Kwenye Ukaguzi huwa wanakagua ( NAO) National Audit Office sio CAG kwa Kuwa CAG Ni top wa NAO
Ukaguzi huo hufanywa Na Independent Audit firm
N.B CAG Kwenye ofisi yake imehakikishwa hana majukumu yoyote ya kiutawala Kama vile kudhinisha malipo, kushiriki Michakato ya zabuni Na Mengineyo ya namna hiyo ili kuhakikisha Mara zote hahusiswi Na makando kando Mengine kwa Kuwa Maadui wa kazi zake wanaweza kutumia huo mwanya kumchomekea kashfa
2016 Baada ya Ukaguzi wa MV Dsm report yake kutoka Gazeti la Mtanzania lilianzisha uzushi dhidi ya Prof Assad Kuwa kanunua gari la ofisi yake bila ya kufuata Taratibu Za Manunuzi Na kashfa hiyo ika trend Sana Kwenye Mitandao baadae wakajulishwa Kuwa mipaka ya CAG Kwenye routine duties yoyote ya namna hiyo kwa namna yoyote ile CAG binafsi huwa hahusiki kabisa Hata kwa ushauri Basi ile kashfa ikafa ghafla kwa Kuwa ilitengenezwa kumchafua Assad Na hawakutaka kuendelea nayo kwa Kuwa Huenda ingewakumba wale ambao hawakukusudiwa
Likaja Suala la kwenda Hijja kwa Fedha Za Ofisi kwa Kuwa tu waliona anaomba Kibali Cha kusafiri toka Jumba jeupe bila ya kujua kwa utaratibu wa utumishi Hata ukiwa Likizo Na unaenda nje kwa mambo yako binafsi Na kwa gharama zako Basi kuomba Kibali Cha Ruhusa ni lazima
Nchi yetu Bado changa Sana kumudu Kuwa Na CAG wa Viwango vya Mussa Assad, Kama vipi tupewe Kazi ya kupita pita Udsm , Mzumbe Na Udom tunaweza kupata Prof wa Accounting anae fanana na kasi yetu Na wapo wengi Sana
Mfano;
Wakati wa awamu ya Nne ukitaka Mtaalam wa kukueleza Ubovu wa Katiba iliyopo alikuwa Prof Palamagamba Kabudi
Wakati wa awamu ya Tano ukitaka Mtaalam wa kukueleza ubora wa Katiba iliyopo Basi ni Yule Yule Prof Palamagamba Kabudi