanga kujibu mapigo ya CAG! kudadadeki mmetafuna na kumeza wembe
 
Swali gani hilo? Lini ulisikia Wadudu wanaosababisha Malaria wameugua Malaria?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Wafanye ukaguzi ili wavumbue nini

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kwanza naomba uelewe kuwa CAG ni sawa na neno Rais.

Swali lako ni sawa na kusema nani huwa anaikagua ofisi ya Rais?

Jibu ni kuwa, Mkaguzi anayekagua hesabu za Ofisi ya CAG anatoka kwenye makampuni binafsi ya ukaguzi (Private Audit Firms) inayotambuliwa kisheria na Bodi ya Taifa ya Wahasibu na Wakaguzi (NBAA) ambaye atachaguliwa na Kamati ya bunge ya Hesabu za Serikali kuu ( PAC).

Hii ni kwa mujibu wa Sheria ya Ukaguzi wa Umma Na. 11 ya mwaka 2008 Kifungu 46 (1-6)
 
Hata huyo anaemkagua nae atahitaji kukaguliwa.hiyo itakuw ni endless process km rocky cycle.
Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ukiona hivyo ujue ma ccm yanataka kujenga hoja na kuweka zengwe ofisi ya NOAT
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…