Nani atalia Ukifa?

Nani atalia Ukifa?

Ctech

JF-Expert Member
Joined
Nov 21, 2010
Posts
754
Reaction score
818
Wiki iliyopita Nikiwa katika shughuli zangu Jijini Dar es salaam napigiwa simu toka nyumbani, ujumbe ni kwamba Mshikaji wangu S Amefaiki (Mungu Amrehemu)
Ni msiba ulionistua sana hasa kwa sababu ni msiba wa mtu wangu wa karibu, kijana ambaye hata Miaka 30 hana, mke hana.. ndio maisha yalishamkalia Poa.. mtu aliyekuwa anamalizia kujenga, ana kausafiri kake na kazi nzuri.. Katika umri mdogo kama wake tayari alikuwa akipata shahada yake ya pili.. lakini amefariki!
Hii ni ishara kuwa kifo kipo muda wowote, tazama waliofariki ghafla ajali ya Mv Nyerere.. watu ghafla wanaondoka hawajajipanga, Naguswa sana na hii misiba, najiuliza nawe pia jiulize ghafla kifo kikakuta utakumbukwa kwa Mema yapi? Jambo lipi Jema litabaki juu ya jina lako!

Nikajikuta Nakumbuka Maneno ya Mtu anayeaminika Kuwa Miongoni mwa watu wenye akili nyingi kuwahi kutokea yaani Leornado Da Vinci, wakati wa kufa kwake aliwaomba watu na Mungu Radhi kwa Kutotumia uwezo aliopewa na Mungu kwa kadri ilivyostahili!

Tufanye Mema ya Kukumbukwa Maana Kifo Hutuchukua wakati wowote!

Rest in Peace Mwanangu Samson, Mungu Ailaze Roho yako Mahali Pema Peponi, Nakumbuka Nyakati zile tukifurahi Pamoja kwa Kucheza Draft!

Santana
 
Kukumbukwa au kutokumbukwa hakukusaidii chochote kwako uliyekufa.
Kulia sio kuhuzunika, kuna kilio cha fulaha pia.
Cha msingi umejiandaaje kuishi maisha baada ya kifo.
Kukumbukwa na binadamu hakuta kusaidia kitu.
Pigania kukumbukwa na Mungu.
 
Dunia mapito utumie vizuri pumzi ulizopewa kwan hujui saa, siku, mwaka lin Itakuwa zamu yako na utakufa katika mazingira gan
 
Tujitahid tutende mema tnapokua hai.. na tuishi maisha ya kumtukuza Mungu!!
Watu wanasahau wafu haraka sana usiwajali sana... Nadhan kutenda mema kwa imani yako inapaswa iwe kipaumbele zaidi.

Apumzike kwa amani huyo kijana
 
Back
Top Bottom