Asalaam,
Kila uchao maswali yanakuwa mengi bila majibu. Katika mijadala inayoendelea hasa hasa kuhusu bandari na mingine inayoanza kusikika kama TFS, TPDC, etc. Kuna eneo nimejaribu kuangalia kama limeongelewa sijaona. Kelele ni nyingi, uchungu ni mwingi, furaha ni kubwa, vijembe na tambo mbali mbali. Wako wanaolaumu na wanatoa sababu, wako wanao sifia na wanatoa sababu japo hawagusi vifungu ndani ya mkataba. Sasa swali la msingi: Je, NI NANI HASA HASA HUWA ANAFANYA MAAUZI JUU YA MASUALA MAZITO YA KIDOLA KAMA HAYA? Au ni Idara gani katika serikali, katika chama au katika bunge au taaisisi nyingine yoyote ile. Huyu mfanya maamuzi akijulikana akijulikana anaweza kuyafafanua haya.
Nimeona na kusikia haya majadiliano ya juzi akiwemo RA, Zitto, Jenerali na wengine wengi. Nao wamejaa vijembe, masengenyo na lugha tamu lkn kali kwa umma. Sijasikia mtu akihoji aliko mfanya maamuzi ya taifa hili, yaani walioamua na kuanza maongezi na hawa watia saini. Hawa wafanya maamuzi huwa wanamulikwa na kuangaliwa na nani au na chombo gani ili wasipige rushwa? Hicho chombo kama kipo kwanini hakijitokezi kuwasemea na kutetea? Kwanini kwanini kwanini kwanini?
Jambo la Pili
Nani hasa ni mlinzi wa hizi mali na rasilimali za taifa? Kwa kawaida huwa anazilinda kwa kutumia mbinu gani? Huyu mlinzi anasemaje juu ya usalama wa mali hizi, huyu mlinzi huwa analipwa na nani kuzilinda.?
Kwa maswali mengi ya namna hii najiuliza hivi Taifa hili lina yeyote anaelijua? Au lina yeyote anaejua linakoenda? Au bado wavumbuzi wanahangaika kulijua?
Mwisho
Hawa wanaoongea Wanasiasa, wapinga mkataba, Waunga mkono mkataba nani anatumia tumbo na nani anatumia akili? Au wote wako sehemu moja.
Tunendelee kujifunza