Nani kama Nyerere? hakika tutamkumbuka sana huyu mzee!

Nani kama Nyerere? hakika tutamkumbuka sana huyu mzee!

attachment.php
 
Range Rover za wakati huo hazikuwa as comfortable as za siku hizi, hivyo bado hiyo 109 ilikuwa ni nzuri zaidi. Pia, kipindi hicho uchumi wetu haukuweza kumudu zaidi ya hapo, leo hii uchumi wetu ni mkubwa zaidi mara 100 zaidi ya ule enzi za Mwl. Hivyo, hatuwezi kuwa na uchumi uliokuwa halafu tukaishi kama vile uchumi umedumaa. Kama ingekuwa hivyo basi hata Obama angetumia corolla!
Diga Diga unataka kumaanisha nini kwenye hoja yako hii? Ni kweli Range Rover iliwahi kuwa kwenye kiwango cha chini kuliko Land Rover 109? Kweli uchumi wetu umekuwa kwa asilimia 100 zaidi kuliko ulivyokuwa miaka ya Mwalimu, wewe unaona kukua huko kwa uchumi?
 
Last edited by a moderator:
Pamoja na mapungufu yake, lakini ukweli unabaki palepale kwamba HAKUNA kiongozi Tanganyika mwenye sifa za kipekee za utumishi wa kuwajali wengine kama Nyerere.
 
Pengine kabla ya kuingia kwenye mjadala kati yangu na wewe, ni vema nikajua ulizaliwa lini? Inawezekana ulizaliwa baada ya kurejeshwa mfumo wa vyama vingi. Kama hivyo ndivyo, nitakuwa napoteza nguvu zangu bure. Je, unajua enzi hizo Range Rover hazirukuruhisiwa kuegeshwa benki?
I am old enough to be called grandpa!
 
Range Rover za wakati huo hazikuwa as comfortable as za siku hizi, hivyo bado hiyo 109 ilikuwa ni nzuri zaidi. Pia, kipindi hicho uchumi wetu haukuweza kumudu zaidi ya hapo, leo hii uchumi wetu ni mkubwa zaidi mara 100 zaidi ya ule enzi za Mwl. Hivyo, hatuwezi kuwa na uchumi uliokuwa halafu tukaishi kama vile uchumi umedumaa. Kama ingekuwa hivyo basi hata Obama angetumia corolla!
Kwa hiyo hiyo 109 ilikuwa comfortable kuliko Range rover za wakati huo? Ni kweli kabisa uchumi wetu umekua sana, ndiyo maana hata Mkapa akaamua kuachana na lile Fokker la enzi za mwalimu na kuchukua kitu Gulf Stream linaloogopa vumbi la viwanja vyetu.
 
Range Rover za wakati huo hazikuwa as comfortable as za siku hizi, hivyo bado hiyo 109 ilikuwa ni nzuri zaidi. Pia, kipindi hicho uchumi wetu haukuweza kumudu zaidi ya hapo, leo hii uchumi wetu ni mkubwa zaidi mara 100 zaidi ya ule enzi za Mwl. Hivyo, hatuwezi kuwa na uchumi uliokuwa halafu tukaishi kama vile uchumi umedumaa. Kama ingekuwa hivyo basi hata Obama angetumia corolla!

Nchi wahisani wanashangaa magari viongozi wetu wanayotumia wanakataa nchi hii siyo maskini, so mirija inaanza kuzibwa, unafikiri huu mkakati serikali inaouanzisha kupunguza magari ya kifahari kutoka kwa baadhi ya kada wameupenda?
 
Diga Diga unataka kumaanisha nini kwenye hoja yako hii? Ni kweli Range Rover iliwahi kuwa kwenye kiwango cha chini kuliko Land Rover 109? Kweli uchumi wetu umekuwa kwa asilimia 100 zaidi kuliko ulivyokuwa miaka ya Mwalimu, wewe unaona kukua huko kwa uchumi?
Kwahiyo wewe unataka kusema uchumi wetu kwa leo bado uko vile vile sawa na enzi za Mwl? Huwezi kuona kirahisi tangible effects za uchumi kwa mtu mmoja mmoja kwani idadi ya wananchi nayo inaongezeka. Au napo bado tuko vile vile kama enzi za Mwl?
 
Watanzania bana,

Kumbuka kuwa Dunia inabadilika kwa maana kuwa hata maisha pia yanabadilika. Harafu kumbuka kipindi hicho, hakukuwepo na uhuru wa habari na tekinologia ya juu kama sasa.

Hujui kama kuna benzi la bei mbaya ambalo Mwalimu Nyerere alikuwa akilitumia pale ikulu?

Siasa na maisha ya Mwalimu Nyerere vilijengwa kwa propoganda ya hali ya juu ndiyo maana hata photo ziko very selective, wakati viongozi wetu kwa sasa siasa na maisha yao yanawekwa wazi katika jamii kwa kila mwananchi kujionea na kuchagua kwa maamuzi yasiyo na shinikizo la propaganda wala mawazo kandamizi.

He was good but not that good the way some people try to portlay him. Hata hivyo siasa zake ziligonga mwamba na akaamua kuchanja mbuga.
 
Mwalimu kwa sasa kama unamlinganisha na binadamu aliye hai basi atakuwa Mandela (Madiba) baada ya hapo hatuna viongozi tuna mabwana watawala tu wasiowatakia mema wananchi wao duniani
 
Range Rover za wakati huo hazikuwa as comfortable as za siku hizi, hivyo bado hiyo 109 ilikuwa ni nzuri zaidi. Pia, kipindi hicho uchumi wetu haukuweza kumudu zaidi ya hapo, leo hii uchumi wetu ni mkubwa zaidi mara 100 zaidi ya ule enzi za Mwl. Hivyo, hatuwezi kuwa na uchumi uliokuwa halafu tukaishi kama vile uchumi umedumaa. Kama ingekuwa hivyo basi hata Obama angetumia corolla!
ACHA UWONGO, kuanzia lini Range ikazidiwa na 109 kwa confortability?
NELSON MANDELA:-
We arrived in Dar es Salaam the next day and I met with Julius Nyerere, the newly independent country’s first president. We talked at his house,
which was not at all grand, and I recall that he drove himself in a simple car, a little Austin. This impressed me, for it suggested that he was a man of
the people. Class, Nyerere always insisted, was alien to Africa; socialism indigenous
Long Walk to Freedom
 
Mkuu Diga Diga kumbuka hilo gari lilikuwa likitumiwa huko Mafia council !.

Range Rover za wakati huo hazikuwa as comfortable as za siku hizi, hivyo bado hiyo 109 ilikuwa ni nzuri zaidi. Pia, kipindi hicho uchumi wetu haukuweza kumudu zaidi ya hapo, leo hii uchumi wetu ni mkubwa zaidi mara 100 zaidi ya ule enzi za Mwl. Hivyo, hatuwezi kuwa na uchumi uliokuwa halafu tukaishi kama vile uchumi umedumaa. Kama ingekuwa hivyo basi hata Obama angetumia corolla!
 
Last edited by a moderator:
Kwahiyo wewe unataka kusema uchumi wetu kwa leo bado uko vile vile sawa na enzi za Mwl? Huwezi kuona kirahisi tangible effects za uchumi kwa mtu mmoja mmoja kwani idadi ya wananchi nayo inaongezeka. Au napo bado tuko vile vile kama enzi za Mwl?
Ukuaji wa uchumi kwako unamaanisha nini? Haya maghorofa yaliyotapakaa ambayo watu wa Manzese kwa Mfuga Mbwa hawawezi kuyatumia wala hayaongezi mlo au ubora wa mlo wenyewe kwao!! Njoo huku useme kwamba uchumi umekuwa kuliko enzi za Mwalimu uone vita yake!!
 
Tatizo kubwa ni kwamba unapokuwa na serikali ya chama kimoja na ambayo katiba ya nchi imempa madaraka makubwa Raisi na pia katiba hiyo imefuta haki za binadamu kwenye katiba. Pia nchi nzima inasikiliza redio moja, magazeti wawili la chama na Serikali.Pia vyama vya wafanyakazi ni sehemu ya taasisi za Chama na chama kimeshika hatamu.Kwaiyo kila watu wanaimba sifa za huyo mtu.Hii katika propaganda ni kupandikiza uzuri bila kusikiliza upande mwingine na hii ndiyo inafanyika hata Korea Kaskazini hadi sasa na Nerere aliwafanyia hivyo watanzania. Kwaiyo sifa za Nyerere zimekuzwa sana na watu walioishi kipindi hicho cha kuimba na kusifu bila kutoa nafasi kwa watu wengine kukosoa. Ndio maana mambo mengi ya aliyoamini Nyerere hayakufanikiwa. Ukikosana nae hukuruhusiwa kutamba either ukimbie nchi au uende gerezani. Muulizeni Oscar Kambona.
 
Watanzania bana,

Kumbuka kuwa Dunia inabadilika kwa maana kuwa hata maisha pia yanabadilika. Harafu kumbuka kipindi hicho, hakukuwepo na uhuru wa habari na tekinologia ya juu kama sasa.

Hujui kama kuna benzi la bei mbaya ambalo Mwalimu Nyerere alikuwa akilitumia pale ikulu?

Siasa na maisha ya Mwalimu Nyerere vilijengwa kwa propoganda ya hali ya juu ndiyo maana hata photo ziko very selective, wakati viongozi wetu kwa sasa siasa na maisha yao yanawekwa wazi katika jamii kwa kila mwananchi kujionea na kuchagua kwa maamuzi yasiyo na shinikizo la propaganda wala mawazo kandamizi.

He was good but not that good the way some people try to portlay him. Hata hivyo siasa zake ziligonga mwamba na akaamua kuchanja mbuga.

Acheni unafiki nyie.
Akiwa ikulu Nyerere hakuwahi kutumia Mercedes Benz. Ukienda makumbusho ya taifa pale mtaa wa Shabaan Robert utayakuta magari yote aliyoyatumia toka enzi za kupigania uhuru (Dennis, RR, Austin etc). Gari alilolitumia kwa mda mrefu ni RR ya kifahari ambayo kwa maelezo ya makumbusho ilitolewa na malkia wa uingereza kama zawadi kwa kiongozi wa nchi mwaka 1966 na hasa alilitumia kwenda airpot kupokea wageni wa kitaifa na lilikuwa na uwezo wa kuchua yeye, mgeni wake na mwandishi wake wa habari. RR (Rolls Royce) pia ilitumiwa na Mwinyi pamoja na Mkapa mpaka 2003 Mkapa alipoamua kuipeleka pale makumbusho.

Benz pekee alilotumia mwalimu ni lile alilonunuliwa na serikali miaka ya 90 kwa ajili ya kumpeleka mahali popote anapoenda akapewa na dereva pia, hata ukienda pale makumbusho nalo utalikuta na bado liko katika hali nzuri kabisa na halina tofauti na haya ya kisasa.

Kabla hujablaff haba nenda kafanye utafiti.
 
Alipostaafu tu Urais mwaka 1985 hadi leo,Tanzania si nchi yenye maadili tena kuanzia serikalini hadi mitaani,mzee huyu alistaafu akiliachia taifa uchumi mzuri sambamba na pesa yenye thamani kubwa,noti ya mwisho ikiwa ni 100,enzi zile hata cent zilifanya kazi,taifa lilikuwa na viwanda vingi,serikali iliogopwa na kila mtu,hakuna aliyekuwa akienda ikulu hovyo kama wafanyavyo matajiri siku hizi,leo hii ikulu pamekuwa sehemu ya matajiri kuonana na rais kila mara watakavyo,makampuni makubwa ya kigeni kama BARRICK yamekuwa yakiwanyanyasa wazawa bila serikali kuweka zuio lolote,watu wanafanya biashara ya pesa bila leseni,nani wa kuwagusa? mzee huyu hakuwa mwanachama wa ccm,bali alikuwa mwanachama wa Tanzania,ndo maana hakuwahi hata siku moja kuvaa sare za ccm,matajiri wote enzi zile walifyata mkia kwa serikali,ccm hii ya leo ni maiti inayohangaikia uzima,wameua viwanda vyote,halafu wanasema "we shall create 1mil job posts".zitatoka wapi? waliojiajiri mnavuruga biashara zao,NANI KAMA NYERERE? PUMZIKA BABA YETU.
 
Utamkumbuka peke yako, ivi yuko motoni uko anakula marungu ya moto!
 
Nyerere alikuwa Rais wa mfano Duniani. Namuona Dr slaa anaweza kufanana na Nyerere kama atapata nafasi ya kugombea anaweza kutuvusha hapa tulipo kwa sasa.

Fikiria daftari la wapiga kura linafutwa lote na kuandikisha upya na tsh bil.293 zitatumika kuandikisha kwenye mfumo mpya wa BVR.

Kwa nini wasingeandikisha walio poteza na wale wapya ili pesa zingine ziende kwenye maendeleo hasa maji na miundo mbinu.RIP Nyerere
 
Tatizo kuwa aliuwa kabisa kale kambegu ka ujasiriamali hasa kwa wazawa, ndio maana na matokeo yake mikataba FAKE ya kitaifa sababu watu hawana ujasiriamali wanajua matumizi na 10% kwao kubwa sana, hawajui NEGOTIATION, Tatu kubwa sana alipanua midomo ya watanzania kelele nyingi sana kazi hakuna sababu ana HAKI, HATIMAYE UMASKINI MKUBWA PIA HAKUPENDA WATU WAELIMIKE ILI AWATAWALE VEMA

FAIDA : UMOJA, AMANI, MAWASILIANO-KISWAHILI, MAADILI KIJAMII, MAADILI YA UONGOZI JAPO PIA RUSHWA ILIKUWEPO
 
Back
Top Bottom