Nani atalia Ukifa?

Nani atalia Ukifa?

Tujitahid tutende mema tnapokua hai.. na tuishi maisha ya kumtukuza Mungu!!
Watu wanasahau wafu haraka sana usiwajali sana... Nadhan kutenda mema kwa imani yako inapaswa iwe kipaumbele zaidi.

Apumzike kwa amani huyo kijana
Kabisa matendo yetu mema tutakayokumbukwa nayo yatafanya hata kizazi chetu hai kitachobaki kithaminiwe!
 
Wiki iliyopita Nikiwa katika shughuli zangu Jijini Dar es salaam napigiwa simu toka nyumbani, ujumbe ni kwamba Mshikaji wangu S Amefaiki (Mungu Amrehemu)
Ni msiba ulionistua sana hasa kwa sababu ni msiba wa mtu wangu wa karibu, kijana ambaye hata Miaka 30 hana, mke hana.. ndio maisha yalishamkalia Poa.. mtu aliyekuwa anamalizia kujenga, ana kausafiri kake na kazi nzuri.. Katika umri mdogo kama wake tayari alikuwa akipata shahada yake ya pili.. lakini amefariki!
Hii ni ishara kuwa kifo kipo muda wowote, tazama waliofariki ghafla ajali ya Mv Nyerere.. watu ghafla wanaondoka hawajajipanga, Naguswa sana na hii misiba, najiuliza nawe pia jiulize ghafla kifo kikakuta utakumbukwa kwa Mema yapi? Jambo lipi Jema litabaki juu ya jina lako!

Nikajikuta Nakumbuka Maneno ya Mtu anayeaminika Kuwa Miongoni mwa watu wenye akili nyingi kuwahi kutokea yaani Leornado Da Vinci, wakati wa kufa kwake aliwaomba watu na Mungu Radhi kwa Kutotumia uwezo aliopewa na Mungu kwa kadri ilivyostahili!

Tufanye Mema ya Kukumbukwa Maana Kifo Hutuchukua wakati wowote!

Rest in Peace Mwanangu Samson, Mungu Ailaze Roho yako Mahali Pema Peponi, Nakumbuka Nyakati zile tukifurahi Pamoja kwa Kucheza Draft!

Santana
Rip
 
Kaka kuna kufa kuacha kumbukumbu.

Nakuna kufa kuacha Historia.

Which one are you???.

Ukiacha kumbukumbu. Siku ukifa kuanzia mtoto mpaka wazee wa mitaani watalia sana.
 
Kwa kweli inahuzunisha pale ambapo unapotelewa mpendwa wako. cha msini ni kumuomba Mungu atusaidie kuishi maisha yaliyo mema ambayo yatawavutia na wengine watamani wawe kama mimi au wewe siku ya kifo
 
Lesson learnt bro naimani kuna kitu nitabadilisha pia maishani
 
siku ipo utaelewa, kumbukwa kwa mabaya uone hata kizazi chako kitakavyoteseka!
Mabaya na Mazuri yapo kwa kila binadamu.
Kila mtu atabeba dhambi zake, uovu wa baba haurithishwi kwa watoto.
Sio kila mtoto mwema na babaye alikuwa mwema na kinyume chake kwa mtoto mbaya.
La msingi ni kutubu mabaya uliyotenda ili Mungu akusamehe hayo mabaya na aku alike katika maisha ya milele katika ufalme wake.
Huyo atakaye kumbuka mabaya yako hawezi kuishi miaka mia mbili.
Kwa Mungu kuna maisha ya milele ambayo ni mazilioni ya miaka.
Mimi naona ni afadhali nichukiwe na binadamu wote, Ila nipendwe na Mungu.
 
Back
Top Bottom