Ukisoma ninachoandika kabla kuandika kwa kudhani unajibu nilichoandika kumbe sikuandika ivo, utanielewa. Kwanza sijasema mahali popote pale kwamba mashairi yana thamani kuliko dhahabu na sijabisha kwamba dhahabu inatumika dunia nzima kupima utajiri wa serikali na nchi ambao ndio huamua thamani ya fedha ya nchi husika.
Lakini ninachosema ni kwamba kwangu mimi nikiwa na hela halafu kukawa na dhahabu mbele yangu na shairi lililoandikwa kwa mkono wa Shaaban Robert, basi mimi nitanunua shairi badala ya dhahabu.
View attachment 886370
Hizi ndio zilikuwa fedha za zama hizo, wakati huo zilikuwa na thamani kuliko dhahabu. Kwa uchumi wa sasa hata Marekani imeacha kutumia dhahabu kama kipimo kinachoamua thamani ya Dola yao. Marekani wanadai dola zilizoko mtaani wenyewe wakizirudisha kwenye Benki Kuu yao hakuna dhahabu ya kulingana thamani na dola walizo nazo.
Kidunia dhahabu ina thamani kubwa sana kuliko Mashairi ya Shaaban Robert!!