Nani atawaambia Dola na CCM kwamba wapinzani ni Watanzania

Nani atawaambia Dola na CCM kwamba wapinzani ni Watanzania

Dp800

JF-Expert Member
Joined
Apr 3, 2012
Posts
2,310
Reaction score
4,714
Kuna kila aina ya vitisho na hisia hasi juu ya upinzani na wapinzani.

Mimi ni kijani niliyesomeshwa kwa fedhg za serikali kuanzia sekondari hadi chuo kikuu.

Sioni ubaya wala sina uadui na CCM lakini mtizamo wangu ni kwamba tunahitaji kwa namna moja au nyingine kuongozwa na akili mpya maana watu waliopo ndani ya CCM kuna namna hawana tena ule uzalendo juu ya nchi yetu.

Leo naona ni rahisi kwa mchina maskini au mhindi maskini kufanikiwa Tanzania maana CCM haiamini katika mawazo ya vijana wa Tanzania au mifumo ya rushwa iliyopo ni vigumu kwa vijana wengi kupenya vikwazo hivyo.

Sasa hali na mambo kama hayo yananisukuma kutamani kuona aina nyingine ya utawala katika nchi yetu.

TATIZO NILIONALO
Mifumo yote rasmi ya nchi inayopaswa kutenda kwa usawa mfano
1. Mahakami
2. Viongozi wa Serikali
3. Taasisi za kiusalama (Polisi, TISS, JW etc)

Wote kwa namna moja au nyingine hisia, maneno na mitizamo yaa inayoonekana dhahiri ni kwamba Vyama vya upinzani ni tishio la kiusalama kwa nchi yettu.

Ninajiuliza nini lilikuwa lengo la kuanzishwa kwa vyama vya upinzani ikiwa hawa watu wanahesabika kama maharamia dhidi ya dola na ustawi wa Taifa.

Je? Ni kweli hawa walioapa kulinda na kuitetea katiba hawana ufahamu juu ya uhalali wa vyama vya upinzani kushiriki katika kulisimamia Taifa la Tanzania.

Mtume Paulo aliuza wakati fulani kwamba "Tutapataje kupona?"

Haya maumivu na mateso yanayowapata Chadema ni nani atakaye waponya? Ikiwa Raisi wala hajali, Jaji Mkuu haoni unyama uliifanyika katika mahakama za Tanzania? Usalama wa Taifa, Jeshi la Polisi, Jeshi la Wananchi wote hawa wamenyamaza kwenye uharamia mkubwa wa kupigwa na kuumizwa kwa watanzania hawa ambao pia ni wafuasi na wapenzi wa Chadema?

Wapinzani ni maharamia au ni watanzania wema wenye mawazo tofauti na CCM?

Je ni halali au haramu kuwa mfuasi wa upinzani hususani Chadema?

Haki kwa vyama vya upinzani ni suala la hisani au kwa mujibu wa kanuni na taratabu za nchi yetu tuliojiwekea?
 

Attachments

  • unanweres cries.jpg
    unanweres cries.jpg
    42.5 KB · Views: 31
Back
Top Bottom