Nani hasa anastahili kubeba BALLON D'OR


King Messi
 
modric-alifanya vizuri kwenye world cup na uefa pia kidogo
messi-alifanya vizuri kwenye ligi kuliko wachezaji wa ligi zote
ronaldo-alifanya vizuri kwenye UEFA
Ukiangalia hapo Messi na ronaldo wakipewa hiyo tuzo itakuwa kwa mahaba,anayesitahili ni modric tu
 
Kama Wenger vile
 
Kama wakipewa teena Messi au Ronaldo,basi heshima ya Ballon D'or imeshuka. Hawa watu imefika wakati naona kama wanadhulumu haki za wengine sasa.

L.Modric na A.Griezman.
 
Na wewe una mahaba, mbona humtaji Varane kachukua UEFA na Kombe la dunia, au kisa beki unadhani hana mchango wowote?
 
Mtoa mada anasema UEFA ni ngumu kuliko world cup eti kwa sababu world cup team zinacheza mechi chache kuliko UEFA.

Kwa logic yako basi hata Laliga ni ngumu kuliko UEFA kwa sababu Laliga ina mechi nyingi kuliko UEFA!

Nikirudi kwenye mada, top three ya ballon d'or ni Cristian Ronaldo, Leonel Messi na Luca Modric.

Messi ameshinda Laliga na Copa delrey, pia akawa top scorer laliga na ulaya kwa ujumla akashinda European golden boot. Pia ndie mchezaji mwenye assist nyingi zaidi kwa last season.

Cristian Ronaldo ameshinda champions league na akawa top scorer wa michuano hiyo.

Luca Modric ameshinda champions league na akaiwezesha Croatia kufika fainali ya kombe la dunia kwa mara ya kwanza.

Binafsi naamini Luca Modric anastahili zaidi kupewa hii tuzo kwa sababu ya mchango wake mkubwa kwa madrid kushinda UEFA na kuifikisha Croatia fainali kombe la dunia.

Maana hapa hatuangalii mafanikio ya mchezaji kushinda kombe flani, tunaangalia nani kawa na mchango mkubwa katika mafanikio hayo!

Kwa sababu hizo naamini Luca Modric anastahili.

Kwa wanao sema Griezman au Mbappe au Varane, je hao wachezaji walizibeba team zao kama alivyofanya Modric?

Maana tukisema tu eti ameshinda kombe flani tukumbuke hata Olivier Giroud ameshinda kombe la dunia japo hakupiga hata shuti moja lililolenga goli.

[emoji39][emoji39][emoji39][emoji39][emoji39]
 
Shirikisho la Soka Duniani (FIFA) limetangaza majina 10 ya wachezaji wa kiume wanaowania tuzo ya FIFA ya mchezaji bora wa kiume wa mwaka 2017/18.

Kitu cha kushangaza kwenye orodha hiyo jina la Neymar na Pogba ambao mwaka jana waliingia kwenye orodha hiyo mwaka huu hawajafanikiwa kuingia.

Majina haya yamechujwa kuanzia tarehe 3 Julai 2017 hadi Julai 15, 2018 ambapo tuzo hiyo zitatolewa Septemba 24, 2018 jijini London nchini Uingereza.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…