Nani atatusaidia kuondoa 'state capture' Tanzania?

Nani atatusaidia kuondoa 'state capture' Tanzania?

SWALI HIVI KWELI Jeshi letu linajielewa vzr kabisa?au kuna changamoto kubwa ndani yake.

Jeshi letu lipo kwa ajili ya kulinda maslahi ya serikali. Ndio maana maandamano yakiitishwa jeshi linatumika kutishia waandamanaji
 
labda simba na yanga zibadilishwe kuwa vyama vya siasa, maana parade ya timu hizi mbili ndo parade pekee kwa tanzania zinazoongoza kukutanisha watu wengi zaidi na sirikali ikawa comfortable, na wakati mwingine inayatumia haya makutano kupenyeza agenda zake, otherwise tusubiri miaka mingine60.

Aiseeh! Simba na Yanga nazo ni janga.
 
Jeshi letu lipo kwa ajili ya kulinda maslahi ya serikali. Ndio maana maandamano yakiitishwa jeshi linatumika kutishia waandamanaji
Sio kwamba polisi hawafahamu sheria au wajibu wao lakini ni kwamba akili zao zimefumbwa na wamekuwa ni lazima wasikilize serikali inoongozwa na chama tawala yataka wao watende vipi kazi zao.

Ndo maana moja ya ushauri wangu mwingine ni kwamba siku mara paap Yesu kashuka basi polisi wote ni lazima wawe na shahada ya kwanza ya chuo kikuu. nasisistiza shahada sio diploma.

Pia polisi ifungue njia kwa wahitimu wa vyuo vikuu mbalimbali kutoka ndani na nje wenye utaalam na ujuzi mbalimbali waingie polisi.

Hapa nilipo sasa hivi mbwa wa polisi wavaa body camera wakienda kumtafuta mhalifu mahala hivyo wafundishwa wakiwa wadogo kutumia body camera na sehemu ya mdomo kuachwa wazi.

Hivyo polisi wahitaji masuala kama uvumbuzi (innovations), teknolojia na maendeleo mengine ya kisayansi ili wafanye kazi zao kisayansi zaidi badala ya kuanza kutafutana na kutekana, kwani hiyo yaonyesha polisi wamekosa majukumu mengine ya kufanya wapo kusubiri orodha ya watekwaji.
 
Tangu lini mihimili ya serikali ya Tanzania ya kawa huru wa kulaumu ni Nyerere ndo chanzo cha siasa za state supremancy
Kati ya walio hai na wafu nani wenye nguvu?
Haiingii akilini kwa mtu aliye hai kumlaumu mfu.
Akili ya kawaida inaonesha kwamba walio hai hupambana wenyewe hata kuuana ili kufanya mabadiliko. Sasa mfu ambaye nguvu na habari yake imekwisha kwa nini alaumiwe?
 
Kwa Sasa Tanzania ipo kwenye Hali ya state capture, baada ya serikali, vyombo vya Dola , mahakama na bunge kuwa kitu kimoja na kuondoa uwajibikaji. Leo bunge limeacha kazi yake ya kuisimamia serikali baadala yake limekuwa rubber stamp ya maamuzi ya serikali. Kwa mfano bunge la Tanzania limetumika kupokea wabunge wasiokuwa na chama au waliofukuzwa kwenye chama chao.

Ila kwa sababu ya state capture bunge linafanya maovu na hakuna wa kuligusa. Bunge kupitia Spika wake wameona suala la wananchi kutekwa sio la msingi kujadiliwa bungeni ila kumpongeza Rais Kwa hotuba yake ndio la muhimu zaidi.

Swali ni je, nani atasaidia tuondokkane na bunge la mchongo lililojaa machawa wa serikali wasiojua majukumu yao?.

Mahakama ndio imeoza kupindukia. Kuna kipindi Jaji Mkuu Ibrahim Juma alisema hadharani ya kwamba majaji watoe hukumu kwa kuangalia falsafa ya serikali.

Yani baadala ya mahakama kuwa huru na kufanya maamuzi stahiki, Jaji Mkuu anashauri majaji waangalie muelekeo wa serikali ni upi.

Jaji Mkuu mwenyewe alitakiwa kustaafu kwa mujibu wa Katiba ila kutokana na state capture aliongezewa muda kinyemela. Ndio maana Rostam Aziz alidai ya kwamba mahakama zetu zinapigiwa simu tu na kutoa maamuzi.

Swali ni nani atawasaidia wananchi waondokane na mahakama mbovu ya Tanzania?

Vyombo vya Dola navyo vinajiendesha under state capture.

Ndio maana mpaka Leo tunajikanyaga kuhusu nani anateka watu na kuwapoteza. Polisi hawajui, TISS hawajui na hata JWTZ hawajui. Sasa nani atawalinda wananchi dhidi ya utekaji . Leo Kuna wananchi jumla ya 89 wamepotezwa mpaka Leo ila kila mtu hajui wapi wapi. Yani raia anaondolewa kwenye basi na kuuawa na hakuna anayewajibika.

Inasikitisha sana. Kutokana na state capture wananchi watazidi kupotezwa na hata kuuawa bila ya msaada. Nani atawasaidia wananchi na huu ukatili?

Serikali imejaa dharau na kebehi. Waziri wa Fedha alifikia sehemu ya kusema asiyeridhika na tozo ya miamala ya simu ahamie Burundi. Kauli za dharau na kiburi maana hakuna wa kumwajibisha. Rais Samia akatoa Lugha ya dharau kwamba wanaotekwa wanajiteka wenyewe.

Na hakuishia hapo akaendelea kudai hata waliouawa kwenye matukio ya utekaji Vifo vyao ni vya kawaida. Yani kwake uhai wa raia ni kawaida tu. Anaongea hivyo maana state capture inamsaidia na hakuna uwajibikaji na hakuna atakalofanywa. Ni nani atatusaidia tuondokkane na Rais mwenye kiburi na dharau Kama huyu?

Leo Tanzania Tume ya Uchaguzi inaweza kuamua kuwapa CCM majimbo yote na hakuna atayeiwajibisha.

Leo watu wanaweza kuamka asubuhi na kwenda kuapishwa bungeni bila kuwa na chama na Wakaaapishwa.

Mimi nadhani Kuna njia nne za kuondokana na huu ufirauni wa state capture nchini Tanzania.

1. Katiba Mpya itakayoweka structures na uwajibikaji. Yani mtu akitekwa hadharani mchana akaenda kuuawa , RPC wa eneo lililotokea utekwaji anawajibika mwenyewe kwa kutochukua hatua. Juzi hapo Kenya IGP Msaidizi alihukumiwa miezi SITA jela kwa kudharau mahakama baada ya raia kupotea bila sababu. Pona yake wale raia wawili waliopotea walipatikana siku hiyo na yeye kuomba msamaha mahakama na kusamehewa.

2. Mass Uprising. Wananchi waanazishe maandamano nchi nzima kushinikiza kuoondka kwa state capture Tanzania. Hii kwa Tanzania itakuwa ngumu mpaka pale kila mmoja atakapoguswa .

3. Second Liberization movement. Hapa ni kuanzisha kikundi Cha uasi kuondoka state capture na kurudisha mamlaka kwa wananchi. Hii njia sio nzuri maana itapelekea vita na mauaji na mambo mengi kurudi nyuma.

4. Kumuomba Mungu afanye miujiza tuondokane na hii laana ya state capture.
Mungu atatusaidia. kwani kipindi cha nyuma nani alitusaidia?
 
Hii nchi inachosha sana, Wananchi wameshaichoka kwa mambo haya

Sasa kama Jaji msomi kabisa na Elimu yake eti anapigiwa simu kutoka juu aamue kesi kwa namna Serikali inavyotaka

Ajabu sana hii
Na ndiyo sababu 2020 watawala walikuwa na jeuri ya kuiba uchaguzi mkuu kwa ujumla wake, maana wanajua hakuna cha kuwafanya.
Hata mkienda mahakamani kudai ni hakuna kitu, kwa kuwa mahakama haipo huru, inaamua wanavyotaka
 
Kumuomba Mungu afanye miujiza tuondokane na hii laana ya state capture.
Hili
.https://www.jamiiforums.com/threads/nusura-ya-tanganyika-ni-anguko-la-ccm.2264411/
 
Kwanza state capture unayosema na umaiti tuliofikia suala la watu kuungana kubadiri mambo sahau kabsa.
Kwa sababu wanaotakiwa kuungana ndo tatizo lenyewe.
Njia pekee imebaki ni
1. Kanuni ya asili ya ubaya.
Ubaya una tabia ya kujivuruga maana ndan yake kuna ulafi na ubinafsi, roho mbaya, fitina na dhulma. Ujinga na upumbavu.
Kuna maslahi ya mmoja yataguswa watanukiana.
2. Kundi dogo sana la wenye maamuzi, weredi na malengo wakiamua kuondoa mmoja mmoja katika wadhalimu.
Wakiwa pamoja katika karamu hakuna wa kuwamudu.
Njia hii huondoa kiini cha tatizo once and for all
Hata hivyo jamii yenyewe ina tatizo kubwa zaidi ndo mana kila mmoja anawaza kuiba kama wao.
 
Sio kwamba polisi hawafahamu sheria au wajibu wao lakini ni kwamba akili zao zimefumbwa na wamekuwa ni lazima wasikilize serikali inoongozwa na chama tawala yataka wao watende vipi kazi zao.

Ndo maana moja ya ushauri wangu mwingine ni kwamba siku mara paap Yesu kashuka basi polisi wote ni lazima wawe na shahada ya kwanza ya chuo kikuu. nasisistiza shahada sio diploma.

Pia polisi ifungue njia kwa wahitimu wa vyuo vikuu mbalimbali kutoka ndani na nje wenye utaalam na ujuzi mbalimbali waingie polisi.

Hapa nilipo sasa hivi mbwa wa polisi wavaa body camera wakienda kumtafuta mhalifu mahala hivyo wafundishwa wakiwa wadogo kutumia body camera na sehemu ya mdomo kuachwa wazi.

Hivyo polisi wahitaji masuala kama uvumbuzi (innovations), teknolojia na maendeleo mengine ya kisayansi ili wafanye kazi zao kisayansi zaidi badala ya kuanza kutafutana na kutekana, kwani hiyo yaonyesha polisi wamekosa majukumu mengine ya kufanya wapo kusubiri orodha ya watekwaji.

Kweli kabisa mkuu, ushauri wako ufanyiwe kazi
 
Kati ya walio hai na wafu nani wenye nguvu?
Haiingii akilini kwa mtu aliye hai kumlaumu mfu.
Akili ya kawaida inaonesha kwamba walio hai hupambana wenyewe hata kuuana ili kufanya mabadiliko. Sasa mfu ambaye nguvu na habari yake imekwisha kwa nini alaumiwe?

Kweli kabisa mkuu. Ni muda wa kuacha lawama na kuangalia reforms zitakazo ipeleka nchi mbele.
 
Na ndiyo sababu 2020 watawala walikuwa na jeuri ya kuiba uchaguzi mkuu kwa ujumla wake, maana wanajua hakuna cha kuwafanya.
Hata mkienda mahakamani kudai ni hakuna kitu, kwa kuwa mahakama haipo huru, inaamua wanavyotaka

Kweli kabisa mkuu. Uchaguzi mkuu wa 2020 ni mfano mzuri wa state capture.
 
Kwanza state capture unayosema na umaiti tuliofikia suala la watu kuungana kubadiri mambo sahau kabsa.
Kwa sababu wanaotakiwa kuungana ndo tatizo lenyewe.
Njia pekee imebaki ni
1. Kanuni ya asili ya ubaya.
Ubaya una tabia ya kujivuruga maana ndan yake kuna ulafi na ubinafsi, roho mbaya, fitina na dhulma. Ujinga na upumbavu.
Kuna maslahi ya mmoja yataguswa watanukiana.
2. Kundi dogo sana la wenye maamuzi, weredi na malengo wakiamua kuondoa mmoja mmoja katika wadhalimu.
Wakiwa pamoja katika karamu hakuna wa kuwamudu.
Njia hii huondoa kiini cha tatizo once and for all
Hata hivyo jamii yenyewe ina tatizo kubwa zaidi ndo mana kila mmoja anawaza kuiba kama wao.

Umeongea hoja ya msingi Sana. Tusubirie asili ichukue mkondo wake.
 
Back
Top Bottom