Nani atasimamia utekelezaji ikiwa mamlaka zilizounda Tume ya kuchunguza matukio ya Oktoba 29 zitaguswa?

DodomaTZ

Senior Member
Joined
May 20, 2022
Posts
197
Reaction score
233
Hili ndilo swali linalobeba kiini cha wasiwasi wa wengi kuhusu hatima ya mapendekezo ya Tume. Suala si kutolewa kwa ripoti pekee, bali ni nani atasimamia utekelezaji wake endapo mapendekezo yatagusa mamlaka ya waliounda chombo hicho.

Hapa ndipo mjadala wa uwajibikaji unakuwa mzito zaidi, ambapo baadhi ya wananchi na wadau wanajiuliza iwapo mfumo unaweza kujichunguza na kujirekebisha bila usimamizi huru.

Inawezekana ripoti hiyo ikagusa mamlaka za uteuzi endapo uchunguzi utaonesha kuwa zinahusika? Je, Tume ina uwezo wa kueleza wazi endapo jambo hilo litajitokeza?

Na ikiwa itafanikiwa kufanya hivyo, wasiwasi unaweza kuibuka: je, taasisi zilezile zitabeba jukumu la kusimamia mabadiliko yanayozigusa? Eneo hili linaibua hofu ya mgongano wa maslahi.

Tukumbuke kuwa zimebakia siku chache kabla ya ripoti hiyo kutolewa baada ya kukamilika kwa muda wake. Licha ya kuwepo kwa ukosoaji dhidi ya muundo wa Tume hiyo, bado ripoti inaweza kuwa chanzo cha mijadala, bila kujali itakavyokuwa imewasilishwa.
 
Hiyo report ni virus ...usipoteze muda wako bure ROSTAM AZIZI NA GENGE LAKE AWAWEZI KUHUKUMIWA NA MAHAKAMA YOYOTE
 
Hivi mkuu, unafikiri Samia na viongozi hawajui ni kitu Gani kipo kwenye ripoti mpaka muda huu ?

Hiyo tume sio huru ...na wameshawaeleza tutasema hiki na hiki...na kama Kuna jambo la ukakasi wanaambiwa toa hii mada...

Mfano Madai ya Uchaguzi huru na haki au wizi wa kura..vitu kama hivi viongozi hawapendi kuvisikia masikioni
 
Hili ndilo swali linalobeba kiini cha wasiwasi wa wengi kuhusu hatima ya mapendekezo ya Tume. Suala si kutolewa kwa ripoti pekee, bali ni nani atasimamia utekelezaji wake endapo mapendekezo yatagusa mamlaka ya waliounda chombo hicho.

Hapa ndipo mjadala wa uwajibikaji unakuwa mzito zaidi, ambapo baadhi ya wananchi na wadau wanajiuliza iwapo mfumo unaweza kujichunguza na kujirekebisha bila usimamizi huru.

Inawezekana ripoti hiyo ikagusa mamlaka za uteuzi endapo uchunguzi utaonesha kuwa zinahusika? Je, Tume ina uwezo wa kueleza wazi endapo jambo hilo litajitokeza?

Na ikiwa itafanikiwa kufanya hivyo, wasiwasi unaweza kuibuka: je, taasisi zilezile zitabeba jukumu la kusimamia mabadiliko yanayozigusa? Eneo hili linaibua hofu ya mgongano wa maslahi.

Tukumbuke kuwa zimebakia siku chache kabla ya ripoti hiyo kutolewa baada ya kukamilika kwa muda wake. Licha ya kuwepo kwa ukosoaji dhidi ya muundo wa Tume hiyo, bado ripoti inaweza kuwa chanzo cha mijadala, bila kujali itakavyokuwa imewasilishwa.
Swali zuri sana na jibu rahisi sana.

Hakuna mamlaka ya serikali itakayohusishwa na what transpired on 29th October, 2025. This is because maana zote ziliua kwa makusudi! kwa amri ya Amiri Jeshi Mkuu. Meaning implicating any of those government agencies is IMPLICATING AMIRI JESHI MKUU, WHICH IS STRICTLY FORBIDDEN BY DICTATORIAL REGIMES
 
Back
Top Bottom