Nani hununua vitu vya watu mashuhuri wa Tanzania?

Allen Kilewella

JF-Expert Member
Joined
Sep 30, 2011
Posts
21,470
Reaction score
40,593
Kwenye nchi za Ulaya na Marekani ni ufahari mtu kununua kitu chochote kile kilichotumiwa au kumilikiwa na mtu maarufu ama mashuhuri kwa bei kubwa sana na kuhifadhi kwenye majumba yao.

Lakini ni nani kwa mfano kwa sasa anamiliki kiatu alichovaa Steven Kanumba saa chache kabla ya kufariki kwake. Hivi nguo alizovaa Diamond wakati wa ku - shoot wimbo wa Mbagala ziko wapi kwa sasa.

Nani anajua Gitaa la Mbaraka Mwinshehe lilipo kwa sasa ama mashahiri ya wimbo wa "Dada Asha" yaliyoandikwa kwa mkono na Shemu Kalenga mwenyewe nani anayo? Vitu gani alivyokuwa anamiliki Shaabani Robert wakati wa kufanya kazi zake za fasihi bado vipo na vipo kwa nani?

Jee utamaduni wa kununua vitu vya watu mashuhuri na Maarufu unaweza kuwepo hapa kwetu Tanzania?
 
Acha uhuni wewe ...hizo sio mila zetu sisi wa afrika ... Nani akatowe mamilioni kununua uchafu wa secondhand ... Ayo ni mambo ya wazungu ....
Uwe na heshima unapochangia ama kujibu hoja za wengine. Mila za kiafrika ni zipi na unajua zilianzaje? Jee ni mila zetu kuanza mahusiano kabla ya ndoa, ni mila yetu kubusiana hadharani, ni mila yetu kukataa mchumba uliyechaguliwa na wazazi, ni mila yetu kuwa wavivu na ni mila yetu kusema uongo?

Mambo ya kufanya uzamani ndiyo mila za Kiafrika ni kujikosea sisi wenyewe!!
 
Acha uhuni wewe ...hizo sio mila zetu sisi wa afrika ... Nani akatowe mamilioni kununua uchafu wa secondhand ... Ayo ni mambo ya wazungu ....
Sio vya mamilion tu!
Bongo hakuna mashabiki ila mashabiki maandazi!!

Iko wapi wasafi.com?
Zile nyimbo zilikua zinauzwa mamilion?

Si ilipoanza nyimbo zao ilikua hakuna kuweka kwenye free website?
ila Sasa je?
 
Nadhani huku kwetu hatuna hela ya kufanya kitu too luxirious kama hicho, kipato tulucho nacho kinatosheleza mambo ya msingi tu
Ngushi kaleta hoja ya msingi. si lazima viwe vya mamilioni hata vya bei ya kawaida hatununui. Utasikia kununua kinyago cha Kimakonde ni anasa, lakini tuko bize kila siku kununua midoli toka ulaya!!
 
Hii ni moja ya sababu za msingi, unafikiri nani anunue mashairi kwa gharama eti kisa tu yameandikwa kwa mkono?

Mwafrika hana pesa ya kununua kitu kwa pesa ndefu ikiwa kitu hicho hakitumii.
 
Inanikumbusha Marlo Stansfiled kwenye series ya The Wire....mchizi kawachana wehu fulani hivi:

-I dont need those SENTIMENTAL VALUE shit,I need its REAL VALUE!

Mambo ya vitu sijui vya watu mashuhuri sijui nini ni Sentimental Value ambazo ni value za kufikirika!

Sisi tunataka Real Value mzee!
 
Mwafrika hana pesa ya kununua kitu kwa pesa ndefu ikiwa kitu hicho hakitumii.
Hata kuhifadhi nako ni kutumia. Leo wazungu na waaarabu wanaweza kutaja historia za koo zao hata vizazi vitano nyuma, sisi siku hizi unakuta mtu hata bibi aliyemzaa babu yake hajui jina lake!
 
Kwenye nchi za Ulaya na Marekani ni ufahari mtu kununua kitu chochote kile kilichotumiwa au kumilikiwa na mtu maarufu ama mashuhuri kwa bei kubwa sana na kuhifadhi kwenye majumba yao.

Lakini ni nani kwa mfano kwa sasa anamiliki kiatu alichovaa Steven Kanumba saa chache kabla ya kufariki kwake. Hivi nguo alizovaa Diamond wakati wa ku - shoot wimbo wa Mbagala ziko wapi kwa sasa.

Nani anajua Gitaa la Mbaraka Mwinshehe lilipo kwa sasa ama mashahiri ya wimbo wa "Dada Asha" yaliyoandikwa kwa mkono na Shemu Kalenga mwenyewe nani anayo? Vitu gani alivyokuwa anamiliki Shaabani Robert wakati wa kufanya kazi zake za fasihi bado vipo na vipo kwa nani?

Jee utamaduni wa kununua vitu vya watu mashuhuri na Maarufu unaweza kuwepo hapa kwetu Tanzania?
Nathani hili ni wazo zuri hata la kuanzisha Makumbusho ya Vitu kama hivyo halafu watu wakawa wanatembelea na mtu kujipatia kipato.
 
Back
Top Bottom