Nani atakuwa Mgombea Mwenza wa Samia mwaka 2025?

Mama Samia ataenda na BKM kama mchezo hautabadilika
 

Hoja hii nadhani asili yake ni wana mtandao -Msoga. Hawa wa Msoga ndio waliokuwa na wakina Membe kazi yao ikiwa kukusanya hela kwa GADAFFI na kuzificha DUBAI huku kila siku wakipishana juu kwa juu airport wakisafiri dunia nzima kufanya madili yao! Halafu leo ndio mnakuja kutoka kumsafisha kusema eti Membe anafaa kuwa mgombea mwenza; mtu asiyekuwa na msimamo wala intergrity!! Hana mvuto!

Nchimbi hana sifa nzuri kwani ni mla rushwa bingwa!! Alipokuwa akiongoza vijana ndio alihusika na ujenzi wa hilo jumba la Vijana Hapo upanga ; jumba hilo lilijengwa na Kampuni ya Esteem construction , kampuni ya ujenzi ya rafiki wa Kikwete Marehemu Shubaash Patel. Gharama za ujenzi wa jumba hilo zilikuwa OVERINVOICED na 10% ya malipo ikachukuliwa na huyu fisadi!!

Kassim Majaliwa hana charisma na sio mtendaji mzuri magico yake hayatekelezwi na wachini wake na Ndio maana migo unamuangukia Samia;ndio maana hata Jiwe alimwambia waziwazi kuwa asingekuwa Waziri Mkuu wa miaka kumi!!

The only person remaining standing na ambae hana uchafu na TRANSFORMATIVE leader ni current Njombe RC Anthony Mtaka!!
 
Mzee wa kutia wino mwekundu, aliharibu kwenda chama kile , na kujiaribia mvuto wa kisiasa aliokua nao

Vasco Dagama Ndio anataka kucheza karata hiyo ya Membe lakini lazıma wamzuie kwani ataiharibu nchi! Hiyo yote ni kumtengenezea njia mtoto wake Ridhwani!!!!
 
Bro hiv bado hujui kuwa rais anachaguliwa na wenye nchi? Kama Bado unaamini rais wa Tanzania anachaguliwa na wananchi aisee wewe bado sana.
Pili. Huyo makamu wa rais hakuchaguliwa na Mama yule alichaguliwa mahsusi kubalance Mambo. Coz kwanza alikuwa wazir wa fedha so that inshu yoyote inayohusiana na uharibifu wa pesa wakati wa Mh Magufuli ili umkamate yeyote wa serikali ile lazima uanzie na mpango so wazee waliballance kati ya Sukuma gang na msoga gang ili wasiumizane nchi ikaharibika.
3. Nchi hii kuna mhimili usiooneka kati ya kanisa katoliki na bakwata so aliwekwa mtu loyal kwa kanisa wakati wa bakwata yuko juu yake. Ndio hesabu za wenye nchi. Kupisha Mambo yaende. Huyo jamaa kama asingekuwa makamu wa raisi kuna watu wengi wangekamatwa niamin. Ndio maana ile ripoti ya uchunguz wa matumiz ya hela tangu mwez wa kwanza mpaka Mh.Magufuli anafariki 2021 waliizuia kuitoa pamoja na mkwara wote wa mama. Hii nchi ni zaid ya uijuavyo.
 
Makamu wa Rais wa sasa
 
Hii ni opinion yako inaheshimiwa. Ingawa hauko scientific! Unaposema Mhe. Rais hana nguvu za kisiasa Bara sijui unapima kwa evidence ipi? Mhe. Rais nguvu zake kisiasa zimo ndani ya CCM siyo kwa Mhe. Makamu wa Rais. Pili, unakiri Mhe. Rais alimteua Dk. Mpango amsaidie ikiwemo kukuza uchumi; jibu ni yes imelipa, uchumi unakua kwa kasi na umetulia. Mengine muda ukifika itakavyompendeza Rais ataamua. 🙏🙏🙏
 
Wewe bado mchanga kweli kwenye siasa za CCM na Tanganyika(kama ulivyosema wewe) kwa ujumla. Unamtaja Bashe, Bashungwa, Simbachawene kwenye nafasi ya VP?
 
Dr mpango siyo mchumi mahili kama inavyitaka kutuaminisha. Kuna mchumi Gani asiyejua hesabu. Mpango amesoma HGE which means hajui hesabu. Mchumi mahili ni aliyesoma EGM
 
Acha kupoteza muda, 2025 Mgombea wa CCM ni SSH na mgombea mwenza ni Dr. Phillip Mpango. Hayo mengine ni ramli
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…