Nani hununua vitu vya watu mashuhuri wa Tanzania?

Lakini ninachosema ni kwamba kwangu mimi nikiwa na hela halafu kukawa na dhahabu mbele yangu na shairi lililoandikwa kwa mkono wa Shaaban Robert, basi mimi nitanunua shairi badala ya dhahabu.
wengi hawaelewi na hawajawahi kuweka thamani katika maneno na kazi za sanaa kama mashairi ni kwa kiasi gani yanaweza kuleta hamasa na mabadiliko katika jamii na uchumi kwa ujumla na ndo maana hawawezi elewa na wengi tunapenda kuchukua vitu kimzahamzaha tu tukifikiri tunaelewa.
siku moja nilikuwa namuuliza abiria mwenzangu kuwa anajua shilingi 500/- inapicha gani mbele na nyuma, hakuwa na jibu kisha tukamuuliza konda ambaye anazishika kila wakati naye hakuwa na jibu la uhakika mpaka alipoangalia na abiria wengi waliingia katika huo mjadala kwa kutokuwa wadadisi hata kwa vitu vidogo sasa ukimwambia mtu shairi lina thamani hawezi elewa lakini tuangalie lile shairi tu maarufu la kama tunataka mali tutaipata shambani kwa waliolifuatilia na kama lingetumika kama kauli mbiu lingeleta mageuzi makubwa kwa kilimo.
lakini ni msukuma mkokoteni aliyeandika mkokoteni wake mtaji wa maskini ni nguvu zake mwenyewe na Mkapa kwa kuthamini maneno yale alimlipa yule msukuma mkokoteni kwa kazi nzuri na leo ndio tunaona walioelwa walijitahidi kujituma na kufanya kazi.
hivyo tuanze taratibu tutafika japo kwa kuchelewa.
 
Alisema masanja hela izungukage humo humo kwenye ukoo[emoji23] [emoji23] [emoji23]

Ingawa ukiacha hilo mwamko kwa Wabongo kununua kazi za wasanii wetu ni mdogo sana!

Diamond awe makini kama akileta hayo Hata kwenye TV Na radio haitakua poa!
Anatakiwa kuangalia uwezo na siyo kufahamiana ohoo atakwisha
 
Kwan wahusika,warithi au wamiliki wameamua kuviuza? Labda waamue tunaweza kujaribu
 
Anazungumzia kina Wolper,Irene,Tunda Castro,Sister Fay,Giggy Money,Ferouz,Daz Mwalimu,Afande sele etc
Ha ha ha... Hivi kuna mtu mwenye akili timamu atanunua kutoka kwa hawa watu? Hata hivyo, hakuna aliye mashuhuri miongoni mwao, labda maarufu kidole (locally) huku wakiishi maisha ya kuigiza...

Kwa kifupi mtu mashuhuri ni prominent na maarufu ni popular..

Watu mashuhuri ni watu wenye kufanya jambo kubwa katika jamii au la heshima ya hali ya juu, kama viongozi, wakiweemo mawaziri, maraisi n.k., pia utawakuta wafanyabiashara, wanasayansi, waandishi, wagunduzi n.k...
 
Director umeongea vitu vya Msingi sana,ni kweli Hao ndio watu wanapaswa vitu vyao kununuliwa au kwekwa makumbusho na sio watu maarufu anaozungumzia mtoa mada.
 
Watu mashuhuri ni watu wenye kufanya jambo kubwa katika jamii au la heshima ya hali ya juu, kama viongozi, wakiweemo mawaziri, maraisi n.k., pia utawakuta wafanyabiashara, wanasayansi, waandishi, wagunduzi n.k...
Ni kosa kudhani kwamba wasanii hawana mchango kwenye kuibadili jamii na kuchangia maendeleo yake. Ni kosa kubwa sana kudhani ni wanasayansi, wafanyabiashara na wanasiasa pekee ndiyo wanakuwa na sifa ya "Prominent Figure" kwenye jamii.
 
Aah mwishowe nirithi majini buree!!
"chako chako, changu changu "
 
Ka kimya wew
 
Acha uhuni wewe ...hizo sio mila zetu sisi wa afrika ... Nani akatowe mamilioni kununua uchafu wa secondhand ... Ayo ni mambo ya wazungu ....
Umeniwahi mkuu ,huyu ni limbukeni eti kwa kuwa wanafanya hivyo Marekani na Ulaya basi nasi tufanye ,mwishowe atadai mbona hatuna ndoa za jinsia moja kama Ulaya na marekani,basi awaambie huko Marekani na Ulaya wanawake hawanyonyeshi hadharani kama Afrika na kwanini hawafanyi hivyo.
 
Umeona mkuu ..kuna watu wanataka tuige mauchafu yote ya kizungu.
 
tatizo wabongo zana zao za kazi zote huzipitisha kwa babu kufukiza ndumba, hivyo ni mwiko kwao kuuza tunguri zao na ni uchuro kwetu kununua vitu vyao vilovyo rogwa marogo mazito mazito
 
Ni kosa kudhani kwamba wasanii hawana mchango kwenye kuibadili jamii na kuchangia maendeleo yake. Ni kosa kubwa sana kudhani ni wanasayansi, wafanyabiashara na wanasiasa pekee ndiyo wanakuwa na sifa ya "Prominent Figure" kwenye jamii.
Usikurupuke, ulitakiwa kwanza kuelewa nilichoandika kabla hujachangia. Nimesema watu mashuhuri ni wale waliofanya mambo makubwa au yenye heshima kwa jamii. Kuwa msanii au mtu maarufu tu (maana umaarufu inategemea umeupataje, unaweza kuwa mwizi maarufu, changudoa maarufu, kichaa maarufu, mama ntilie maarufu etc.) hakukufanyi wewe kuwa mashuhuri. Je, umetoa mchango gani kwenye jamii?...
 
Bishop Hiluka kwenye bandiko lako hukuandika hata mtu mmoja wa sanaa kwenye hao watu mashuhuri, ivo moja kwa moja nikatafsiri kwamba wewe huamini kwamba na wasanii pia wanaweza kuwa watu mashuhuri. mfianchi na bestmale wapi nimeandika kwamba tunatakiwa kuiga "kila" mauchafu ya wazungu? Mifumo ya maisha yetu ya sasa hauna huo uafrika mnaojifanya kuupigania. HIvi uafrika ni nini na mila zake ni zipi?
 

mimi nauza boska yangu sijafuwa mwaka wa tano.dau laki mbili
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…