Nani atakuwa Mgombea Mwenza wa Samia mwaka 2025?

Ninauhakika Ridhiwani Kikwete ananafasi nzuri na uzoefu wa ikulu.
 
anaongea kisauti chembamba utadhani siyo M/Raisi.

HANA USHAWISHI KIUFUPI HATA NIPTE ROAD NIONE KASIMAMA ANAONGEA NA WATU NITAENDELEA NA SHUGHULI ZANGU
 
Fact 100%
 
Munasemaga hicho cheo ni kama ceremonially tu sasa imekuwaje ??!! Atateuliwa tena huyo huyo na watashinda tu !! Kwanza kwani katiba mpya itakuwa tayari kabla ya 2025 ??!!
 

Unaongea pumba. Unasema kama vile wanasisa waongo ni bora kuliko watendaji. Tumshukuru sana Mpango kwa kusaidia sera za uchumi ambao unakuwa kwa kasi. Kuleta watu wa malumbano haisaidii
 
Mada nzuri sana , mada inayofikirisha na kutafarisha kidogo.
Umeiwasilisha kwa ufasaha na umakini sana .

Yote ya yote nadhani kwa Emannuel nchimbi kuna usfadhali kidogo, yuko mbali na up down za hapa bongo , maybe anaandaliwa kwa nafasi kubwa hapo mbeleni.
 
Umeandika vizuri na kutoa ushauri kwa chama chako angalau kiweze kujikongoja 2025(kama uchaguzi ukifanyiaka maana iko wazi no katiba mpya no uchaguzi hili lazima viongozi walijue na kulielewa)

Mbili ccm kama jina na chama sio shida ,shida ni waliomo ndani ya chama, kwa kuamini top 20 wanaojulikana ndo wenye uwezo wa kupeperusha bendela ya chama , ( nazingatia nafasi ambayo unaijadili katika uzi wako) huwa hakifanyi kwa sasa tafiti kwa kina bali wao huamini kwenye maono ya watu wachache top ,likipendekezwa jina top ten ikalikubali basi ili hali wanajua namna ya kucheza goli la mkono , ila kama sio hivyo

Kuna watu wana ccm wanao ushawishi na mvuto ambao wenda wapo chini serikalini au nje ya mfumo ila wanaweza msaidia mgombea wenu angalau kupata nusu ya kura kama sio robo tatu, maana siasa ni upepo

1. Kwa sasa katika bunge lenu la sasa na watu wako umewajadili katika uzi wako hakuna anaweza kuwa juu kisiasa kwa na kama akiendelea hivi
MBUNGE MPINA(akiendelea hivi anafaa)

2.mh AGGREy( mzee wa toronto) aliekua mkuu wa mkoa Tabora( mtacheka) ila iyo machine katulia tuli uyu hata mtoto mdogo anamjua tokana na machachari yake yenye utendaji mkubwa ndani yake

3.Mnaweka mbali familia ya Mw nyerere, kwa kuchafuana ila nawambia ,
Makongoro Nyerere sio mtu wa mchezo achilia mbali na utani mwingi anafaa sana pia nafasi iyo.

4 mh Mtaka ( uyu yuko juu kwenye jamii ya kitanzania kutokana na aina yake ya uongozi kama ni mvuto kwenye jamii upo)

NAISHIA HAPA BWANA CCM HAMNILIPI ila kwa list ulioitaja akichukuliwa mmoja mkifikisha robo ya kura katika uchaguzi huru na haki niite kuku niko pale
 
Kwani Katiba Inaruhusu Top Leaders wa dini mmoja
Yaan President na Vice Katika list yako hivi majaliwa anaweza gombea kama mwenza wa Samia ingali wote ni Misilims!??
 
Membe akae huko huko a.k joka la mdimu[emoji51]
 
Kwani Katiba Inaruhusu Top Leaders wa dini mmoja
Yaan President na Vice Katika list yako hivi majaliwa anaweza gombea kama mwenza wa Samia ingali wote ni Misilims!??
Hakuna kitu kama hicho
 
Uzuri ni kwamba ataprint form nyingi tutajichagulia tunayemtaka
 
Nyie ongeeni yooote andikeni yoote mala paaah ifikapo 2025 Doctor Musukuma kapewa nafasi ya kuiwakilisha ccm kugombea urais[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23].

Ccm hawashindwi kitu, na masuala ya siasa hakunaga kujiaminisha sana wao wenyewe hawaaminiani sana hivyo wanapokosa mgombea wa kutimiza agenda zao huona bora ashike nchi mtu yeyote yule ila asiguse ulaji wao[emoji23][emoji23][emoji23].

Ndio hapo mtakapoona Musukuma kawa rais, ndugai makamu wa rais, makonda waziri mkuu, yule jamaa musiba akiwa msemaji wa serikali, na yule jamaa yenu Ex mkuu wa wilaya ya hai akiwa kama kamanda mkuu wa majeshi kama sikosei[emoji23][emoji23][emoji23].

Mchungaji gwajima akiwa waziri wa nishati, mwigulu akitupwa sentro, majaliwa akitupwa nje ya siasa ama ubunge kuukosa kabisa[emoji16].

Mambo ya siasa tusiyaamini sana, huenda chini ya pazia kuna njama za kimapinduzi zinafanyika kuusuka uongozi mpya nje ya huu wa sasa[emoji23].

Maneno yangu si sheria kwamba lazima yawe ama yatokee lakn mark this comment, mambo yatakayokuja kuibuka ni kinyume na matarajio ya wengi humu[emoji23].

Sipatii picha wengi wa wanasiasa wataikimbia hii nchi maana kuna visasi vitalipwa ama baadhi ya wanasiasa kufa kwa presha maana matarajio yatakayoibuka ni zaidi ya yale ya 2015.
 
Huyo Antony mtaka ndo anayefaa, tunataka mtu mwenye umagufuli kidogo na hofu ya Mungu pia, mpina in mzuri ila anapiga kelele ili asogezewe buyu la asali tu, Mtaka na Dr.Hussein mwinyi ndo viongozi waliobaki hapa tz.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…