Wakuu, sisi wakazi wa Kaskazini ambao tunaishi huku, tunaweza kukuambia majimbo ambayo Chadema inaweza kupoteza. Na kitu kingine kipya ni hali ya uchangamfu na ushabiki umepungua sana 2020. Kipindi kama hichi cha uchaguzi 2015 ukitembelea huku ilikuwa unajua Nchi inakwenda Upinzani.
Ushabiki wa kwetu Kaskazini ni wa wazi hauna kificho, iwe sokoni, Baa, kilabu cha pombe za kienyeji, mashambani, kanisani na popote penye mkusanyiko wa watu.
Na usidanganywe na mtuu yeyote, kuna hali fulani ya kusema ngoja tupigie CCM tuone labda kuna matunda. Hii ndio hali haklisi ila kuna majimbo au jimbo linalo weza kubaki Chadema.
Nguvu ya upinzani imepungua sana huku Kaskazini yote, kuna hali ya kuona tukiendelea tutatengwa.
KINYUME NA HUU USHAHIDI NI KINYUME NA HALI HALISI LABDA KUJIPA MOYO.