Nani Bingwa wako wa Kushoot katika Olimpiki

Lady Whistledown

JF-Expert Member
Joined
Aug 2, 2021
Posts
1,147
Reaction score
2,008
Kati ya Mastaa wa Olimpiki waliotikisa Vichwa vya Habari ni Mturuki Yusuf Dikec na Mkorea Kim Ye-ji katika Mashindano ya Kulenga Bunduki ambao wote walishinda Medali za Fedha

Kim Ye-ji, amekuwa miongoni mwa Wanawake waliovutia Mashabiki wengi, amesifiwa si tu kwa ujuzi wake, bali pia mtindo wake wa Kipekee, akivalia miwani ya kisasa yenye muonekano wa Steampunk na mavazi ya kisasa. Amefananishwa na James Bond na Satoru Gojo, mhusika Maarufu ndani ya Manga Jujutsu Kaisen

Upande mwingine, Picha zilizosambazwa zaidi zinaonyesha Dikec akipiga risasi akiwa amevaa T-shati, mkono mmoja mfukoni, na miwani ya kawaida huku akiwa na uso usioonyesha hisia zozote. Amefananishwa na mtu wa kawaida anayeshindana kwenye Olimpiki, au hata muuaji wa kulipwa


 
Aisee jana niliangalia basketball kati USA na Sudan Kusini si mchezo, Marekani wana mastaa kibao ila walikimbizwa japo sudan alikufa.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…