Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Kabisa matendo yetu mema tutakayokumbukwa nayo yatafanya hata kizazi chetu hai kitachobaki kithaminiwe!Tujitahid tutende mema tnapokua hai.. na tuishi maisha ya kumtukuza Mungu!!
Watu wanasahau wafu haraka sana usiwajali sana... Nadhan kutenda mema kwa imani yako inapaswa iwe kipaumbele zaidi.
Apumzike kwa amani huyo kijana
Amina, tuiandae Njia yetu ambayo ni Moja!Naogopa kufa mm
Mungu wangu anipe mwisho ulio mwema tu nikiwaza kifo nguvu zinaniisha kuwa kifo changu sijui kitakuwaje yaani
Mungu ampumzishe kwa amani huyo kijana
Amina, tuiandae Njia yetu ambayo ni Moja!
RipWiki iliyopita Nikiwa katika shughuli zangu Jijini Dar es salaam napigiwa simu toka nyumbani, ujumbe ni kwamba Mshikaji wangu S Amefaiki (Mungu Amrehemu)
Ni msiba ulionistua sana hasa kwa sababu ni msiba wa mtu wangu wa karibu, kijana ambaye hata Miaka 30 hana, mke hana.. ndio maisha yalishamkalia Poa.. mtu aliyekuwa anamalizia kujenga, ana kausafiri kake na kazi nzuri.. Katika umri mdogo kama wake tayari alikuwa akipata shahada yake ya pili.. lakini amefariki!
Hii ni ishara kuwa kifo kipo muda wowote, tazama waliofariki ghafla ajali ya Mv Nyerere.. watu ghafla wanaondoka hawajajipanga, Naguswa sana na hii misiba, najiuliza nawe pia jiulize ghafla kifo kikakuta utakumbukwa kwa Mema yapi? Jambo lipi Jema litabaki juu ya jina lako!
Nikajikuta Nakumbuka Maneno ya Mtu anayeaminika Kuwa Miongoni mwa watu wenye akili nyingi kuwahi kutokea yaani Leornado Da Vinci, wakati wa kufa kwake aliwaomba watu na Mungu Radhi kwa Kutotumia uwezo aliopewa na Mungu kwa kadri ilivyostahili!
Tufanye Mema ya Kukumbukwa Maana Kifo Hutuchukua wakati wowote!
Rest in Peace Mwanangu Samson, Mungu Ailaze Roho yako Mahali Pema Peponi, Nakumbuka Nyakati zile tukifurahi Pamoja kwa Kucheza Draft!
Santana
Asante Kakapole sana mkuu
Mabaya na Mazuri yapo kwa kila binadamu.siku ipo utaelewa, kumbukwa kwa mabaya uone hata kizazi chako kitakavyoteseka!