Mtoa mada anasema UEFA ni ngumu kuliko world cup eti kwa sababu world cup team zinacheza mechi chache kuliko UEFA.
Kwa logic yako basi hata Laliga ni ngumu kuliko UEFA kwa sababu Laliga ina mechi nyingi kuliko UEFA!
Nikirudi kwenye mada, top three ya ballon d'or ni Cristian Ronaldo, Leonel Messi na Luca Modric.
Messi ameshinda Laliga na Copa delrey, pia akawa top scorer laliga na ulaya kwa ujumla akashinda European golden boot. Pia ndie mchezaji mwenye assist nyingi zaidi kwa last season.
Cristian Ronaldo ameshinda champions league na akawa top scorer wa michuano hiyo.
Luca Modric ameshinda champions league na akaiwezesha Croatia kufika fainali ya kombe la dunia kwa mara ya kwanza.
Binafsi naamini Luca Modric anastahili zaidi kupewa hii tuzo kwa sababu ya mchango wake mkubwa kwa madrid kushinda UEFA na kuifikisha Croatia fainali kombe la dunia.
Maana hapa hatuangalii mafanikio ya mchezaji kushinda kombe flani, tunaangalia nani kawa na mchango mkubwa katika mafanikio hayo!
Kwa sababu hizo naamini Luca Modric anastahili.
Kwa wanao sema Griezman au Mbappe au Varane, je hao wachezaji walizibeba team zao kama alivyofanya Modric?
Maana tukisema tu eti ameshinda kombe flani tukumbuke hata Olivier Giroud ameshinda kombe la dunia japo hakupiga hata shuti moja lililolenga goli.
[emoji39][emoji39][emoji39][emoji39][emoji39]